Ticker

10/recent/ticker-posts

KILIMANJARO SAR YATOA MAFUNZO YA HUDUMA YA KWANZA KWA WAONGOZA WATALII ZAIDI YA 500.

Mtaalamu wa huduma ya kwanza kwa Magonjwa ya Mlima kutoka kampuni ya Utafutaji na Uokoaji ya Kilimanjaro SAR, Paul Gloy akionesha waongoza watalli namna ambavyo unaweza okoa maisha ya mtu aliyepata changamoto akiwa katika muinuko .
Mtaalamu wa Magonjwa ya Dharura na Uokoaji kutoka kampuni ya Kilimanjaro SAR,Dkt Hussein Abrodha akizungumza wakati akitoa mafunzo kwa waongoza watalii jijini Arusha. 
Baadhi ya Waongoza Watalii wakifuatilia mafunzo katika ukumbi wa mikutano wa hotel ya Rose Garden jijini Arusha .
 Mtaalamu wa Masoko wa Kampuni ya Utafutaji na uokoaji ya Kilimanjaro SAR ,akizungumza wakati wa mafunzo hayo.
Baadhi ya Washiriki 
Mtaalamu wa Huduma ya Kwanza wa Kampuni ya Kilimanjaro SAR ,Paul Gloy akiwalekeza waongoza Watalii namna ya kumhudumia mtu aliyepata changamoto ya kuvunjika Mguu.
Baada ya kupata mafunzo kutoka kwa Wataalamu wa Kampuni ya Utafutaji na Uokoaji ya Kilimanjaro ,Waongoza Watalii wakionesha namna ya kumhudumia mtu aliyepata changamoto ya kuvunjika uti wa mgongo .
Waongoza Watalii wakionesha namna ay kumuhudumia mtu aliyepatwa na Changamoto ya kuvunjika Mguu. 
Mtaalamu wa Magonjwa ya Dharura na Uokoaji kutoka Kilimanjaro SAR,Dkt Hussein Abrodha pamoja na Sarah Pascal wa kitengo cha simu za dharura (Waliosimama) wakitoa maelekezo kwa Waongoza watalii namna ya kurejesha uhai kwa mtu aliypatwa na tatizo la upumuaji .
Paul Gloy akiwaonesha Waongoza Watalii namna ya kumbeba mtu aliyepatwa na tatizo la kuvunjika Uti wa Mgongo . 
Sarah Pascal wa kituo cha MAwasiliano ya simu za Dharura katika kampuni ya Kilimanjaro SAR ,akitoa maelekezo ya namna ya kutumia kitabu kujaza taarifa za mtu aliefikwa na matatizo wakati wa kupanda Mlima.
 Afisa Uhusiano na Masoko wa Kampuni ay Utafutaji na Uokoaji ya Kilimanjaro SAR ,Abdulrahim Damian akitoa maelezo kwa washiriki wa mafunzo hayo kuhusu kampuni ya Kilimanjaro SAR.


Na Dixon Busagaga ,Arusha .



KATIKA kuongeza thamani ya Utalii wa milimani ,waongoza watalii zaidi ya 500 wa mikoa ya Arusha na Kilimanjaro wameanza kupatiwa mafunzo ya namna ya kutoa huduma ya kwanza kwa wageni pindi wapatapo changamoto wakati wa kupanda.



Mafunzo hayo yanayofanyika kwa wiki mbili kwa kuanza na jiji la Arusha yanatolewa bila malipo na kampuni ya Utafutaji na Uokoaji ya Kilimanjaro SAR ya mkoani Kilimanjaro, mafunzo ambayo hutolewa kipindi cha mapumziko ya biashara ya utalii.



Mtaalamu wa Masoko wa kampuuni hiyo ,William Mbogo alisema Kilimanjaro SAR kwa miaka miwili ya mwanzo imeanza kutoa mafunzo kwa waongoza watalii wa milimani peke yake na kwamba baadae watafanya kwa waongoza watalii wa Safari za hifadhini.



“Kwenye mafunzo yetu haya tumeyagawanya katika sehemu kuu tatu ,sehemu ya kwanza tuna wataalamu wanaozungumzia namna ya kumpatia mtu huduma ya kwanza pale inapotokea mgeni amepata changamoto ,hatuishii hapo tu wanaingia kufanya pia kwa vitendo.”alisema Mbogo.



Alisema sehemu ya pili ya mafunzo hayo washiriki wanafundishwa namna ya kutambua aina mbalimbali ya magonjwa yatokanayo na mlima na pia namna ya kumrejeshea uhai mtu ambaye amepatwa na tatizo la upumuaji kwa kitaalamu wanaita CPR .



Mbogo alisema suala la usalama ni kivutio kikubwa cha wageni kwa kampuni zinazofanya shughuli za utalii huku usalama toa wito kwa kampuni hizo kuendelea kujenga imani na Kilimanjaro SAR ili kujiongezea thamani katika biashara ya utalii .



“Sasa hivi kampuni za utalii  zina ujasili wa kuuza mlima Kilimanjaro na Mlima Meru wakijua kabisa kwamba kuna huduma ya haraka tena ya uhakika kwa kutumia helkopta ambayo atapata mgeni wake na kampuni ya bima ya mgeni ndio itahusika kwenye malipo”alisema Mbogo .



Naye Afisa Uhusiano na Masoko wa kampuni ya Kilimanjaro SAR ,Abdulrahim Damian alisema kwa sasa mafunzo yanatolewa kwa waongoza watalii pekee kwa sababu wao ndio viongozi wa kundi linaloshiriki katika kuwapandisha wageni .



“Tunatoa mafunzo bure kwa hawa waongoza watalii ambao tunaamini ndio viongozi ,tunawapa maarifa waweze kuhudumia wageni lakini pia na watu wote ambao wanaongozana nao katika safari ya kupanda mlimani “ alisema Damian.



“Hii tunafanya kwa sababu mbili, ya kwanza tunashiriki katika uboreshaji wa huduma za kitalii hapa nchini  kwa kushirikiana na wadu wote wa utalii pamoja na serikali ili kuvutia wageni pindi wanapokuja nchini wasiwe na hofu juu ya usalama wao.”aliongeza Damian.



Kwa upande wao washiriki wa mafunzo hayo , Waongoza watalii ,Jonas Luta ,Joyce Jacob na Hussein Paul wameishukuru Kampuni ya Kilimanjaro SAR kwa kuanzisha utaratibu wa kuwapa mafunzo hayo ambayo wameeleza hawakuwahi kuyapata hapo awali .



Mwisho




from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2CK6Rrk
via

Post a Comment

0 Comments