Ticker

10/recent/ticker-posts

Kampeni ya ujenzi Wa vyumba vya madarasa Arumeru yafanikiwa kwa asilimia 100

Na Woinde Shizza Michuzi Tv, Arusha

Kampeni ya ujenzi Wa vyumba vya madara mapya 107 ilioanzishwa na Mkuu Wa wilaya ya Arumeru Jerry Muro  imekamilika na kupita malengo kwani wilaya hiyo imeweza kujenga vyumba vya  madarasa 149.

Akizungumzia  kampeni hiyo  Mkuu huyo Wa wilaya  alisema kuwa kampeni hiyo ilianza Mara baada ya kuingia tu wilayani humo ambapo alikuta wilaya hiyo   ikikabiliwa na tatizo LA uhaba Wa  vyumba vya  madarasa.

"Nikizungumzia sekta ya Elimu katika wilaya ya  Arumeru kama mtakumbuka nilipoteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Tarehe 28/08/2019 Wilaya yenye Halmashauri mbili za Arusha Dc, na Meru Dc zenye jumla ya tarafa 6 na kata 53 Zenye Majimbo mawili ya Arumeru Mashariki na Magharibi   Moja kati ya kazi niliyoanza nayo ni kuanzisha kampeni ya ujenzi wa madarasa 107 mapya kwa ajili ya shule za sekondari na msingi ujenzi ambao unagharimu zaidi ya Shilingi Bilioni 2  na sasa tumeweza kujenga vyumba vya madarasa 149 badala ya 107" Alisema Muro

Alibainisha kubwa Katika Halmashauri ya Meru Vyumba 35 vya madarasa ya shule za msingi na Sekondari yamekamilika na Vyumba 42 vya madarasa ya sekondari na msingi vipo kwenye hatua za mwisho kukamilika
Aliongeza kuwa mejiongeza kwa kujenga Mejengo ya utawala 2 hatua ya ukamilishaji, pamoja na Maabara 2 za science hatua ya uzekaji 
Pamoja na  kukamilisha ujenzi wa jengo jipya na la kisasa la wadhibiti ubora wa Elimu .

Alisema kuwa hadi sasa imefikisha mwaka mmoja  ambapo
katika Halmashauri ya Meru wameshajenga vyumba na majengo 82 

Alibainisha katika Halmashauri ya Arusha Madarasa yaliyokamilika 34 ambapo alisema  yameanza kutumiwa kwa ajili ya sekondari na msingi na yaliyo katika hatua ya mwisho ni madarasa 73 kwa ajili ta shule za msingi na sekondari, katika Halmashauri ya Arusha jumla ya Madarasa 107 yanajengwa katika kampeni hiyo

Aidha alibainisha kuwa Kampeni  ya madarasa hayo mpaka sasa imewapa fursa ya kuwa na jumla ya vyumba vya madarasa 149 kutoka malengo ya kujenga vyumba 107, hivyo tumevuka lengo kwa zaidi ya asilimia 100%

"Tumeweza kuongeza uandikishwaji
Wilaya imefanikiwa kuongeza idadi ya wananfunzi wanaojiunga na elimu ya msingi, sasa katika wilaya ya Arumeru wananfunzi wote wanaopaswa kuanza elimu ya msingi wanaandikishwa kwa asilimia mia 

Alisema madara haya yameaidia kwani hadi sasa Wilaya imeendelea kuongoza kwa kuwa wilaya ya kwanza kitaifa kwa ufaulu wa wanafunzi wa sekondari kidato cha sita (form six), na wako kwenye kumi bora kwa ufaulu kidato cha nne (form four)

"Naomba kuchukua fursa hii kumshukuru sana Mhe Rais, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kwa kutusaidia fedha kwa ajili ya utoaji wa elimu Bure jambo ambalo limetusaidia kuhamasisha wananchi kuchangia ujenzi wa madarasa, pili Niwashukuru sana wakurugenzi wa Halmashauri za Meru Emanuel Mkongo na kwa upande Wa  Arusha Dc  Advera Nbabagoye na mtangulizi wake Mhe Dkt. Charles wilson Mahera , pi waheshimiwa madiwani kwa kuridhia utoaji wa vifaa na fedha kidogo " alisema muro

Aliwashukuru pia  ubalozi wa japani ambao umewasaidia zaidi ya milioni 100, pamoja na  wadau wote  wa maendeleo , viongozi wa dini na wananchi ambao wamesimama na sisi katika kipindi hiki cha kuweka msingi wa Maendeleo ya elimu katika wilaya ya Arumeru.
 Mkuu Wa wilaya ya Arumeru  Jerry Muro akikagua moja ya darasa



from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2qSw00m
via

Post a Comment

0 Comments