Ticker

10/recent/ticker-posts

JAJI MKUU – TANGAZENI MABORESHO YA MAHAKAMA

Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Profesa Ibrahim Hamis Juma, ambaye pia ni Mwenyekiti wa kikao cha wamiliki wa maeneo ya Mpango Mkakati wa Mahakama ya Tanzania,akizungumza jambo wakati wa kikao hicho kilichofanyika Novemba 16, mwaka huu katika ukumbi wa mikutano wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT), uliopo jijini Dar es Salaam.
Balozi Mteule, ambaye alikuwa Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. Hussein Kattanga akitoa mada ya makabidhiano ya Mpango Mkakati wa Mahakama ya Tanzania.
Picha ya pamoja kati ya Jaji Mkuu wa Tanzania, Profesa Ibrahim Juma na viongozi wakuu wa Mahakama ya Tanzania wa sasa na waliopita, wakiwemo wamiliki wa maeneo ya Mpango Mkakati wa Mahakama ya Tanzania.

Wajumbe wa kikao hicho wakifuatilia makabidhiano hayo. 
Balozi Mteule, ambaye alikuwa Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. Hussein Kattanga (kulia) akimkabidhi Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Bw. Mathias Kabunduguru(kushoto) nyaraka muhimu za Mahakama ya Tanzania.
Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Bw. Mathias Kabundunguru akizungumza jambo wakati wa kikao hicho.
(Picha na Mary Gwera-Mahakama)



Na Magreth Kinabo-Mahakama

17.11.2019

Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof.Ibrahim Hamis Juma amewataka watumishi na viongozi wa Mahakama ya Tanzania kutangaza maboresho na shughuli mbalimbali zinazofanywa na Mahakama hiyo ili ziweze kufahamika kwa jamii.

Akizungumza wakati wa uahirishaji kikao cha wamiliki wa maeneo ya Mpango Mkakati wa Mahakama ya Tanzania wa Miaka Mitano kuanzia 2015/16 hadi 2019/20 , kilichofanyika Novemba 16, mwaka huu katika ukumbi wa mikutano wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT), uliopo jijini Dar es Salaam.

Jaji Mkuu alisema kuna haja ya kutafuta namna ya kujitangaza katika maboresho yanayofanyika, ikiwemo shughuli mbalimbali ili ziweze kufahamika kwa umma.

‘ Tuna tatizo la kujitangaza kuwa tunafanya nini, tutafuta namna ya kujitangaza, kama inavyofanya Serikali Kuu, mfano yapo mambo mazuri yamefanyika Kigoma na Sumbawanga , Mahakama ziko vizuri. Tunaona Serikali Kuu inavyojitangaza, hivyo kuna umuhimu wa kufanya jambo hili,’ alisema Jaji Mkuu.

Aliongeza kwamba katika kuboresha taasisi hiyo, mambo ya urasimu yanatakiwa kuvunjwa na kuweka pembeni tofauti ya vyeo au hadhi, kwani jambo linalopaswa kuzingatiwa ni utaalamu wa mtu.

Huku akisisitiza kwamba mkubwa akikosea kuna namna ya kumsaidia , hivyo watumishi wanapaswa kutoa hoja na michango yao ili kuweza kuendeleza maboresho yanayofanyika.

‘Naona mambo mengi yanayofanyika yanatokana na hoja zenu, kazi zetu sisi ni kukubali na kupendekeza mabadiliko, nguvu ya taasisi iko kwa watumishi,’ alisema.

Aidha Jaji Mkuu aliwataka watumishi hao, kuwa huru kuzungumza wakiwa kwenye mikutano ili changamoto mbalimbali ziweze kufahamika na kutatuliwa, hivyo kama kuna hoja zipitishwe kwenye ngazi zinazohusika. 

Alifafanua kuwa lazima watumishi hao wawe na matamanio ya hali ya juu ya kuweza kukabiliana na changamoto zinazoikabili Mhimili huo.

Akizungumzia kuhusu ripoti ya Benki ya Dunia ya mwaka 2020 (Uwezeshaji na Ukuzaji wa Biashara), alisema imeeleza namna ya kupunguza muda na gharama za kutatua migogoro ya biashara. Ripoti hiyo imeeleza urahisi wa kufanya biashara, hivyo Mhimili huo iitumie kwa sababu imeeleza vigezo vya mwaka 2020 ili kutayarisha ya kwake.

‘Sisi tutayarishe ya kwetu tuoneshe namna tumeweza kusaidia kurahisisha uwekezaji na namna ya kufanya biashara na kujitangaza kuwa tumeweza zaidi ya vigezo vya Benki ya Dunia,’ alisisitiza.

Kwa mujibu wa Mjumbe wa kikao hicho, Bw. William Machumu, ambaye ni Mtendaji wa Mahakama ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi, alisema katika ripoti hiyo,Tanzania imekuwa ni nchi ya 71 duniani kati ya nchi 190 zinazopimwa kwa kutumia kigezo cha uvutiaji wa biashara, ambapo Mahakama inapimwa kwa kufanyiwa tathimini hiyo.

Machumu alisema katika ripoti ya mwaka 2019 ya benki hiyo, Tanzania ilikuwa ya 64. Hivyo eneo hilo ninatakiwa lipewe kipaumbele.

Kwa upande wake Balozi Mteule, Mhe. Hussein Kattanga, akizungumzia mpango huo alizungumzia kuhusu maeneo ambayo yamefanyiwa kazi na mengine yanayohitaji mkazo wa kufanyiwa kazi.

Naye Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Bw. Mathias Kabunduguru aliwataka watumishi hao, kuendeleza tabia ya kufanya kazi kwa ushirikiano kwa kuwa wannapofanya kazi vizuri Mahakama ndipo inaposifiwa.


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2r422WV
via

Post a Comment

0 Comments