WADAU WAKUTANA KUJADILI MABADILIKO YA TABIANCHI ILI KUPANGA MIKAKATI YA KUKABILIANA NA MABADILIKO HAYO

  Masama Blog      

Na Said Mwishehe,Michuzi Blog 

WADAU mbalimbali wa mabadiliko ya tabianchi wamekutana jijini Dar es Salaam kwa lengo la kutafakari na kupanga mikakati itakayotoa msimamo ya jinsi gani nchi zinazoendelea na zisizoendelea zitakavyoweza kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi katika kipindi cha sasa.

Mikakati hiyo itakayotolewa na wadau hao na kufanya baadhi ya mada mbalimbali walizozijadili kuweza kuwasilishwa katika mkutano wa kimataifa wa 25 ya mabadiliko ya tabianchi na kuona ni hatua gani kama dunia itaweza kuchukuliwa katika kukabiliana na hali ya mabadiliko ya tabia nchi.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa Programu kutoka Taasisi inayohusu masuala ya mabadiliko ya tabianchi(FORUMCC),Angella Damas wakati wa mkutano huo uliowakutanisha watu kutoka Asasi mbalimbali za kiraia na wadau kutoka serikalini kujadili mapendekezo hayo watakayo yatoa kwa pamoja na kuyawasilisha kwa ngazi ya taifa na kisha kupelekwa katika mkutano huo wa kimataifa .

Amefafanua kuwa mkutano huo wa wadau umepata fursa ya kushirikiana na na Shirika la FORUMCC pamoja na African Climate Justice Alliance (PACJA) Kwa udhamini wa Shirika la Kimataifa la Ushirikiano wa Maendeleo ya Swedish (SIDA)chini ya mradi ujulikanao Kwa jina la kuimarisha Ushiriki wa asasi za kiraia katika Majadiliano na Majibu ya Mabadiliko ya tabianchi ya Matokeo ya Mkataba wa Paris pamoja na mradi WA "nishati ya kijani ya pamoja unaofadhiliwa na Shirika la Hivos unaongeza uwajibikaji wa serikali juu ya fedha za hali ya hewa kwa nishati mbadala.

Amesema wadau hao watawapa fursa kutoka na msimamo mmoja utakaofanya kuwa na mapendekezo yatakayowasilishwa katika mkutano huo na kujadiliwa kidunia.

Ameongeza miongoni mwa maazimio hayo ni pamoja na masuala ya Kilimo ambayo yataonyesha sekta hiyo ya kilimo kuwezwa kulindwa na kuwekewa ulinzi ili kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

“Mkutano huu wa kimataifa wa COP 25 ni muendelezo wa mikutano mbalimbali ilizopita ikiwemo ya Makubaliano ya mkutano wa Paris wa masuala ya tabianchi ambapo uliozungumzia masuala ya upungufu wa nyuzi joto kidunia, kwa nchi zinazoendelea na zilizoendelea na kutaka baadhi ya nchi zinazoendelea kuchangia fedha kwaajili ya kupunguza athari za mabadiliko ya tabianchi kwa nchi zinazoendelea,"amesema

Alisema Mabadiliko ya tabia nchi ni mabadiliko ya wastani ya joto ambayo wastani huo unaangaliwa kuanzia miaka 30 ya nyuma hadi sasa.

“Kabla masuala ya uwepo wa viwanda tulikuwa katika nafasi nzuri ya masuala ya nyuzi joto ila tulipoanza kuwa na mapindunzi ya viwanda kuanzia miaka 60 hadi sasa hali imebadilika tumetoka katika nyuzi joto 0.4 hadi kufikia 0.9,”alisema Damas

Kwa Upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sokoine,Fazal Issa ameeleza kuwa kuelekea mkutano wa 25 wa kimataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi mambo mengi yataenda kujadiliwa na miongoni yake yapo yanayotolewa kipaumbe katika nchi ya Tanzania.

“Katika Mkutano wa mwaka jana wa 24 ulikubaliwa namna ya kutekeleza mkataba wa paris wa masuala ya tabianchi ikiwemo masuala ya fedha ambayo ilikubaliana nchi zilizoendelea kuongeza kiwango cha kutoa fedha ili kusaidia nchi zinazoendelea kukabiliana na mabadiliko hayo,”alisema na kuongeza

"Fedha hizo ni muhimu sana katika kusaidia kuondoa changamoto za mabadiliko ya tabianchi ambazo pia changamoto hizo zinakwamisha jitihada za kupambana na umasikini," amesema

Aidha ameongeza katika mkutano huo wa 24 uliweza kuangazia masuala ya sekta ya kilimo na kudai kuwa suala la utekelezaji wa sekta hiyo kuwekewa kipaumbele katika katika uhimili wa mabadiliko ya tabianchi na sio kupunguza gesi joto.

Issa amefafanua kwamba suala la teknolojia ni miongoni mwa suala linalotakiwa kutiliwa mkazo katika upunguzaji wa gesi joto na pia kuweka uhimili wa mabadiliko ya tabia nchi kwa kuweka misingi ndani ya miaka Sita .from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2N5V4rV
via
logoblog

Thanks for reading WADAU WAKUTANA KUJADILI MABADILIKO YA TABIANCHI ILI KUPANGA MIKAKATI YA KUKABILIANA NA MABADILIKO HAYO

Previous
« Prev Post