Ticker

10/recent/ticker-posts

UJENZI HOSPITALI YA RUFAA YA KWANGWA MUSOMA KUKAMILIKA MWAKANI

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula (Wa pili kulia) akioongozwa na Kaimu Mkurugenzi Ubunifu Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Magret Ezekiel (kulia) kukagua maendeleo ya ujenzi wa mradi wa Hospitali ya Rufaa ya Kwangwa Musoma mkoa wa Mara jana wakati wa ziara yake mkoani humo. Mradi huo unajengwa na Shirika la Nyumba la Taifa.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula (Wa pili kulia) akitoa maelekezo kwa Kaimu Mkurugenzi Ubunifu Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Magret Ezekiel (kulia) kabla ya kuanza kufanya ukaguzi wa maendeleo ya ujenzi wa mradi wa Hospitali ya Rufaa ya Kwangwa Musoma mkoa wa Mara jana. Katikati ni Katibu Tawala mkoa wa Mara Carlone Mtapula.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula (Wa pili kulia) akipata maelezo kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi Ubunifu Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Magret Ezekiel (kulia) kabla ya kuanza kufanya ukaguzi wa maendeleo ya ujenzi wa mradi wa Hospitali ya Rufaa ya Kwangwa Musoma mkoa wa Mara jana. Wa pili kulia ni Katibu Tawala mkoa wa Mara Carlone Mtapula.

………………….


Na Munir Shemweta, WANMM MUSOMA

Ujenzi wa Mradi wa Hospitali ya Rufaa ya Kwanga iliyopo Musoma mkoa wa Mara unaojengwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) na kugharimu zaidi ya shilingi Bilioni 15 unatarajiwa kukamilika Agosti 2020.

Hayo yameelezwa jana mjini Musoma na Kaimu Mkurugenzi wa Ubunifu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Margret Ezekiel wakati akitoa taarifa ya maendeleo ya uendelezaji ujenzi wa mradi wa hospitali hiyo kwa Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula wakati wa ukaguzi wa maendeleo ya ujenzi wa jengo hilo,

Margret alisema, jengo hilo lenye mita za mraba 24482 na majengo mengine ya pembeni yenye mita za mraba 1039 lina sehemu kuu tatu zinazojumisha sehemu zenye ghorofa tano, nne na sehemu ya tatu ghorofa mbili.

Alisema, ujenzi wa mradi wa hospitali ya Kwangwa ulianza septemba 2019 na kuchelewa kuanza kwa ujenzi wa mradi huo kulitokana na changamoto ya upatikanaji wa michoro ya kujengea pamoja na kutokamilika kwa mchakato wa kumpata Mshauri Mwelekezi wa mradi.

‘’jengo hili ambalo limepitia wakandarasi wawili kabla ya shirika letu kukabidhiwa limefanyiwa maboresho ili kuwa na huduma zote kadri ya hospitali ya Rufaa inavyotakiwa’’. Alisema Margaret

Kwa mujibu wa Kaimu Mkurugenzi huyo Ubunifu wa NHC, kazi za ujenzi zinazoendelea kwa sasa ni pamoja na kupiga lipu katika katika maeneo yote ambayo hayatakuwa na marejkebisho , kuvunja baadhi ya kuta na kuzijenga kwa mujibu wa marekebisho sambamba na kuandaa sehemu ya nyongeza,

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula alisema kukamilika kwa jengo la hospitali ya Rufaa la Kangwa itakuwa mkombozi kwa wananchi wa mkoa wa Mara ambao baada ya kukamilika ujenzi watakuwa wakipata huduma za hospitali ya rufaa katika mkoa huo tofauti na awali ambapo waanalazika kwenda hadi Bugando mkoani Mwanza.

‘’ Tunaishukuru serikali ya awamu ya tano chini ya Rais John Pombe Magufuli kwa kufanikisha kutoa kiasi cha zaidi ya bilioni 15 kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa jengo hilo ambao ulisimama kwa muda mrefu kuanzia mwaka 2011’’ alisema Dkt Mabula.

Amelitaka shirika la Nyumba la Taifa kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Mara kuhakikisha kuchelewa kwa Mshauri Mwelekezi wa ujenzi wa jengo hilo hakucheleweshi ujenzi wa ujenzi wa mradi wa hospitali hiyo.

Katika hatua nyingine, Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula ameitaka Kampuni ya Kiure Engineering ianyojenga jengo la kitega uchumi la Shirika la Nyumba la Taifa la Mkendo Plaza kuhakikisha inakamilisha ujenzi wa jengo hilo la ghorofa tano ifikapo Desemba 30 2019 vinginevyo mkataba wa ujenzi wa jengo hilo utavunjwa bila kujali kama kampuni hiyo imefikia asilimia ngapi ya ujenzi na kampuni hiyo itatakiwa kurejesha gharama za ujenzi.

Hatua ya Dkt Mabula inafuatia kampuni hiyo ya Kiure kushindwa kukamilisha ujenzi wa jengo hilo tangu kuingia kwa mkataba wa ujenzi mwaka 2015. Kwa mujibu wa Mhandsi wa ujenzi wa jengo hilo, kampuni ya Kiure iliingia mkataba wa ujenzi wa jengo hilo mwaka 2015 na ujenzi kuanza rasmi 2017.


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2MJk1cF
via

Post a Comment

0 Comments