Ticker

10/recent/ticker-posts

Airtel Africa yaingia ushirikiano na Mastercard kuwezesha wateja wa Airtel Money kufanya malipo kidigitali

• Wateja wa Airtel Money, hata wale ambao hawana akaunti za benki kwa sasa wanaweza kufanya malipo ya kimtandao/kidigitali wakiwa popote duniani kwa kutumia Airtel Money virtual card

Kampuni ya simu za mkononi Airtel Tanzania  imetangaza kuingia ushirikiano na Mastercard kwa kuzindua huduma ya Airtel Money Mastercard Virtual card ambayo itawawezesha wateja wa Airtel Money kulipia huduma, bidhaa, applikesheni, hoteli, gharama za usafiri pamoja na kulipia huduma za mtandao (kama Netflix) wakati wowote kidigitali zaidi kupitia watoa huduma wote waliounganishwa au wanaokubali malipo kwa Mastercard. Wateja wa Airtel Tanzania wataweza kufurahia huduma hii ya kipekee kutokana na usalama na uhakika kwa kufanya malipo kidigitali popote kupitia ushirikiano huu.

Vile vile, wateja wa Airtel Money wataweza kufanya malipo binafsi kwa watoa huduma popote kwa kutumia huduma ya Quick Response (QR) kwa wauzaji wa bidhaa mbalimbali au watoa huduma kupitisha QR akaunti ya Airtel Money au kuandika namba ya wakala/mtoa huduma anaekubali malipo kwa Mastercard .

Uzinduzi wa huduma hii unalenga kuendelea kukuza sekta ya fedha hapa Tanzania huku taarifa za hivi karibuni za Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) zikionesha kuwa, nchini Tanzania watumiaji wa huduma za fedha kupitia mitandao ya simu za mkononi wanaongezeka ambapo hadi kufikia mwezi machi mwaka huu wamefikia takribani milioni 22 wakiwa wamefanya miamala inayofikia thamani ya zaidi ya TZS trilioni 8. 

Vile vile, kwa miaka ya hivi karibuni, kumekuwa na maendeleo makubwa katika baadhi ya huduma kama utumaji wa fedha kupitia mitandao mbalimbali kutoka ule wa zamani uliokuwa ukifanyika kwa kumtuma mtu ili kusafirishae fedha ndani au nje ya nchi, ubunifu umefanyika hata kwenye kununua muda wa maongezi kwa mtandao na hivyo kufanya huduma ya fedha wa njia ya mtandao kuwa moja ya huduma yenye tija katika sekta ya kifedha nchini.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati wa kuzindua huduma hiyo ya Airtel Money Mastercard Virtual card, Mkurugenzi wa Airtel Money Isack Nchuda alisema “Kwa sasa tunaishi kwenye dunia ambapo malipo yanafanyika kila sekunde. 

Ushirikiano wetu na Mastercard unatufanya tuendelee kukamilisha dhamira yetu ya kutoa huduma na bidhaa ambazo ni za kipekee na zenye unafuu zaidi ili kukidhi mahitaji ya kila siku ya wateja wetu.’ Alisema Nchunda huku akiongeza kuwa uzinduzi wa Airtel Money Mastercard Virtual card unaonyesha ni kiasi ngani Airtel inaunga mkono juhudi za Serikali za kurahishisha na kupanua sekta na huduma za kifedha hapa nchini.

Airtel Money Mastercard inamuwezesha mteja wa Airtel kufanya malipo kwa urahisi kwenye sehemu zote ambazo Mastercard inakubalika hata kama mteja huyo hana akaunti ya benki au kadi ya malipo. Ili mteja wa Airtel Money aweze kupata Airtel Money Mastercard Virtual card piga *150*60# chagua 6 kisha 1 na ufuate maelekezo kuapata Airtel Money Mastercard Yako. Pale Airtel Money Mastercard inapokamilika pia inakuwa tayari kwa malipo ya kupitia mtandao.

