WATUMISHI WA UMMA WATAKIWA KUENDANA NA WAKATI KIUTENDAJI

  Masama Blog      
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb), Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Mhe. Aggrey Mwanri na Balozi wa Sweden nchini Tanzania, Mhe. Anders Sjoberg wakiungana na wanafunzi na watumishi wa Chuo cha Utumishi wa Umma, Kampasi ya Tabora na wageni wengine kucheza muziki uliokuwa ukitumbuizwa na bendi ya Msange JKT wakati wageni hao walipotembelea Chuo cha Utumishi wa Umma Kampasi ya Tabora jana kwa lengo la kuona maendeleo ya chuo hicho kilichojengwa kwa ushirikiano wa Serikali ya Tanzania na Sweden mwaka 1970. Kulia kwa Mkuu wa Mkoa ni Mtendaji Mkuu na Mkuu wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania, Dkt. Emmanuel Shindika.
Mkufunzi Msaidizi wa Chuo cha Utumishi wa Umma, Kampasi ya Tabora, Bw. Alex Massengo akiwaonyesha Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb), Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Mhe. Aggrey Mwanri na Balozi wa Sweden nchini Tanzania, Mhe. Anders Sjoberg matukio mbalimbali katika picha yakiwemo yanayohusu ushirikiano wa Serikali ya Tanzania na Sweden katika kujenga Chuo cha Utumishi wa Umma, Kampasi ya Tabora wakati wageni hao walipotembelea Chuo cha Utumishi wa Umma Tawi la Tabora jana kwa lengo la kuona maendeleo ya chuo hicho.Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Mhe. Aggrey Mwanri akielezea historia fupi ya Mkoa wa Tabora kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) na Balozi wa Sweden nchini Tanzania, Mhe. Anders Sjoberg walipomtembelea ofisini kwake jana kabla ya kutembelea Chuo cha Utumishi wa Umma, Kampasi ya Tabora kwa lengo la kuona maendeleo ya chuo hicho kilichojengwa kwa ushirikiano wa Serikali ya Tanzania na Sweden mwaka 1970. Kushoto kwa Naibu Waziri ni Mkuu wa Wilaya ya Tabora Mjini, Mhe. Kitwala Komanya.

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akiongozana na Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Mhe. Aggrey Mwanri na Balozi wa Sweden nchini Tanzania, Mhe. Anders Sjoberg kuingia Chuo cha Utumishi wa Umma Kampasi ya Tabora jana kwa lengo la kuona maendeleo ya chuo hicho kilichojengwa kwa ushirikiano wa Serikali ya Tanzania na Sweden mwaka 1970. Kulia kwa Mkuu wa Mkoa ni Mtendaji Mkuu na Mkuu wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania, Dkt. Emmanuel Shindika.

Mkuu wa Idara ya Uhazili, Chuo cha Utumishi wa Umma, Kampasi ya Tabora, Bw. Given Simkwai akiwaonyesha Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb), Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Mhe. Aggrey Mwanri na Balozi wa Sweden nchini Tanzania, Mhe. Anders Sjoberg umuhimu wa matumizi ya hati mkato wakati wageni hao walipotembelea Chuo cha Utumishi wa Umma, Kampasi ya Tabora jana kwa lengo la kuona maendeleo ya chuo hicho kilichojengwa kwa ushirikiano wa Serikali ya Tanzania na Sweden mwaka 1970.

***********************************

Na Mary Mwakapenda, Tabora

18 Oktoba, 2019

Watumishi wa Umma nchini wametakiwa kubadilika kiutendaji ili kuendana na
kasi ya mabadiliko mbalimbali yanayotokea hivi sasa duniani kwa lengo la
kuliletea taifa letu maendeleo.

Hayo yalisemwa jana na Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi
wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) wakati wa ziara
yake ya kikazi na Balozi wa Sweden nchini Tanzania, Mhe. Anders Sjoberg
iliyolenga kuangalia maendeleo ya Chuo cha Utumishi wa Umma, Kampasi ya
Tabora kilichojengwa mwaka 1970 kwa ushirikiano wa Serikali ya Tanzania
na Sweden.

Mhe. Dkt. Mwanjelwa amesema hivi sasa kila kitu kinabadilika duniani
ikiwemo uchumi, maisha na teknolojia, hivyo watumishi wa umma hawana
budi kubadilika kulingana na wakati uliopo, kwa mantiki hiyo ni lazima wawe
wabunifu na kuacha kufanya kazi kwa mazoea hatimaye taifa liweze
kunufaika na mchango wao.

“Kama katika sekta binafsi wanafanya kazi ipasavyo kwanini katika Sekta ya
Umma tushindwe? ikizingatiwa kuwa wananchi ambao ndio walengwa wakuu
wanahitaji huduma kutoka serikalini na waliopewa dhamana ya kuwahudumia
ni sisi,” Mhe. Dkt. Mwanjelwa alihoji na kuongeza kuwa, ndio maana Serikali
ya Awamu ya Tano chini ya Uongozi makini wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli inasisitiza na kuiishi
kauli mbiu ya Hapa Kazi Tu ili watumishi wa umma wawe na tija kwa taifa.

Aidha, Mhe. Dkt. Mwanjelwa amewasisitiza watumishi na wanafunzi wa Chuo
cha Utumishi wa Umma kila mmoja kwa nafasi yake kutekeleza wajibu wake
ipasavyo ili kutimiza malengo waliyojiwekea.

“Ukiwa mwanafunzi soma kwa bidii na mtumishi fanya kazi kwa bidii ili
kutimiza ndoto yako kwani Serikali inataka Chuo cha Utumishi wa Umma
Tanzania kiendelee kutoa mchango katika maendeleo ya taifa na kuwa mfano
bora wa kuigwa na vyuo vingine” Mhe. Dkt. Mwanjelwa aliongeza.

Akitoa salamu za Mkoa wa Tabora, Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Mhe. Aggrey
Mwanri amemshukuru Naibu Waziri na Balozi Sjoberg kwa ujio wao kwani
unaendelea kudumisha ushirikiano baina ya Tanzania na Sweden ambao
ulianza tangu Serikali ya Awamu ya Kwanza mpaka sasa.

Mhe. Mwanri amewaasa wanafunzi wa chuo hicho kutumia vema ujuzi
watakaoupata kwa manufaa yao na maslahi ya taifa na kuongeza kuwa chuo
hicho kina historia ya kutoa viongozi bora huku akitoa mfano wa baadhi ya
viongozi waliosoma hapo na kupata mafanikio makubwa akiwemo Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu na Mke
wa Rais wa zamani wa Zimbabwe, Hayati Robert Mugabe, Mama Grace
Mugabe.

Kwa upande wake, Balozi wa Sweden nchini Tanzania Mhe. Anders Sjoberg
alishukuru kwa mapokezi mazuri aliyoyapata na kuwaasa wanafunzi na
watumishi wa chuo hicho kutekeleza wajibu wao ipasavyo, na hakusita
kupongeza juhudi zinazofanywa na Serikali ya Tanzania za kukiendeleza
chuo hicho.

Ziara hiyo ilitoa fursa kwa viongozi hao kutembelea maktaba ya kumbukumbu,
maktaba, chumba cha Kompyuta, darasa la kupiga chapa, mabweni ya
wanafunzi na jengo jipya la utawala linalojengwa kwa fedha za ndani ambalo
limekamilika kwa asilimia 94 kwa gharama ya shilingi bilioni 2.7.


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2pA07bT
via
logoblog

Thanks for reading WATUMISHI WA UMMA WATAKIWA KUENDANA NA WAKATI KIUTENDAJI

Previous
« Prev Post