DOWNLOAD APP YETU HAPA

Huduma Ya Matibabu Bure Yatolewa Wilayani Urambo

  Masama Blog      

Na Editha Edward -Tabora 

Mkuu wa mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri amezindua huduma ya Matibabu ya bure ya kibingwa wilayani Urambo Mkoani Tabora ambapo huduma hiyo inatolewa kwa siku tano na timu ya madaktari bingwa 45 wa JITOLEE group ambayo yanaratibiwa na familia ya hayati Samweli Sitta aliyekuwa Spika wa Bunge la Jamhuri Ya muungano wa Tanzania kwa lengo la kuenzi mchango wake katika jumbo la Urambo

Akizindua Matibabu Hayo Mwanri amesema huduma hiyo ni muhimu sana hivyo wananchi wa urambo wanatakiwa kutoipuuzia na wajenge utamadumi wa kwenda hospitali ili waweze kuangalia afya zao na kufata masharti watakayo pewa na madaktari 

"Sisi tunapenda mambo ya kupuuza watu zamani tulikuwa tunakula magimbi viazi mchemsho magimbi mboga za majani matunda lakini siku hizi tumekalia kula chipsi Ndo maana magonjwa makubwa kama presha tunayapata tunatakiwa tupunguze"Amesema Mwanri

Kwa upande wake Mbunge Wa Urambo Magreth Sitta amesema yeye na familia yake walikubaliana kuendesha zoezi hilo Ikiwa ni sehemu ya kuenzi mchango wa Samweli Sitta kwa wananchi wa wilaya ya Urambo"kama mapenzi ya Mungu Yametimizwa hivyo tumeamua kuangalia jinsi gani tunaweza kusaidia jamii inayotunzunguka katika kuangalia afya za kina mama na kupimwa magonjwa mbalimbali yakiwemo meno, macho na kupima afya zao kwa ujumla "Amesema Magreth

Nae Mwenyekiti wa JITOLEE group Daktari Erick Muhumba amesema wanategemea kuona watu wengi zaidi katika huduma hiyo ambapo ametoa takwimu kwa mwaka 2017 wananchi waliojitokeza kuangaliwa afaya zao walikuwa Elf moja Mia moja kumi na nane na mwaka 2018 walikuwa Elf moja mia nne thelathini na nane

Aidha huduma hiyo itasaidia kwa kiasi kikubwa wananchi wa Wilaya ya Urambo hivyo wananchi hao wanatakiwa kutosita kwenda kuangaliwa afya zao ili kupunguza adha ya kwenda kutibiwa nje ya Mkoa Wa Tabora. 
Madaktari bingwa 45 wa JITOLEE group ambao wanatoa huduma ya kupima magonjwa mbalimbali kwa wananchi wa Wilaya ya Urambo
Mbunge wa jimbo la Urambo Magreth Sitta akizungumza katika uzinduzi huo wa Matibabu bure ambayo unaratibiwa na familia ya hayati Samweli Sitta.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri akizungumza katika huduma ya Matibabu bure wilayani Urambo


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2X6UwXu
via
logoblog

Thanks for reading Huduma Ya Matibabu Bure Yatolewa Wilayani Urambo

Previous
« Prev Post