Ticker

10/recent/ticker-posts

Barabara ya kutua na kuruka ndege Kiwanja cha Arusha kurefushwa zaidi

BARABARA ya kutua na kuruka ndege ya Kiwanja cha Ndege cha Arusha itaongezwa urefu, ili iweze kuruhusu ndege kubwa za abiria kuanzia 70 ziweze kutua na kuruka bila tatizo, imeelezwa.

Mhe. Husna Malima, Mbunge wa Kigoma Kusini mwishoni mwa juma hili (Ijumaa) alihoji Je serikali inampango gani wa kuboresha Kiwanja cha Ndege cha Arusha ili wananchi wa mikoa ya Singida, Manyara, Simiyu, Manyara, Mara na Dodoma wahamasike kutumia usafiri wa ndege, ambazo zinatosheleza kwa sasa?

Amesema mafaniko ya uwepo wa ndege nyingi za abiria nchini ni pamoja na ndege hizo kutumika kwa wananchi kuzipanda.Akijibu swali hilo Bungeni, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Issac Kamwelwe amesema kurefushwa huko kutafanikisha ndege aina ya Bombardier ambayo inabeba abiria kuanzia 70 kutua na kuruka bila tatizo.

Mhe. Kamwelwe amesema tayari bajeti imetengwa kwa ajili ya kazi hiyo, ambapo kiwanja hicho ni cha tatu nchini kwa kutua na kuruka ndege nyingi zaidi ya 125 kwa siku.

“Tumeweka bajeti kuendeleza kiwanja cha ndege cha Arusha na tayari tenda
imetangazwa, kiwanja hiki kinaongoza kwa kutua ndege nyingi zaidi kwa siku nibiashara kubwa na ndio maana tunataka ndege ya Bombardier itue hapo,” alisisitiza Mhe. Kamwelwe.

Amesema mikoa jirani na Arusha ya Manyara, Singida, Dodoma, Simiyu na Maraitafaidika na maboresho ya kiwanja hicho kwa kuwa wataweza kukitumia ipasavyo.

Naye Meneja wa Kiwanja hicho, Mhandisi Elipid Tesha amesema barabara ya kutua na kuruka ndege itaongezwa urefu kwa meta 200, ambapo sasa inaurefu wa meta 1600 na itakuwa 1800, na pia patajengwa eneo la kugeuza ndege.

Mhandisi Tesha amesema kwa sasa kazi inayoendelea ni ujenzi wa eneo la maegesho ya ndege (Apron), ambayo yakikamilika yatapunguza msongamano kwa asilimia 30; pia barabara ya kupita ndege kwenda katika maegesho (taxiway); ujenzi wa maegesho ya magari yapatayo 350 kwa kiwango cha lami ambapo unakwenda sambamba na ujenzi wa mfumo wa malipo ya maegesho hayo.

Pia amesema ujenzi huo wa maboresho ya kiwanja cha ndege cha Arusha utahusisha ujenzi wa eneo la kupumzika abiria, ofisi za waegesha ndege (mashellers), kibanda cha ulinzi na vyoo .


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2qx8t4J
via

Post a Comment

0 Comments