ANTONIO CONTE AWAFUNDISHA WACHEZAJI WAKE KUJAMIANA

  Masama Blog      

Na Bakari Madjeshi, Michuzi TV

Inter Milan ya Italia ina lengo lakumaliza Ligi (Serie A) ikiwa katika nafasi ya kwanza, katika kuhakikisha timu hiyo inashika usukani hadi mwisho wa msimu huu, Kocha Mkuu wa Klabu hiyo, Antonio Conte amewapa somo Wachezaji wake namna yakufanya mapenzi katika kipindi cha Ligi ili kuwa na kiwango bora wawapo uwanjani. 

Kupitia Jarida la L'Equipe Kocha huyo amenukuliwa akisema “Katika msimu, mahusiano hayatakiwi kufanywa kwa muda mrefu, lazima ufanye mapenzi kidogo ikiwezekana pale ukiwa na mpenzi wako”

Conte anataka kushika usukani wa Serie A akiwa na Inter Milan wenye alama 31 mpaka sasa akiwa na michezo 12 akiachwa alama moja na Juventus wenye alama 32 katika msimamo wa Ligi hiyo.

Somo lakujamiana kwa Wanamichezo wengi duniani, Je? ni funzo kwa Wachezaji wa Inter Milan – mnamo 2010 katika Michuano ya Kombe la Dunia, Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya Uingereza, Fabio Capello aliwaambia Nyota wake kutofanya mapenzi na Wake zao, Rafiki zao wa Kike ili kuwa nguvu na kulinda viwango vyao uwanjani. Lakini Uingereza ilitupwa nje ya Michuano hiyo mapema baada ya hatua ya Makundi ya Michuano hiyo mikubwa Ulimwenguni.

Kwa Aliyekuwa Bondia wa Uzito wa Juu, Mike Tyson mnamo mwaka 2017 alieleza alijizuia kujamiana kipindi cha miaka mitano ili kuwa na Kiwango Bora licha yakueleza alikuwa hafahamu chochote kuhusu suala hilo.

Aliyekuwa Bondia mahiri katika historia ya Ngumi, Muhammad Ali, imeelezwa kuwa aliwahi kusema kipindi anajiandaa kupambana Pigano kubwa huwa anajizuia kujamiana kwa wiki sita.
Kocha Mkuu wa Inter Milan, Antonio Conte


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2ObhoSE
via
logoblog

Thanks for reading ANTONIO CONTE AWAFUNDISHA WACHEZAJI WAKE KUJAMIANA

Previous
« Prev Post