CHADEMA WALALAMIKA WAGOMBEA WAO KUNYANG'ANYWA FOMU NA KUCHANWA WAKATI WAKIREJESHA

  Masama Blog      
Na Woinde Shizza globu ya jamii ,Arusha
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mkoa wa Arusha kimekutana na kujadili changamoto za urejeshwaji wa fomu za wagombea wake Katika nafasi ya serikali ya Mtaa kitongoji na vijiji.

Aidha chama hicho kimebaini kuwa zoezi hilo lilifanyika bila kuwepo kwa demokrasia kwani wagombea wake walikuwa wananyanganywa fomu na kuchanwa kwa kutumia mabavu huku wakitishiwa kwa bastola kupitia kwa makada Wa ccm

Akizungumza na vyombo vya habari Katibu wa Chadema Arusha Innocent Kisanyage Amesema kwamba makada wa chama chamapinduzi Ccm wamekua wakitumia nguvu kubwa kunyanganya Fomu za wagombea na kuchana kwa kushirikiana na wasimamizi wa vituo huku watendaji wa Kata wakikimbia vituo vyao vya kazi .

Amesema kitendo hicho kinaonyesha kwamba Chadema Mkoa Wa Arusha bado ni tishio kubwa kwakua inatumika nguvu nyingi kuhakikisha kwamba wanashindwa kuwaweka wagombea.

Aidha Baadhi ya wagombea walio nyanganywa fomu zao na kupigwa mapanga na wengine kunyooshewa bastola wamesema walifika kituo kikuu cha Polisi jijini Arusha lakini walijibiwa watoe fomu za kugombea ndio wapate P 3 ili waweze kupatiwa matibabu.

Sakata la urudishwaji wa fomu kwa wagombea wa vyama vya siasa limebubujikwa na sintofahamu kwani watendaji wamekua wakiwarudisha wagombea wa upinzani kwa kile wanacho Dai kwamba hawana sifa za kugombea nafasi hizo 

Mbunge wa jimbo la Arusha Mjini God Bless Lema amesema kwamba kitendo hicho nicha kiuni kwani Ccm wanatumia nguvu kubwa kuaharibu uchaguzi na kama wanataka upinzani wajitoe waseme kwamba uchaguzi ni wa chama kimoja tu 

Lema ameeleza kwamba awapo tayari kuona uchaguzi mdogo unatumika nguvu kubwa kuwaumiza wagombea kwa kunyooshewa bastola mapanga kwani nchi hii ni ya kila Mtanzania na sio mtu mmoja peke yake 

Katibu wa Chadema Mkoa wa Arusha Elisa Mungure amesema mpaka sasa vijiji vyote katika jimbo la Arumeru Magharibi na mashariki Munduli akuna mgombea aliyefanikiwa kurejesha fomu na kumekuwepo na huuni mkubwa kwa kutishiwa na wengine kukimbiwa na watendaji wa kata

Uchaguzi huo Mdogo kabla kuelekea uchaguzi mkuu mwakani tayari umeonyesha kwamba Ccm aikubaliki ndio maana wanatumia jeshi la Polisi kuvuruga uchaguzi huo 

Msimamizi wa uchaguzi jimbo la Arusha Msena Bina amesema akuna malalamiko yoyote walio pokea kutoka kwa Chadema wala wagombea wa nafasi hizo . from MICHUZI BLOG https://ift.tt/32aLM3w
via
logoblog

Thanks for reading CHADEMA WALALAMIKA WAGOMBEA WAO KUNYANG'ANYWA FOMU NA KUCHANWA WAKATI WAKIREJESHA

Previous
« Prev Post