Ticker

10/recent/ticker-posts

DC CHONGOLO AWAFUNDA VIJANA WAJASIRIAMALI

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe. Daniel Chongo amewataka vijana kutumia fursa inayotolewa na serikali kupitia halmashauri kupata mikopo isiyokuwa na riba ili waweze kujikwamua kiuchumi.

9Mhe. Chongolo alisema kuwa Manispaa ya Kinondoni inafungu la bajeti kwa ajili ya kutoa mikopo kwa Vijana, wakina mama na watu wenye ulemavu kwa lengo la kuwasaidia kujikwamua katika umasikini hivyo vijana wanapaswa kutumia nafasi hizo wanazozipata kwani itawawezesha kukuza mitaji yao na hivyo kufikia lengo la kuwa na viwanda huku akitolea mfano wa mfanyabiashara mkubwa Marehemu Dk. Reginal Mengi ambaye alifanikiwa kuwa na viwanda kupitia ujasiriamali.

Alifafanua kuwa iwapo watatumia vizuri mafunzo hayo yataleta tija katika kukuza uchumi wa ndani na kwamba serikali kupitia halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni itasimamia kupata mikopo hiyo na hivyo kuwawezesha kupata mashine pamoja na eneo la kujenga kiwanda chakutengeneza bidhaa za ngozi.

“ Nawapongeza sana idara husika ambayo imeandaa haya mafunzo sambamba na maonyesho ya bidhaa za ngozi, vijana mliopo hapa ,tumieni hii fursa mliyoipata, hakuna mafanikio ya siku moja, wote waliofanikiwa walianza kama nyie hapa” alisema Mhe. Chongolo.

“ Tunahitaji watu ambao watakuwa na nia ya kweli ya kujikwamua kiuchumi, inawezekana kuzalisha bidhaa za ngozi kwakuwa Tanzania tunaongoza kwakuwa na mifugo, ukiangalia Dar es Salaam ndio inaongoza kwa kula nyama,kwahiyo tunazana za kutengenezea bidhaa zetu” alifafanua.

Kwaupande wake , Meneja ukuzaji Bidhaa kutoka Tan Tredi , Masha Husein alisema kuwa wataendelea kushirikiana na manispaa ya Kinondoni katika kuwaelimisha wajasiriamali namna ya kufanya biashara kwenye maonesho kwani hiyo imekuwa ni changamoto kubwa kwao.

Alifafanua kuwa, wajasiriamali wengi hawana uelewa wa kutosha kuhusiana na namna ya kushiriki kwenye maonesho mbalimbali wanapopata nafasi jambo ambalo kama Tan Tredi imeliona na hivyo kusisitiza kuwa watahakikisha wanatoa elimu hiyo ili waweze kunufaika.

Naye Mkuu wa Idara ya Mifugo na Uvuvi Dk. Patricia Henjewele alimpongeza Mhe. Chongolo kwakujali vijana na kusema kuwa katika maonesho ya nane nane waliona umuhimu wakukutana na wajasiriamali hao na hivyo kuandaa semina hiyo iliyoambatana na maonesho.

Dk. Henjewele aliwapongeza Tan Tredi kwakuwezesha maonesho hayo na hivyo kuahidi kuendeleza ushirikiano zaidi katika kutoa elimu kwa wajasiriamali hao.
 Mkuu wa Idara ya Mifugo na Uvuvi, wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni , Dk. Patricia Henjewele akizungumza na washiriki vijana wajasiriamali wa bidhaa za ngozi wakati wa semina iliyofanyika jana katika ukumbi wa Manispaa. Kushoto ni mkuu wa Wilaya hiyo Mhe. Daniel Chongolo.
 Meneja ukuzaji bidhaa wa Tan Tred, Masha Hussein, akizungumza na vijana wajasiriamali jana wakati wa uzinduzi wa semina ya vijana wajasiriamali wa bidhaa za ngozi iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe. Daniel Chongolo akifuatilia kwa makini majadiliano ya semina ya vijana wajasiriamali wa bidhaa za ngozi kabla ya kufua kwa semina hiyo iliyofanyika jana katika ukumbi wa mikutano. Kulia ni Mkuu wa Idara ya mifugo na Uvuvi Dk. Patricia Henjewele.
 Mmoja wa maafisa  Mifugo wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, Deusdedit Nestory kutoka Idara ya Mifugo na Uvuvi akifafanua jambo kwa vijana wajasiria mali wa bidhaa za ngozi wakati wa semina iliyofanyika jana.
Mshiriki wa semina hiyo kijana anayejihusisha na utengenezaji wabidhaa za ngozi za kampuni ya asili asilia Viola Munishi akichangia mada iliyokuwa ikijadiliwa katika semina hiyo.


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2KlFEPX
via

Post a Comment

0 Comments