MAFUNZO YA AWALI JESHI LA AKIBA WILAYA YA CHEMBA YAMALIZIKA

  Masama Blog      
Mkuu wa Wilaya ya Chemba Mhe.Simon Odunga awapongeza wazazi wa wilaya ya Chemba kwa kuonyesha ushirikiano kwa kuwaruhusu watoto wao kushiriki katika Mafunzo ya Jeshi la Akiba na ikumbukwe kuwa mzalendo ni pamoja na kutumikia nchi yako hata kwenye ulinzi na usalama wa Taifa. 

Mhe. Simon Odunga aliyazungumza hayo alipokuwa anafunga rasmi Mafunzo ya Jeshi la Akiba kundi la kumi yaliyomalizika Tarehe , 23/11/2019 katika viwanja vya shule ya msingi Chemba. 

“Jamii inapaswa itambue kazi ya Mgambo mtu yoyote anaweza kuifanya awe mtu wa hali ya chini au juu anaweza kupata Mafunzo, kwani lengo hasa ni kujenga utimamu wa mwili,uzalendo ili kutumikia taifa lao”aliongeza kwa kusema hivyo Mhe.Simon Odunga. 

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Chemba Dkt.Semistatus H.Mashimba amefurahishwa kwa wito wa vijana kushiriki kwenye Mafunzo, inaonyesha dhahili kuwa wilaya ya Chemba inakuwa kimaendeleo na ameahidi wanafunzi waliohitimu mafunzo atafanya nao kazi kwa ushirikiano. 

Meja wa Wilaya ya Chemba Joseph Narsis amesema Mafunzo hayo yalianza Tarehe, 1/7/2019 na kumalizika 23/11/2019 ,walianza na wanafunzi 72 na kumalizika wanafunzi 52 ,wanawake 9 ,wanaume 43,changamoto zilikuwepo ikiwemo baadhi yao kutoona umuhimu wa mafunzo hayo na kukatishana tama lakini waliweza kukabiliana nazo paka kuweza kukamilisha Mafunzo hayo.from MICHUZI BLOG https://ift.tt/35uqZKe
via
logoblog

Thanks for reading MAFUNZO YA AWALI JESHI LA AKIBA WILAYA YA CHEMBA YAMALIZIKA

Previous
« Prev Post