DOWNLOAD APP YETU HAPA

Washtakiwa Raia wa Kigeni wahukumiwa kulipa faini ya sh.Milioni 100 au kwenda jela miezi 12

  Masama Blog      
HAKIMU Mkazi wa Mahakama ya Wilaya Arusha Rose Ngoka amewahukumu washitakiwa kumi ambao ni raia wa kigeni, kulipa Sh.milioni 100 au kwenda jela miezi 12, kwa kosa kufanya kazi kampuni ya uwindaji ya Oterlo Businness Coperation (OBC) bila kuwa na kibali cha kufanya kazi nchini.

Ametaja majina ya raia hao kuwa ni Darweshi Jumma, Riaz Aziz Khan, Mohammad Tayyab, Ali Bakhash, Abdulrahman Mohammed, Martin Crasta, Imtiaz Feyaz, Arshad Muhammad, Hamza Sharif na Zulfiqar Ali.

Hakimu Ngoka amesema mahakama imewatia hatiani washitakiwa hao kwa kukiri kufanya kosa hilo nchini na kuamuru kila mmoja kulipa faini ya Sh.milioni 10 au kwenda jela miezi 12.

"Kwa kuzingatia maombi ya Wakili wenu wa utetezi Steven Mosha na kwa kuangalia mazingira ya kesi na madhara ya kijamii kama alivyosema mahakama imekata hatiani na kuwapa adabu hiyo ili iwe fundisho kwa wengine,"alisema

Amesema mbali na kuwapa adhabu ya kulipa faini,pia aliwaonya washitakiwa hao na kuwataka kutii sheria,kanuni na taratibu za nchi pindi wanapoingia nchini.

Steven Mosha ni wakili wa utetezi kabla ya hukumu hiyo kutolewa ameiomba Mahakama hiyo kuwapa adhabu ndogo washitakiwa hao kwa sababu ni kosa lao la kwanza kufanya.

" Naomba Mahakama iwapunguzie adhabu sababu wamekiri na kuokoa muda wa mahakama,lakini pia washitakiwa wawili wana utaifa wa nchi ya India na nane raia wa Pakstani na walishitakiwa miezi mingi nyuma na kutumia gharama kubwa za kuishi,"alisema

Amesema kutokana na kushitakiwa wamelazimika kutumia fedha nyingi katika kuishi nchini na wengi wao vijana wanahitajika katika taifa lao kujenga taifa." Hakimu naomba wape adhabu ndogo sababu wengine umri wao mkubwa wanahitaji kukaa wanafamiliya zao,"alisema

Aidha amesema kuwapa adhabu kubwa itasababisha ugumu wa maisha kwa familia zao,hivyo aliomba wapewa adhabu ya kulipa fedha kwa sababu wapo tayari kulipa kiasi chochote cha fedha ambacho mahakama hiyo itaamuru.

Kabla ya Wakili wa utetezi kutoa maombi hayo Wakili Mkuu wa Serikali Maritenus Marandu amesema kabla ya jana washitakiwa hao waliandika barua iliyowasilishwa na Wakili wao Steven Mosha ikionyesha washitakiwa hao kukiri makosa yao.

Pia aliiambia mahakamani hiyo kuwa, upande wa Jamuhuri hauna kumbukumbu za makosa ya nyuma,ila aliomba mahakama iwape adhabu inayostahili kulingana na kosa walilofanya.

Akiwakumbusha washitakiwa hao makosa yao Wakili Mwandamizi wa serikali Mkoa wa Arusha Abdallah Chavula akiwa na Wakili Idara ya Kazi Arusha Emmanuel Mweta amesema washitakiwa hao walifanya kosa la kufanya kazi nchini bila vibali vya kazi kati ya Novemba 2018 na Januari 2019.

Washitakiwa hao wenye taaluma mbalimbali walikamatwa wakiwa na hatia zao zà kusafiria wakijiandaa kuondoka nchini.

Washitakiwa hao walikamatwa Januari mwaka huu na Septemba 2 mwaka huu kesi hiyo ilifutwa na Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Mfawidhi Arusha Niku Mwakatobe kutokana na Wakili wa serikali kutokuwa tayari kuwasomea hoja za awali ili kesi iendelee.

Wakati huo huo mshitakiwa wa kwanza Isaya Mollel katika kesi hiyo ambaye ni Mkurugenzi wa OBC anayekabiliwa na kosa la kuajiri raia hao wa kigeni, bila ya kuwa na vibali kwa mujibu wa sheria za nchi za kutoa ajira kwa wageni hajakiri kosa na amepangiwa kesi yake Oktoba 16 mwaka huu.

Washitakiwa hao walifanikiwa kulipa faini hiyo na kuachwa huru.


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2o3AsIB
via
logoblog

Thanks for reading Washtakiwa Raia wa Kigeni wahukumiwa kulipa faini ya sh.Milioni 100 au kwenda jela miezi 12

Previous
« Prev Post