Ticker

10/recent/ticker-posts

HUKUMU KESI YA ALIYEKUWA RAIS WA TFF JAMAL MALINZI NA WENZAKE WATATU YAKWAMA KUSOMWA

HUKUMU dhidi ya kesi ya aliyekuwa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania ((TFF), Jamal Malinzi na wenzake watatu iliyokuwa isomwe leo Novemva 7,2019 imeshindwa kusomwa kwa sababu hakimu aliyekuwa akisikiliza kesi hiyo amehamishiwa sehemu nyingine.

Mapema, wakili wa serikali kutoka Takukuru Pendo Temu amedai mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Kevin Mhina kuwa kesi hiyo leo ilikuja kwa ajili ya kusomewa hukumu Mbele ya Hakimu Maira Kasonde lakini wamepata taarifa kuwa amehamishwa hivyo wanaonba muongozo.

"Ni kweli amepata uhamisho na arrangement zimeishakamilika kumuwezesha kuandika hukumu hivyo nawapangia tarehe nyingine" amesena Mhina.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Novemba 21,mwaka hu kwa ajili ya kusomewa hukumu.

 Awali kesi hiyo ilikuwa na mashtaka 30 lakini ilipofikia katika uamuzi wa kama washtakiwa wana kesi ya Kujibu ama la  walipunguziwa mashtaka 10 kati ya 30 yaliyokuwa yakiwakabili baada ya Jamhuri kushindwa kuonesha kama washtakiwa wana kesi katika makosa hayo.

Mahakama hiyo iliwakuta wana kesi ya kujibu washtakiwa hao kwa mashtaka 20 yaliyobakia baada ya Jamhuri kuonesha kwamba wana kesi hivyo walijitetea wenyewe bila kuita na mashahidi.

Upande wa Jamhuri katika kesi hiyo ulikuwa na  mashahidi 15 na vielelezo tisa.

Katika hatua hiyo mshtakiwa watano Miriam Zayumba aliachiwa huru kwa sababu kaonekana hana kesi ya kujibu kwa mashtaka yote yaliyokuwa yakimkabili.

Washtakiwa wengine waliobakia katika kesi hiyo ni Mhasibu wa TFF, Nsiande Mwanga, Katibu wa shirikisho hilo,, Selestine Mwesigwa na Karani wa TFF, Flora Rauya ambao kwa pamoja wanakabiliwa na mashtaka 20 katika kesi ya jinai namba 213 ya mwaka 2017.

Washtakiwa wanakabiliwa na mashtaka mbalimbali yakiwamo ya kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na utakatishaji wa dola za Marekani 173,335.



from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2JZMlqF
via

Post a Comment

0 Comments