Benki Ya Exim Yakamilisha Rasmi Umiliki Wa Benki Ya UBL

  Masama Blog      
Benki ya Exim Tanzania imeendelea kujitanua zaidi baada ya kufungua rasmi tawi lake jipya katika mtaa wa Mkwepu jijini Dar es salaam kufuatia benki hiyo kukamilisha taratibu za umiliki wa iliyokuwa Benki ya UBL Tanzania.

Hatua hiyo inafanya Benki ya Exim Tanzania kuwa benki ya kwanza miongoni mwa benki za sekta binafsi hapa nchini zilizofanikiwa kuunganisha benki nyingine na hivyo kuifanya kuwa miongoni mwa benki tano kubwa hapa nchini ikiwa na ukwasi wa kiasi cha Tsh 1.7 Trilioni.

"Tunafurahishwa na ongezeko kubwa la wa wateja wa aina tofauti ambao watajiunga na familia ya benki ya Exim na tunawahakikishia kuwa tunafurahi kuwa nao kwenye safari yetu na tunajitoa kuhakikisha kwamba wanaendelea kufurahia huduma zenye ubunifu kutoka kwetu.''

''Wateja wakiwa ni sehemu muhimu zaidi ya biashara yetu, tunaahidi kufanya kazi kwa bidii ili kuhakikisha wanafurahia huduma zetu,'' Alisema Bwana Jaffari Matundu, Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Exim.

Kwa mujibu wa Bw. Matundu hatua hiyo inakwenda sambamba na msimamo wa Rais Dk John Magufuli ambae amekuwa akisisitiza juu ya umuhimu wa kuwa na benki kubwa zaidi na ndogo nchini kwa kuwa ni hatua muhimu kwa afya ya kifedha katika ukuaji wa uchumi hususani katika kutoa huduma kamili na zenye ubunifu kwa wateja.

"Tanzania ina benki nyingi ukilinganisha na mataifa mengine ikiwemo Afrika Kusini na Nigeria. Sekta ya benki imekuwa ikishuhudia uunganishwaji wa mabenki ambao mwisho wa siku utaziacha benki zikiwa na uwezo wa kusukuma ukuaji wa uchumi kikamilifu. ''

"Dar es salaam ni soko muhimu kwa Benki ya Exim na hivyo uwepo wa tawi jipya la Mkwepu ambalo lenye teknolojia, ubunifu na muundo ambao utawawezesha wateja kukutana na maafisa wa benki kwa njia ambayo inawafaa na katika mazingira ambayo ni yanafikika kwa wote,'' alisema.

Aidha Bw Matundu alisema mchanganyiko wa benki binafsi na zile za umma zilizosambaa kote nchini utahakikisha kuwa kuna mtiririko mzuri wa huduma za kifedha.

"Wajasiriamali watakuwa wamehakikishiwa upatikanaji wa kutosha wa mitaji inayohitajika kupanua biashara zao, ambayo itasababisha kasi kubwa ya ongezeko la ajira na hivyo kupunguza kabisa tatizo la ukosefu wa ajira nchini,'' alisema

Ujio wa tawi hilo jipya unaifanya benki ya Exim Tanzania kuwa kuwa na jumla ya matawi 33 kote nchini.

Kwa zaidi ya miaka 22, benki ya Exim imefanikiwa kupata hadhi ya kuwa benki kimbilio si tu Tanzania bali pia nje ya nchi ambapo imeweza kujitanua kwa kuanzisha matawi yake ikiwemo nchi za Djibouti, Comoros na Uganda.

Meneja wa Huduma kwa wateja na Uendeshaji wa Benki ya Exim Tawi la jipya la Mkwepu, jijini Dar es Salaam Bw Brian Bennet (Kushoto) akimkaribisha mmoja wa wateja wa benki hiyo aliefika kwenye tawi hilo ili kupata huduma za benki hiyo. Tawi hilo jipya ni mkakati wa benki hiyo kujitanua zaidi baada ya kukamilisha taratibu za umiliki wa iliyokuwa Benki ya UBL Tanzania.
 Ofisa Huduma kwa wateja na Uendeshaji wa Benki ya Exim Tawi la jipya la Mkwepu, jijini Dar es Salaam Bi Helen Muhenga (Kushoto) akimkaribisha mmoja wa wateja aliefika kwenye tawi hilo ili kupata huduma za benki hiyo. Tawi hilo jipya ni mkakati wa benki hiyo kujitanua zaidi baada ya kukamilisha taratibu za umiliki rasmi wa iliyokuwa Benki ya UBL Tanzania.


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2qr4BSV
via
logoblog

Thanks for reading Benki Ya Exim Yakamilisha Rasmi Umiliki Wa Benki Ya UBL

Previous
« Prev Post