CGP PHAUSTINE KASIKE AANZA ZIARA YA KIKAZI MKOANI MANYARA

  Masama Blog      

 Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini - CGP Phaustine Kasike (kushoto) akizungumza na Mkuu wa Magereza Mkoa wa Manyara, Kamishna Msaidizi wa Magereza, Lipina Lyimo(katikati) pamoja na Kamishna Msaidizi wa Magereza, Masoud Kimolo(kulia) muda mfupi alipowasili leo Novemba 16, 2019 Mkoani humo. CGP Kasike yupo mkoani Manyara kwa ziara ya kikazi yenye lengo la kukagua magereza yote ya Mkoa huo na kuzungumza na Maafisa na askari wa Jeshi hilo.
 Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini - CGP Phaustine Kasike akisalimiana na Maafisa wa Magereza Mkoani Manyara mara baada ya kuwasili Gereza Babati kwa ziara yake ya kikazi leo Novemba 16, 2019.
  Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini - CGP Phaustine Kasike(meza kuu) akiongoza kikao kazi na Maafisa wa Magereza Mkoani Manyara kabla ya kufanya Baraza la Wafungwa na mahabusu wa Gereza Babati.
 Mkuu wa Magereza Mkoani Arusha, Kamishna Msaidizi wa Magereza, Anderson Kamtiaro(kulia) akimuonesha  Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini - CGP Phaustine Kasike(kushoto) shamba la maharage ambalo limelimwa kwa kutumia Kilimo cha umwagiliaji Gereza Arusha.
  Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini - CGP Phaustine Kasike(wa pili toka kulia) akitoa maelekezo kwa Mkuu wa Magereza Mkoani Arusha, Kamishna Msaidizi wa Magereza, Anderson Kamtiaro(kulia)alipokagua Shamba la mahindi kabla ya kuendelea na ziara  ya kikazi Mkoani Manyara leo Novemba 16, 2019(Picha zote na Jeshi la Magereza).


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2CO0yCO
via
logoblog

Thanks for reading CGP PHAUSTINE KASIKE AANZA ZIARA YA KIKAZI MKOANI MANYARA

Previous
« Prev Post