KORTI YAAHIRISHA KESI YA UHUJUMU UCHUMI INAYOMAKABILI MWANDISHI WA HABARI ZA UCHUNGUZI ERICK KABENDERA

  Masama Blog      
Na Karama Kenyunko, globu ya jamii.

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imeahirisha kesi ya Uhujumu Uchumi inayomkabili Mwandishi wa Habari za uchunguzi, Erick Kabendera hadi Novemba 20, mwaka huu kufuatia upande wa Mashtaka kudai upelelezi wa shauri hilo bado haujakamilika.

Katika kesi hiyo, Kabendera anakabiliwa na mashtaka matatu likiwemo la utakatishaji wa zaidi ya sh milioni 173.

Wakili wa serikali Mwandamizi, Wankyo Simon amedai mbele ya Hakimu Mkazi, Vicky Mwaikambo kuwa Kesi hiyo leo Novemba 7, ilipangwa kwa ajili kutajwa, upelelezi wake bado haujakamilika pia Hakimu Mkazi Mwandamizi, Augustine Rwizile aliyekuwa  akisikiliza kesi hiyo ameteuliwa kuwa jaji wa Mahakama Kuu hivyo ameiomba mahakama kuahirisha kesi hiyo wakati ikisubiri ipangiwe Hakimu mwingine wa kuendelea kuisikiliza.

Baada ya kusikiliza hoja hiyo, Hakimu Mwaikambo ameahirisha kesi hiyo hadi Novemba 20, mwaka huu kwa ajili ya kutajwa.

Katika shtaka la kwanza, Kabendera anadaiwa kujihusisha na mtandao wa kihalifu kwa kutoa msaada kwa genge la uhalifu kwa nia ya kujipatia faida.

Pia anadaiwa kuwa bila ya sababu, alikwepa kodi ya Sh 173,247,047.02 ambayo ilitakiwa ilipwe kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

Katika shtaka la tatu, kabendera anadaiwa kutakaisha Sh 173,247047.02 huku akijua fedha hizo ni mazalia ya kosa la kujihusisha na genge la uhalifu na utakatishaji fedha.from MICHUZI BLOG https://ift.tt/34CzBy0
via
logoblog

Thanks for reading KORTI YAAHIRISHA KESI YA UHUJUMU UCHUMI INAYOMAKABILI MWANDISHI WA HABARI ZA UCHUNGUZI ERICK KABENDERA

Previous
« Prev Post