Ticker

10/recent/ticker-posts

Benki ya Exim Yajizatiti kuhudumia sekta korosho Mtwara


Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mtwara-Mikindani  Bw. Emanuel Mwaigobeko akizungumza wakati wa hafla ya chakula cha jioni iliyoandaliwa na benki ya Exim Tanzania kwa ajili ya wadau wa zao la korosho mkoani Mtwara iliyolenga kupata wasaa wa kujadili fursa mbalimbali za kibiashara hususani katika zao hilo pamoja na  uboreshaji wa huduma zitolewazo na benki hiyo kwa wadau hao mkoani humo.

 Mmoja wa wadau wakubwa wa Korosho mkoani Mtwara Bw Ramesh Kennedy akizungumza wakati wa hafla ya chakula cha jioni iliyoandaliwa na benki ya Exim Tanzania kwa ajili ya wadau haoili kupata wasaa wa kujadili fursa mbalimbali za kibiashara hususani katika zao hilo pamoja na  uboreshaji wa huduma zitolewazo na benki hiyo kwa wadau hao mkoani humo.
Mkuu wa huduma ya rejareja wa benki ya Exim, Bw. Andrew Lyimo (wa kwanza kushoto) pamoja na Mkuu wa Hazina na Masoko ya Fedha wa benki hiyo Bw Arafat Haji (wa kwanza kulia) wakiwaongoza wageni waalikwa akiwemo Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mtwara-Mikindani  Bw. Emanuel Mwaigobeko (alievaa suti nyeusi) kupata chakula wakati wa hafla hiyo.

Mtwara ; Octoba 31, 2019: Benki ya Exim Tanzania mapema wiki hii iliandaa hafla ya chakula maalum kwa ajili ya wadau mbalimbali wa zao la korosho mkoani Mtwara ili kupata wasaa wa kujadili fursa mbalimbali za kibiashara hususani katika zao hilo, mipango ya ukuaji na uboreshaji wa huduma zitolewazo na benki hiyo kwa wadau hao mkoani humo.
Akizungumza kwenye hafla hiyo iliyohudhuliwa na wadau mbalimbali wa zao la korosho wakiwemo viongozi wa kiserikali, wafanyabiashara wakubwa na wadogo pamoja na wafanyakazi wa benki hiyo, Mkuu wa huduma ya rejareja wa benki ya Exim, Bw. Andrew Lyimo alisema kupitia hafla hiyo  walilenga pia  kutoa fursa miongoni mwa wateja hao ili waweze kufahamiana na kufungua wigo wa kufanya biashara pamoja.
“Pamoja na kushukuru kwa namna ambayo wateja wetu wamekuwa nasi hadi kufikia mafanikio ya kuikuaji na ubora wa huduma zetu, hafla hii inatoa fursa kwa wateja wetu pia kufahamiana wao kwa wao na hivyo kufungua milango ya fursa baina yao,’’ alisema Lyimo.
Alisema ukuaji wa benki hiyo unaoshuhudiwa kwasasa ni matokeo ya ushirikiano baina yake na wateja wake ambao kwa kiasi kikubwa wameonyesha imani kubwa kwa benki hiyo hali ambayo imekuwa ikiiwezesha benki hiyo kubuni huduma bora na rafiki za kibenki ili kulinda na kurejesha imani hiyo kwa wateja wa benki hiyo.
Pamoja na mambo mengine hafla hiyo ilipambwa na shuhuda mbalimbali kuhusu ubora wa huduma za benki hiyo kutoka kwa wadau hao.
Akizungumza kwenye hafla hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara Bw. Emanuel Mwaigobeko alisema  mkoa huo umejipanga kwa dhati kuhakikisha ununuzi wa mkorosho unaenda vyema kwa kuzuia watu wachache kuharibu taswira ya serikali pamoja na sekta nzima ya kilimo cha zao hilo.
Pamoja na kuipongeza benki  ya Exim kwa namna inavyoshirikiana  na wadau wa zao hilo mkoani Mtwara, Bw Mwaigobeko alizitaka taasisi zinazohusika na masuala ya fedha mkoani humo kusaidia katika kuwajengea uelewa wa kutosha kuhusu masuala ya kifedha wakulima na wafanyabiashara wa zao hilo mkoani humo.
Alisema ni matarajio yake kwamba wakulima watakuwa waaminifu kupeleka korosho safi ili wasiharibu ubora wa korosho za Tanzania katika soko la ndani na nje.



from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2q9kkWs
via

Post a Comment

0 Comments