Ticker

10/recent/ticker-posts

AFISA UTUMISHI MANYONI KIZIMBANI KWA TUHUMA ZA KUBAKA WANAFUNZI WAWILI WA DARASA LA SITA

Na Jumbe Ismailly MANYONI 

AFISA utumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Manyoni,Mkoani Singida,Benjamen Mombeki (59) amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wilaya ya Manyoni akikabiliwa na tuhuma za kubaka wanafunzi wawili wa shule ya msingi Manyoni.

Shauri hilo la jinai namba 167/2019 na namba 168/2019 lipo mbele ya Hakimu wa Mahakama hiyo,Stela Thomasi Kiama.

Mwendesha Mashtaka wa jeshi la polisi,Nasoro Saidi alidai kwamba katika shitaka la kwanza lenye usajili namba 167/2019 inadaiwa kuwa aug,15,mwaska huu saa nne asubuhi kwenye maeneo ya mjini Manyoni,mshitakiwa alimbaka mwanafunzi wa darasa la sita (jina limehifadhiwa) katika shule ya msingi Manayoni.

Mwendesha Mashtaka wa jeshi la polisi alidai kwamba katika shitaka la pili lenye namba za usajili 168/2019 linalomkabili afisa utumishi Mombeki ni kwamba aug,15,mwaka huu saa nne asubuhi kwenye maeneo ya Mjini Manyoni,mshitakiwa huyo alimbaka mwanafunzi wa darasa la sita katika shule ya msingi Manyoni(jina tunalo).

Hata hivyo Mombeki aliposomewa mashtata hayo yote mawili alikana na yupo nje kwa dhamana hadi disemba,05,mwaka huu kesi hiyo itakapoanza kusikilizwa.


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2Ov5ke6
via

Post a Comment

0 Comments