KAMISHANA WA UHIFADHI TFS PROF.SILAYO AELEZA WALIVYOJIPANGA KUWAKABILI WAHALIFU BAHARINI

  Masama Blog      

Na Said Mwishehe,Michuzi Globu ya jamii 

KAMISHNA wa Uhifadhi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania(TFS) Profesa Dos Santos Silayo amesema kuwa wakala huo umejipanga vema kukabiliana na kila aina ya uhalifu na ujangili ukiwemo wa kutorosha rasimali zitokanazo misitu kwa njia ya bahari na nchi kavu.

Prof.Silayo ameyasema hayo wakati wa akifunga mafunzo ya mbinu za kujiokoa baharini yaliyofanyika katika Chuo cha Baharia cha Dar es Salaam ambapo watumishi wa 15 wa TFS Kanda ya Kusini wanaofanya kazi kwenye misitu ya mikoko, misitu iliyopakana nayo na vikosi vya ukaguzi na udhibiti wa usafirishaji wa mazao ya misitu.

"Niwapongeze watumishi ambao wamehitimu mafunzo haya muhimu , hii inamaanisha kwamba kwa sasa TFS tunao askari na wakati huo huo ni mabaharia ambao wanakwenda kusimama kidete kwa kushirikiana na watumishi wengine kukabiliana na kila aina ya uhalifu hasa baharini.

"Mafunzo haya kunatoa ujumbe kwa wahalifu kuwa sasa hawana nafasi.TFS tumejipanga na tutaendelea kujipanga siku hadi siku kwa kuendelea kuwajenge uwezo watumishi wetu ikiwa pamoja na kuwafundisha mbinu za kisasa za kukabiliana na uhalifu,"amesema Prof.Silayo.

Hata hivyo amesema wakati watumishi wa TFS wakati wa kutekeleza majukumu lao lazima usalama wao pia uangaliwe kwa hali ya juu, hivyo mafunzo hayo ya mbinu za kujiokoa yatasaidia wanapokuwa katika mapambano kuwa na uhakika wa usalama wao.

Ametumia nafasi hiyo kueleza wakati watumishi hao wakipata mafunzo kuna changamoto zimeibuliwa ikiwemo ya uhaba wa vifaa, hivyo TFS itahakikisha inapata vifaa ili kuimarisha utendaji kazi wao ili kufikia malengo na kuongeza kuna boti zimenunuliwa kuimarisha doria.

Awali akisoma rasala ya wahitimu wa mafunzo hayo, Msaidizi Misitu daraja la II Herieth Balua amesema kuwa mafunzo hayo yalianza Oktoba mwaka 2019 hadi Novemba 8 mwaka huu na kutumia nafasi hiyo kuushukuru uongozi wa chuo cha Baharia Dar es Salaam kwa kukubali kutenga muda wao kwa ajili ya kutoa mafunzo hayo.

"Mafunzo haya ya mbinu binafsi za kujiokoa unapokuwa unafanyaka kazi katika maeneo ya bahari ikiwemo misitu ya mikoko ni kitendo au uwezo  ama jitihada za mtu au kundi la watu zinazotumika kuokoa maisha iwapo janga lolote litatokea.Mafunzo haya ni muhimu kwa watendaji tunaofanya kazi katika maeneo ya misitu inayoota sehemu zenye maji.

"Mafunzo haya yalikuwa ni ya nadharia na vitendo .Kwa upande wa nadharia washiriki tumefundishwa aina ya visababishi vya madhara kwenye vyombo vya baharini.Mafunzo kwa vitendo yalishirikisha kwenda kujionea vifaa vya uokozi na namna vinavyotumika iwapo hatari itatokea,"amesema Balua.

Kwa upande wake Mkuu wa Chuo cha Baharia Dar es Salaam Dk.Erick Massami amesema chuo hicho kilianzishwa kwa sheria ya Bunge Na.22 ya mwaka 1991 kwa lengo la kutoa mafunzo ya ubaharia ,utafiti na ushauri katika sekta ya bahari.

Amesema katika ubaharia , chuo kinatoa mafunzo kuanzia ngazi ya awali ya usalama wa vyombo vya majini na maofisa wa meli kuanzia daraja la nne mpaka daraja la kwanza na wanazo aina tano za kozi , hivyo watumishi wa TFS wamepata mafunzo katika moja ya kozi hizo.
 Kamishna wa Uhifadhi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania(TFS) Profesa Dos Santos Silayo(aliyevaa suti nyeusi) akiwa na watumishi wa Wakala huo kutoka Kanda ya Kusini ambao wamehitimi mafunzo ya mbinu zakl kujiokoa baharini ikiwa ni mkakati wa kuwajengea uwezo wanapotekeleza majukumu yao ya kila siku
 Mkuu wa Chuo cha Baharia Dk.Erick Massami akizungumza wakati wa kufungwa kwa mafunzo ya mbinu za kujiokoa Bahari ambapo watumishi 15 wa TFS kutoka Kanda ya Kusini wamehitimu na kutunukiwa vyeti 
 Watumishi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania(TFS) ambao wamehitimu mafunzo ya mbinu za kujiokoa baharini ambayo yametolewa na Chuo cha Baharia jijini Dar es Salaam
Kamishna wa Uhifadhi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) Profesa Dos Santos Silayo akikabidhi cheti cha kuhitimu mafunzo ya mbinu za kujiokoa kwa Herieth Balua ambaye ni Msaidizi Misitu daraja la pili


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2NXWchB
via
logoblog

Thanks for reading KAMISHANA WA UHIFADHI TFS PROF.SILAYO AELEZA WALIVYOJIPANGA KUWAKABILI WAHALIFU BAHARINI

Previous
« Prev Post