Kwa upande wake, Makamu Rais na Mkurugenzi wa Biashara Afrika Mashariki wa Mastercard Adam Jones alisema “Ushirikiano wetu na Airtel utarahishisha huduma za kifedha kwa mamilioni ya Watanzania. Kwa kupitia ushirikiano wetu huu wa huduma za kidigitali, nia yetu ni kuendelea kuboresha utoaji huduma kiditali zaidi kwa kuzingatia urahisi, unafuu na usalama ili kuifanya Tanzania kuwa nchi ya kidigitali. 

Mastercard ni njia ya malipo kwa mtandao inayotumia teknolojia ya kisasa kwa kushirikiana na washirika wake ukanda wa kati pamoja na bara la Afrika kwa lengo la kumfanya mteja kufurahia huduma za kimataifa za malipo”.

“Huduma za fedha kwa mitandao ya simu imesaidia sana kupuguza gharama za miamala na kuongeza ukuaji wa uchumi kwa kuondoa gharama za kusafiri mpaka kwenye matawi ya benki ili kufanya miamala ya malipo. Airtel Money Mastercard sasa itapanua wingo wa matumizi ya akaunti za Airtel Money kufanya malipo kwa njia ya mtandao, alisema Jones.

Airtel Money Tanzania kwa sasa imeunganisha kwa zaidi ya watoa huduma 1000 pamoja na taasisi za kifedha zaidi ya 40 kwa kumfanya mteja kutoa na kuweka fedha. Vile vile, Airtel inazidi kutanua wigo wake hapa nchini kwa kuwa na Zaidi ya Airtel Money branch 80ambazo zinatoa huduma na bidhaa za Airtel.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Selcom Sameer Hirji alisema taasisi yake imejipanga vyema na kwakudhihirisha hilo kwa inaendelea kuwekeza kwenye miundo mbinu na kujiweka kwenye sehemu nzuri kwenye soko ili kuendelea kutoa huduma ya malipo ya uhakika kwa washirika wake kama Mastercard na Airtel ambao dhamira zao ni kutoasuluhisho kwenye huduma za malipo. 

“Selcom imekuwa moja ya taasisi imara kwenye huduma ya malipo kwa zaidi ya muongo mmoja na kutoa mageuzi makubwa kwenye malipo ya kimtandao hapa nchini na wakati tukiendelea kukua tunakua pamoja na washirika wetu kwenye kurahshisha malipo ykidigitali.

“Matokeo ya uzinduzi huu wa Airtel Money Mastercard ni mafanikio makubwa sana kwa kuwa utarahisisha mambo mengi kwa wateja wa Airtel Money”.alimaliza kusema Sameer.
Mkurugenzi wa Airtel Money Isack Nchuda akiongea leo jijini Dar es Salaam wakati wa kuingia ushirikiano na Mastercard kwa kuzindua huduma ya Airtel Money Mastercard Virtual card ambayo itawawezesha wateja wa Airtel Money kulipia huduma, bidhaa, applikesheni, hoteli, gharama za usafiri pamoja na kulipia huduma za mtandao wakati wowote kidigitali zaidi kupitia watoa huduma wote waliounganishwa au wanaokubali malipo kwa Mastercard. 
Makamu Rais na Mkurugenzi wa Biashara Afrika Mashariki wa Mastercard Adam Jones wakati wa kuingia ushirikiano na Mastercard kwa kuzindua huduma ya Airtel Money Mastercard Virtual card ambayo itawawezesha wateja wa Airtel Money kulipia huduma, bidhaa, applikesheni, hoteli, gharama za usafiri pamoja na kulipia huduma za mtandao wakati wowote kidigitali zaidi kupitia watoa huduma wote waliounganishwa au wanaokubali malipo kwa Mastercard. 
Mkurugenzi wa Mawasiliano Airtel Tanzania Beatrice Singano akisisitiza jambo wakati wa kuingia ushirikiano na Mastercard kwa kuzindua huduma ya Airtel Money Mastercard Virtual card ambayo itawawezesha wateja wa Airtel Money kulipia huduma, bidhaa, applikesheni, hoteli, gharama za usafiri pamoja na kulipia huduma za mtandao wakati wowote kidigitali zaidi kupitia watoa huduma wote waliounganishwa au wanaokubali malipo kwa Mastercard .


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/36UULtc
via

Post a Comment

0 Comments