Ticker

10/recent/ticker-posts

TAKUKURU Yamnasa mtuhumiwa waliemsaka tangu mwaka 2017

Charles James, Michuzi TV
TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) imemkamata Be Emmanuel Mziwanda ambaye alikua Afisa Afya Mkuu na Mratibu wa mradi wa Belgian Fund for Food Security (BFFS) wa Halmashauri ya Wilaya ya Bahi ambaye wamekua wakimsaka tangu Juali, 2017.

Mziwanda anakabiliwa na mashtaka ya kutumia nyaraka kumdanganya mwajiri na kuisababishia hasara Serikali ya Shilingi Milioni 15 ambazo TAKUKURU inasema alizipata kwa njia ya udanganyifu.

Akizungumza jijini Dodoma leo, Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Dodoma, Sosthenes Kibwengo amesema baada ya kufanya uchunguzi wao na Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kutoa kibali cha kumfikisha mahakamani Bw Mziwanda alitoweka hadi walipomkamata Oktoba mwaka huu akiwa msibani wilayani Mpwapwa.

" Tunapenda kuwashukuru wananchi wote na wadau walioshirikiana na Taasisi yetu kufanikishwa kukamatwa kwa mtuhumiwa huyu, tutamfikisha Mahakamani muda wowote baada ya taratatibu za kisheria kukamilika," Amesema Kibwengo.

Aidha Katika robo ya Julai hadi Septemba 2019, TAKUKURU Mkoa wa Dodoma imeendelea kutekeleza majukumu yake ambapo wametoa elimu ya rushwa kwa Wananchi hasa Katika kipindi hiki ambacho uchaguzi wa Serikali za Mitaa unakaribia.

Amesema TAKUKURU Mkoa wa Dodoma, imefuatilia miradi 39 ya maendeleo yenye thamani ya jumla ya Shilingi Bilioni 46 katika sekta za ujenzi wa miundombinu, elimu, afya, maji na kilimo ambapo wamegundua viashiria vya uwepo wa uvunjaji wa taratibu kwenye utekelezaji wa miradi minne yenye thamani ya Shilingi Bilioni 1.9.

" Tumeanzisha uchunguzi kuona iwapo kuna vitendo vya rushwa Katika miradi hiyo, Pia tumeingilia kati utekelezaji wa mkataba wa uundwaji wa Kampuni kati ya Halmashauri moja na Taasisi binafsi kwa ajili ya kununua maeneo, kuyapima na kuyauza," Amesema Kibwengo.

Amesema Katika eneo la Kupambana na rushwa kwa kipindi tajwa wamepokea jumla ya tuhuma 155 na makosa yahusianayo ambapo uwiano wa tuhuma hizo kisekta ni kama ifuatavyo.

Kata, Mitaa na Vijiji 39%, Ardhi 13.5%, Elimu 12.3%, Mahamama 7.7%, Wizara 5.8%, Polisi 5.2%, Sekta binafsi 5.2%, Maji 4.5%, ambapo tuhuma zilizobakia zinahusu sekta ya Afya, Uhamiaji, TARURA na vyama vya Siasa.
Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoani Dodoma, Sosthenes Kibwengo akizungumza na wandishi wa habari wakati akitoa taarifa ya robo ya Julai na Septemba ambapo alieleza kukamatwa kwa mtuhumiwa ambaye wamekua wakimsaka kwa zaidi ya miaka miwili.


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2olMmgx
via

Post a Comment

0 Comments