Ticker

10/recent/ticker-posts

DC SIHA:KESHENI KUKAMILISHA UJENZI WA SHULE.

 Mkuu wa Wilaya ya Siha Onesmo Buswelu akikagua ujenzi wa madarasa unaoendelea katika shule ya ya sekondari Songu ambapo alishangazwa  na ujenzi wa shule hiyo kusimama
Mafundi wanaojenga shule hiyo Onesmo  Lyimo na Martin Kingu  wamesema kuwa iwapo wataletewa vifaa vyote muhimu wako tayari kufanya .


Na Vero Ignatus,Killimanjaro.

Agizo limetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Siha Onesmo Buswelu  kuwataka  mafundi kufanya kazi mchana na usiku pamoja  kuhamishia makazi yao kwa muda katika shule ya sekondari Songu inayojengwa ili waweze kukamilisha ujenzi wa shule hiyo hadi ifikapo Novemba 27  mwaka huu .

Buswelu ameyasema hayo  wakati wa ziara yake ya kutembelea ujenzi wa shule ya sekondari Songu na kushangazwa na ujenzi wa shule hiyo kusimama kwa muda licha ya halmashauri kutoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa shule hiyo ambapo ameiagiza Kamati ya ujenzi kununua vifaa vya ujenzi kwa muda ili kukamilisha ujenzi huo.

Mkuu huyo wa wilaya amesema kuwa shule hiyo inapaswa kukamilika haraka ili Mdhibiti ubora aweze kwenda kuikagua na kuipitisha tayari kwa kuanza kupokea wanafunzi januari 2020.

Ameainisha  amesema kuwa serikali imedhamiria kusogeza huduma ya shule karibu ili wanafunzi waweze kunufaika na elimu bure inayotolewa na serikali ya awamu ya tano.

Isaya Mkilindi ni  Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Ujenzi   amesema kuwa kwa sasa wako kwenye hatua ya ununuzi wa mbao na saruji hivyo watakahakikisha kazi hiyo inakamilika kwa muda na kwa wakati.

Kwa upande wao mafundi wanaojenga shule hiyo Onesmo  Lyimo na Martin Yohana Kingu  wamesema kuwa iwapo wataletewa vifaa vyote muhimu wako tayari kufanya kazi hadi muda wa ziada ili kukamilisha ujenzi huo.



from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2XipT1g
via

Post a Comment

0 Comments