Ticker

10/recent/ticker-posts

KOCHA MKUU TAIFA STARS ATAJA MAMBO MATATU TANZANIA KUFANIKIWA KATIKA SOKA

Kocha Mkuu wa Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' Etienne Ndayiragije

Na Said Mwishehe, Michuzi Blogu
KOCHA Mkuu wa Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' Etienne Ndayiragije ametaja mambo matatu ya kufuatwa iwapo tunahitaji kuinua soka letu nchini.

Akizungumza jijini Dar es Salaam Kocha Ndayiragije ameeleza kwa kina mambo ya msingi ambayo nchi yetu inatakiwa kufanya ambayo ni kuwekeza katika soka la vijana, pili viwanja vizuri vya soka na tatu kila mdau wa soka atimiwe wajibu wake.

Akifafanua zaidi amesema kuwa ili kuwa na timu nzuri kwenye vilabu vya Tanzania na kukuza soka, ni vema eneo la kuweka kwa vijana likapewa kipaumbele kwani ndioko ambako wachezaji wazuri wanaandaliwa vya kutosha na hatimaye kupata timu bora kwa ajili ya michuano ya kimataifa.

Kuhsuu viwanja vizuri, Kocha huyo amesema ili kuwa na wachezaji wazuri na walioandaliwa lazima wapate viwanja vilivyokuwa na viwango vya soka."Uzuri wa kiwanja cha soka ni eneo muhimu sana, hivyo ni vema kwa vilabu vya soka nchini Tanzania kuona ni namna gani wanaweza kuwa na viwanja vizuri kwa kushirikiana na wadau wengine wa soka.Kwangu ubora wa kiwanja ni jambo muhimu katika kukuza soka la nchi husika."

Pia amesema jambo la tatu ili kufanikiwa katika soka ni kuhakikisha wadau na wapenda soka wanatimiza wajibu wao kikamilifu ambapo amesema waandishi wa habari za michezo na wachambuzi wa soka wanatakiwa kutimiza wajibu wao, Shirikisho la Mpira wa Miguu nao watimize wajibu wao na makocha nao wafanye kazi yao kikamilifu.

"Kila mmoja akitimiza majukumu yake nina uhakika tutapiga hatua sana katika medani ya soka.Hivyo nishauri kila mmoja awe na jukumu la kuhakikisha anakuwa sehemu ya kufanikisha wajibu wake kwa ajili ya nchi,"amesema Kocha Ndayiragije.

Hata hivyo ametumia nafasi hiyo kueleza katika kazi yake ya ukocha amefundisha katika nchi tisa za Bara la Afrika lakini alichobaini Tanzania kuna vipaji vya hali ya juu vya soka, hivyo kikubwa ni kuwekwa mikakati thabiti kuendeleza vipaji hivyo.

Pamoja na uwepo wa vipaji vya soka, ameonesha hofu kutokana na vilabu vingi kukosa uwezo wa kutosha katika kuendeleza vipaji hivyo akitoa mfano kuwa mchezaji anaweza kuwa na kipaji na yuko katika klabu ambayo haina uwezo mkubwa kifedha, hivyo ikitokea klabu yenye uwezo inamchukua na akifka hapati nafasi, hivyo matokeo yake kipaji kinapotea.


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/33fXoUl
via

Post a Comment

0 Comments