KATORO ISLAMIC WATUMIA MAHAFALI YA 14 KUWAOMBEA DUA WENZAO WANAOSHIKILIWA.

  Masama Blog      
Anaandika Abdullatif Yunus - Michuzi TV.

Shule ya Sekondari ya Katoro Islamic Seminary wamefanya Mahafali ya 14 tangu kuanzishwa kwa Shule hiyo, huku kwikwi, simanzi na majonzi vikitawala juu ya Wenzao wanane wanaoshikiliwa Kwa tuhuma za Kifo cha  Mwanafunzi mwenzao kilichotokea Aprili Mwaka huu katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kagera.

Mahafali hayo yaliyohudhuliwa na Viongozi wa Dini na Siasa wakiwemo wazazi wa wahitimu, walezi pamoja na watu mbalimbali, yaliambatana na Dua ya kumuombea Muasisi wa Shule hiyo  Sheikh Mustapha Khalid Swidiq aliyefariki Machi Mwaka huu, huku Dua hiyo ikifuatiwa na Dua ya kuwaombea waliokuwa Wanafunzi wa kidato cha Nne pamoja na Wafanyakazi wawili wa Shule hiyo wanaoshikiliwa kwa tuhuma za kifo cha mwanafunzi mwenzao.

Awali akizungumza na Michuzi TV ofisini kwake Mkuu wa Shule hiyo Sheikh Fakhrudin Mustapha ambae pia ni Miongoni mwa walioshikiliwa awali kwa tuhuma hizo, na kisha kuondolewa katika tuhuma hizo amesema kuwa, Yale yaliyosambazwa na Vyombo vya Habari kuhusu Tukio hilo siyo ya kweli na zaidi Kuna baadhi ya waandishi wamepandikizwa kwa nia ovu ya kutaka kuichafua Shule, na kusisitiza kuwa mwanafunzi yule marehemu Mudi Muswadiku alikuwa na majeraha kichwani ambayo aliyapata miezi mitatu kabla ya kifo chake baada ya kugombana na Mwenzake (jina limehifadhiwa)majeraha yaliyopelekea kufanyiwa upasuaji wa kichwa kwenye hospitali ya Bugando na tatizo hilo kama Mkuu wa shule ndo alilolidhania kuchangia kifo chake.

Mkuu wa Shule Katoro Islamic ameongeza kuwa Kufuatia ugomvi huo pamoja na mambo mengine Shule ilishiriki kiasi kikubwa kumuhudumia Marehemu ikiwa ni pamoja na kuishirikisha familia katika suala la matibabu, hadi mauti yanamfika Shule ilihusika kumpeleka Hospitali na hatimae umauti ukamkuta. Katika hali ya kushangaza miezi minne baada ya Kifo cha Marehemu Mudi, alijitokeza MTU (jina limehifadhiwa)  akilalamika na kutaka kukamatwa kwa Wafanyakazi na Wanafunzi ili uchunguzi ufanyike juu ya kifo hicho.

Tayari vyombo vya Dola vinaendelea na uchunguzi zaidi wa Tukio hilo, kwa kuendelea kuwashikilia wafanyakazi wawili na Wanafunzi sita Wa Kidato cha Nne ambao wamelazimika kufanya mtihani wao wa kuhitimu wakiwa jela.

Licha ya suala hilo pia kuibuka katika Risala ya Shule iliyosomwa na Mkuu wa Shule hiyo kwa Mgeni Rasmi Mwenyekiti wa Halmashauri ya Bukoba Ndg. Murshidi Ngeze aliyemuwakilisha Mkuu wa Wilaya Bukoba, kutokana na jamii kupokea taarifa  ya tukio kwa maelezo tata, Mkuu wa shule alisisiza na kuwashauri jamaa wa vijana wanaoshikiliwa kuwa na subira na kuwa kesi hiyo mahakamani na hawezi kuizungumzia kwa mapana na kuwa ana imani vyombo vya dola vitawatendea haki vijana wao.

Mhe. Ngeze alishauri kwakuwa kesi hiyo iko mahakamani ni vizuri kuwa na subira na kutolizungumzia sana kwani ana imani mamlaka husika zitalichunguza na kuhakikisha haki inatendeka mapema na kuishauri bodi ya shule izione mamlaka husika kwa malengo mazima ya uharaka wakujua hatima ya vijana wao.
 Pichani Mwenyekiti wa Halmashauri ya Bukoba Murshidi Ngeze akikabidhi cheti kwa mmoja kati ya wahitimu wa kidato NNE 2019 Katoro Islamic seminary, katika mahafali yaliyofanyika katikati ya wiki hii.

 Pichani Mkuu wa Shule Katoro Islamic Seminary Sheikh Fahrudin Mustapha akitoa salaam zake Kwa wageni, wazazi, walezi na wanafunzi wakati wa mahafali ya 14 ya kidato cha Nne Shuleni Katoro.
 Pichani baadhi ya Wahitimu wasichana wakionesha nyuso za furaha wakati Wa mahafali yao ya Kidato cha nne Shule ya Sekondari Katoro Islamic yaliyofanyika katika ukumbi Wa shule
 Pichani baadhi ya Wahitimu wavulana Shule ya Sekondari Katoro Islamic wakiwa katika katika mahafali yao yaliyofanyika katika ukumbi Wa shule.
 Pichani anaonekana Ustadh Nuru mshereheshaji wa mahafali akitoa utaratibu wa zawadi na vyeti
 Baadhi ya akina Mama wazazi Wa wahitimu wakiendelea kufuatailia matukio ukumbini wakati wa mahafali ya kidato cha NNE Katoro Islamic
Pichani Mhe. Murshid Ngeze akitoa hotuba yake kwa niaba ya Mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Bukoba, katika mahafali ya kidato cha Nne 2019 Shuleni Katoro


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2XzNbjg
via
logoblog

Thanks for reading KATORO ISLAMIC WATUMIA MAHAFALI YA 14 KUWAOMBEA DUA WENZAO WANAOSHIKILIWA.

Previous
« Prev Post