BASATA WAMPA BARAKA ZOTE MISS UNIVERSE KWENDA KUWAKILISHA NCHI

  Masama Blog      
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

BARAZA la Sanaa la Taifa (BASATA) limemkabidhi bendera mwakilishi wa mashindano ya Ulimbwende ya dunia ya  Miss Universe 2019 yanayotarajia kufanyika Jiji la Atlanta nchini Marekani.

Mashindano hayo yatafanyika Desemba 08 mwaka huu, na kwa Tanzania yatawakilishwa na Shubila Stanton Kaigarula (23) Miss Universe Tanzania ambaye anasafiri leo Novemba 27 kwenda kuliwakilisha Taifa kwenye mashindano ya ulimbwende ya Miss Universe nchini Marekani. 

Katibu Mtendaji  Godfrey Mngereza amekabidhi bendera kwa mrembo huyo na ameitumia nafasi hii kuwaasa Wasanii wengine nchini wajijengee tabia ya kuaga ili kupata baraka za Serikali.

 Amesema, pindi wanapohitajika kusafiri kwenda kuliwakilisha Taifa kwenye mashindano mbalimbali ni muhimu serikali kufahamu na hilo linajenga taswira nzuri kwa taifa.
 Katibu Mtendaji wa BASATA Godfrey Mngereza akikabidhi bendera kwa Mwakilishi wa Tanzania kwenye mashindano ya ulimbwende Miss Universe 2019 yanayotarajia kufanyika Jiji la Atlanta Nchini Marekani Desemba 12 mwaka huufrom MICHUZI BLOG https://ift.tt/35NWrU7
via
logoblog

Thanks for reading BASATA WAMPA BARAKA ZOTE MISS UNIVERSE KWENDA KUWAKILISHA NCHI

Previous
« Prev Post