Ticker

10/recent/ticker-posts

VILABU 40 KUSHIRIKI MASHINDANO YA DRAFT IRINGA

Baadhi ya wachezaji wa mchezo wa kusukuma kete (Draft) katika kijiwe cha M.R. wakiendelea kupambana katika michezo kutafuta bingwa wa mchezo huo mkoa wa Iringa. (Picha na Denis Mlowe) .

***********************************

NA DENIS MLOWE,IRINGA

JUMLA ya Vilabu 40 vimejitokeza kushiriki mashindano ya kutafuta bingwa wa mchezo wa kusukuma kete (draft) manispaa ya Iringa yanayojulikana kwa jina la Ngajilo Draft Championship 2019 yaliyozinduliwa rasmi juzi katika kijiwe cha M.r Hotel.

Mratibu wa mashindano hayo, Temihanga Kabambe alisema kuwa mashindano hayo yameandaliwa kwa lengo la kuwakusanya watu pamoja mara baada ya kazi za kutwa kuchwa kuweza kudumisha umoja na amani kwa manispaa ya Iringa na kukutanisha wadau wa mchezo huo na kuleta mwamko kwa jamii kushiriki mchezo huo.

Kabambe alisema kuwa mchezo wa draft ni miongoni mwa michezo inayopendwa na kila rika ambapo amewataka wachezaji hao kuungana kwa pamoja na kuutangaza mchezo huo ambao kwa manispaa ya Iringa umekuwa moja ya michezo unaotumika zaidi watu kufahamiana.

Alisema kuwa kutokana na vijiwe vingi kujitokeza katika mchezo huo tofauti na mashindano ya kwanza, mkakati moja wapo ni kukuza mchezo wa draft na kuutambulisha mchezo huo katika ngazi ya kitaifa na kimataifa hivyo 

ili kuinua mchezo huo kuna kila sababu ya kuwa na mashindano ya mara kwa mara kuibua vipaji vitakavyoweza kuutangaza mchezo huo.

Alisema kuwa katika kuandaa mashindano hayo wamefanikiwa kusajili vilabu vyote katika manispaa ya Iringa ambapo vimekubali kushiriki mashindano hayo yenye msisimko mkubwa kwa kuweza kukusanya watu mbalimbali tangu yamezinduliwa katika vilabu husika kuweza kupata mwakilishi atakayeingia kwenye nafasi za kumtafuta bingwa.

Mashindano hayo yanatarajiwa kumalizika Oktoba 19 mwaka huu mgeni rasmi atakuwa mdhamini wa mashindano hayo, Fadhili Ngajilo ambapo timu alizitaja baadhi zinazoshiriki baadhi ni kutoka vilabu vya , Kihesa, Mshindo, Mlandege, M.r, Stand ya Pawaga, Mjimwema, Nduli, Isikalilo, Isoka, Mwangata, Don Bosco na Lukosi.

Alivitaka vilabu vyote kucheza kwa amani kama ambavyo lengo la mashindano hayo kujenge urafiki, amani na kufahamiana ili kuweza kupata bingwa sahihi katika mashindano hayo ambayo hadi sasa washiriki zaidi ya 6 wamejihakikishia kuingia katika fainali za kumtafuta bingwa kutoka katika vilabu wanavyotokea.

Katika mashindano hayo bingwa ataondoka na kitita cha shilingi 500,000 mshindi wa pili sh, laki 200,000 na mshindi wa tatu sh,100,000 huku bingwa wa kila Vilabu atakayeshinda nafasi za kuwakilisha katika kutafuta bingwa wa manispaa ataondoka na sh. 10,000 

Kwa upande wake, mfadhili wa mashindano hayo, Fadhili Ngajilo alisema kuwa mchezo wa kusukuma kete unachezwa na watu wengi katika jamii na mmoja ya michezo inayotumia sana akili katika kuucheza na hata wachezaji wake wana akili hivyo endapo wataanzisha chama chao kitakuwa na umuhimu sana katika jamii hasa kuwakutanisha watu na kubadilishana mawazo.

Ngajilo alisema kuwa mchezo huu wa jadi hauchukuliwi kipaumbele kama ilivyo kwa michezo mingine hali ambayo mkiwekeza katika mtindo wa kisasa zaidi uhakika wa wadau wengine kujitokeza na kudhamini itawezekana kwani moja ya michezo pendwa kwa sasa na rika mbalimbali.

Alisema kuwa mchezo wa draft una changamoto mbalimbali lakini endapo wadhamini wakiwekeza katika mchezo huu ndio asili ya mtanzania kwani ndipo kwenye watu ambao wanajenga uchumi, kujenga jamii iliyobora kutokana na kubadilishana mawazo katika misingi ya kiakili zaidi.

Alisema kuwa lengo la kudhamini mashindano hayo ni kuleta hamasa kubwa na kuchochea watu wengi washiriki katika mchezo wa kusukuma kete lakini pia mchezo wa draft uwe mkubwa zaidi na kuufanya wa kisasa zaidi kwa kuhakikisha kila kata wanashiriki na kutumia kumbi za kisasa zaidi kufanyika kwa mchezo huo.

“Lengo kuufanya mchezo huu kuwa wa kisasa zaidi na mchezo wa draft ni mchezo wa akili sana na kama huna akili huwezi cheza mchezo huu kwani unataka akili sana na kuwe na mahusiano ya akili na viungo aidha unaletea afya ya akili naupenda mchezo huu kwa kuwa unaleta changamoto za akili kuweza kushiriki” alisema

Alisema kuwa endapo wakiamaua kuufanya mchezo huu kisasa zaidi uhakika wa watu wengi kujitokeza zaidi kudhamini hivyo wachezaji ndio chachu ya mafanikio ya mchezo huu kuweza kudhaminiwa na makampuni mbalimbali.

Naye bingwa wa msimu uliopita, Juma Athuman ‘Bin Kulijua’ alisema kuwa anatarajia mwaka huu kuchukua tena ubingwa huo kwa kuwa washiriki wote wanaoshiriki uwezo wao uko chini sana na amejipanga vyema kujishindia sh. laki 5 ambazo zinatolewa na mdhamini wa mashindano hayo Ngajilo.

Athuman alimshukuru mdhamini wa mashindano hayo, Fadhili Ngajilo na kwa kuweza kudhamini mashindano hayo kwani wadau wengi wako zaidi katika michezo mingine na kushindwa kuwafikia mashabiki na wachezaji wa mchezo wa jadi ambao hata mwasisi wa taifa Julias Nyerere alikuwa anaucheza na kumwahakikishia kwamba watatumia mchezo huo kuweza kuleta changamoto chanya katika jamii na kujenga mshikamano.


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/320XkXQ
via

Post a Comment

0 Comments