Ticker

10/recent/ticker-posts

VIJANA WILAYANI RUAGWA WAPONGEZA SERIKALI KWA KUWAWEZESHA STADI ZA KILIMO CHA KISASA

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akieleza jambo alipokuwa akigagua Kitalu nyumba kilichojegwa katika Kijiji cha Chimbila “A” kilichopo Wilayini Ruangwa. Kulia ni Bw. Lucas Mwindima ambaye ni mmoja wa wanufaika wa mafunzo hayo.





Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akizungumza na vijana walionufaika na mafunzo ya ukuzaji ujuzi kupitia teknolojia ya kitalu nyumba (Greenhouse) katika kijiji cha Chimbila “A” alipotembelea eneo hilo kukagua maendeleo ya mafunzo hayo Wilayani Ruangwa.
Sehemu ya Vijana walionufaika na Mafunzo hayo ya Kilimo cha Kisasa kwa kutumia teknolojia ya Kitalu Nyumba wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama (hayupo pichani) alipowatembelea kwa ajili ya kukagua maendeleo ya mafunzo yao.
Bw. Lucas Mwindima ambaye ni mmoja wa wanufaika wa mafunzo hayo akitoa taarifa fupi kuhusu mafanikio waliyopata kupitia teknolojia ya kilimo cha Kitalu Nyumba.

Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira Mhe. Anthony Mavunde akizungumza na vijana wa Kikundi cha Ruwangwa Materials wanaojihusisha na utengenezaji wa matofali walipotembelea kikundi hiko kukagua maendeleo ya mradi wao. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa Mhe. Hashim Mgandilwa.


Kiongozi wa Kikundi cha Ruagwa Materials Bw. Mohammed Moshi akisoma taarifa fupi kuhusu utekelezaji wa mradi wao walipotembelewa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama. (Wa tatu kutoka kulia) ni Waziri wa Vijana, Utamaduni, Sanaa na Michezo kutoka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Balozi Ali Abeid Karume na Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira Mhe. Anthony Mavunde. Kushoto ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Andrew Massawe.


Baadhi ya Vijana wa Kikundi cha Ruangwa Materials wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama (hayupo pichani), alipowatembea kwa lengo la kukagua maendeleo ya kikundi hicho.

PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU

(KAZI, VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVU)

……………………………..

Na; Mwandishi Wetu

Vijana Wilayani Ruagwa wameipongeza Serikali kwa kuwawezesha kupata mafunzo ya kilimo cha Kisasa kwa kutumia teknolojia ya kitalu nyumba (Greenhouse) ambayo yamekuwa ni chachu kwao kujikwamua kiuchumi.

Pongezi hizo zimetolewa Oktoba 11, 2019 wakati wa ziara ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama alipotembelea vijana hao katika Kijiji cha Chimbila “A” kilichopo Wilaya ya Ruagwa kukagua maendeleo ya mafunzo waliyopata vijana kupitia teknolojia ya Kitalu Nyumba.

Mheshimiwa Mhagama alieleza kuwa Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu imeonesha kuwajali, kuwatambua na kuwathamini vijana kwa kuwapatia mafunzo hayo ambayo yamekuwa yakiwasaidia sana katika kuwaendeleza vijana kulima kwa mkakati.

“Mafunzo hayo yamewajengea uwezo vijana wa kushiriki kwa wingi kwenye kilimo cha aina hii kwa kuwa kinatija na ufanisi, hivyo vijana watakuwa kupata mavuno zaidi katika eneo dogo kuliko eneo la wazi, uwezo wa kupata soko la mazao utakuwa wa uhakika, matumizi ya maji ni madogo katika kilimo hiko na hudhibiti viwatilifu,” alisema Mhagama

Alieleza kuwa Ofisi ya Waziri Mkuu ilianzisha Programu ya Ukuzaji Ujuzi ikiwemo mafunzo hayo ya kilimo cha Kisasa ikiwa ni mkakati wa serikali baada ya kubaini asilimia 56 ya nguvukazi nchini ambao ni vijana wamekuwa na changamoto ya ajira, katika kutatua changamoto hiyo kundi hilo limewezeshwa kwa kujengewa uwezo wa kupatiwa ujuzi katika fani mbalimbali.

Waziri Mhagama aliongeza kuwa Mafunzo hayo ya kilimo kupitia teknolojia ya kitalu nyumba yatawasaidia kuboresha stadi bora za kilimo kwa vijana hususan waliopo vijijini ili waweze kujiajiri, kuajiri wenzao na kushiriki katika shughuli mbalimbali za kimaendeleo.

Aidha aliwasihi vijana kuendelea kutunza vitalu nyumba hivyo kwa kuwa watanufaika kiuchumi na sambamba na kuwaleta maendeleo yao na jamii kwa ujumla.

Baadhi ya vijana walionufaika na mradi huo akiwemo Bw. Lucas Mwindima alisema kuwa Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Mhe. Rais, Dkt. John Pombe Magufuli imeonesha dhamira ya dhati katika kuwawezesha vijana wanapata ujuzi utakaowawezesha kukuza ujuzi wao na kuwaondoa katika hali ya umaskini.

“Tunamshukuru Rais Magufuli kwa kutuwezesha vijana kupata mafunzo haya ya kilimo cha kitaalamu yaliyoleta tija tunaona uzalishaji wa mazao ulivyokua tofauti na zamani na mazao tunayozalisha yanafursa ya kupata masoko ndani au nje ya nchi,” alisema Mwindima

Katika kupongeza jitihada hizo wanufaika wa programu ya kilimo hicho walibainisha mafanikio mbalimbali ikiwemo kupata ujuzi wa kilimo cha mazao biashara pamoja na ongezeko la ajira kwa vijana waliowezeshwa elimu hiyo.

Pia Waziri Mhagama alitembelea kikundi cha Ruangwa Materials ambacho kimenufaika na Mkopo wa Maendeleo ya Vijana unaoratibiwa na Ofisi yake kupitia Idara ya Manedleo ya Vijana.


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2OGa428
via

Post a Comment

0 Comments