Ticker

10/recent/ticker-posts

UDP yataka Wananchi wajiendikishe katika daftari la uchaguzi wa Serikali za Mitaa

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

MWENYEKITI wa Chama cha (UDP), John Cheyo ametoa rai ya kuwataka  wananchi kushiriki katika uchaguzi wa serikali za mitaa kwani ndiyo chanzo cha maendeleo nchini.

Akizungumza  jijini Dar es Salaam, Cheyo amesema uchaguzi huo ndiyo kichocheo cha kupata viongozi ambao watakaoleta maendeleo katika mitaa kwani na mipango ya taifa yanaanzia katika serikali za mitaa.

Amesema  uchaguzi wa serikali za mitaa una umuhimu kwani  chama cha UDP kitashiriki kikamilifu katika uchaguzi huo wanachama kugombea uenyekiti wa serikali za Mtaa.

Cheyo amesema UDP maendeleo na watashirikiana na serikali katika masuala yote yanayohusu maendeleo.

Cheyo amesema kuwepo kwa vyama vingi si sababu ya kurudisha maendeleo nyuma bali inatakiwa kushirikiana ili kupigania maendeleo.

“Uchaguzi maana yake ni kumchagua yule kiongozi ambaye unamuona ataweza kukuongoza na kukuletea maendeleo ndiyo maana na sisi tutashiriki kikamilifu ili kusaidia wananchi wetu katika matatizo yao mbalimbali”amesema.

Cheyo amemuunga mkono Rais Dkt. John Magufuli kwa kuwajali wanyonge hasa wakulima ambao wamekuwa wakiendesha maisha yao kupitia kilimo.

Amesema baada ya kusikia lile agizo la Rais Magufuli la wakulima hao wa pamba kulipwa pesa zao, alithibitisha kweli Magufuli ni Rais anayejali wanyonge.“Mimi ni mmoja kati ya watu ambao wanaunga mkono wakulima, na baada ya kusikia lile agizo nimefurahi sana  kwani ile ni haki yao ambayo inasaidia kuendesha maisha  siku amesema

Aidha ameiomba serikali kuandaa mipango ya kuuza mazao ya wakulima mapema ili inapofika msimu kusipo kukwama kwa kilimo hicho kutokana na kukosa fedha.

Cheyo pia alimpongeza Rais Magufuli kwa kuwa mkali kuhusu suala la watu kubambikiwa kesi kwani jambo hilo lkimekuwa likimchafua Rais kwa wananchi wake.“Watu wanatakiwa kushitakiwa kwa makosa yaliyona haki na si kumpa mtu tu kesi kisa unamaslahi yako binafsi kwani kufanya hivyo kunamchafuya Rais Magufuli”amesema


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2IKqRNQ
via

Post a Comment

0 Comments