T-PESA WAZINDUWA BANDO LA TAMTAM

  Masama Blog      
Mwenyekiti wa Bodi ya T-PESA, Brigedia Generali mstaafu, Ramadhan Kimweri (katikati) akizungumza kwenye uzinduzi wa huduma mpya ya Bando la TamTam ambalo linampa uhuru zaidi mteja wa TTCL kufurahiya mawasiliano nafuu ya huduma ya maongezi, inatenti pamoja na ujumbe mfupi(SMS) leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa TTCL Corporation, Waziri Kindamba pamoja na Afisa Mkuu wa T-Pesa, Bi. Lulu Mkudde.
Afisa Mkuu wa T-Pesa, Bi. Lulu Mkudde (kushoto) akizungumza kwenye uzinduzi wa huduma mpya ya Bando la TamTam ambalo linampa uhuru mteja wa TTCL kufurahiya mawasiliano nafuu ya muda wa maongezi, inatenti pamoja na ujumbe mfupi(SMS) leo jijini Dar es Salaam. 
Mwenyekiti wa Bodi ya T-PESA, Brigedia Generali mstaafu, Ramadhan Kimweri (kulia) akipongeza moja ya kikundi cha burudani kwenye hafla ya uzinduzi huo. 
Mmoja wa wateja wa TTCL akipata huduma kwenye uzinduzi wa huduma mpya ya Bando la TamTam. KAMPUNI ya T-PESA imezinduwa huduma mpya ya Bando la TamTam ambalo linampa uhuru zaidi mteja wa TTCL kufurahiya mawasiliano nafuu ya huduma ya maongezi, inatenti pamoja na ujumbe mfupi (SMS).

Huduma hiyo imezinguliwa leo jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Bodi ya T-PESA, Brigedia Generali mstaafu, Ramadhan Kimweri huku akisisitiza kuwa bidhaa hiyo imebuniwa kwa lengo la kuendelea kurahisisha huduma kwa wananchi kwa bei nafuu zaidi. Aidha aliwaomba Watanzania na wateja kwa ujumla kuendelea kutumia huduma za T-PESA ikiwa ni pamoja na kufurahiya mawasiliano ya huduma mpya ya Bando la TamTam.

“...T-PESA inawaletea huduma bora ya kipekee kabisa ya BANDO ambalo ni NAFUU na lenye MVUTO wa aina yake kwa watumiaji. Wananchi watapata fursa ya kupata huduma kwa siku, wiki na mwezi ikiwa na muda wa maongezi, huduma ya Inatenti na ujumbe mfupi (SMS),” alisema Bw. Kimweri.

Awali akifafanua juu ya huduma ya Bando Tam Tam la T-PESA, Afisa Mkuu wa T-Pesa, Bi. Lulu Mkudde alisema huduma hiyo itakuwa na virushi vya aina tatu, ambayo ni pamoja Kifurushi cha Siku, ambacho kinampa mteja MB 500 za kutumia intaneti, SMS 50 na dakika 5 za kupiga simu mitandao yote kwa masaa 24 kwa shilingi 500 tu.

Alibainisha kuwa Kifurushi cha pili cha Wiki, ambacho kinampa mteja GB 1 ya kutumia intaneti, SMS 100 na dakika 5 za kupiga simu mitandao yote kwa siku 7 za wiki kwa shilingi 1000, huku akikitaja Kifurushi cha tatu cha Mwezi, ambacho kinampa mteja GB 2 za kutumia intaneti, SMS 300 na dakika 20 za kupiga simu mitandao yote kwa siku 30,kwa shilingi 5000 tu.

Aidha alibainisha kuwa ili kuendelea kuboresha huduma za T-PESA, kampuni imeendelea kusajili mawakala nchi nzima hadi kufikia sasa T-PESA inamawakala wanaozidi zaidi ya 19,000 nchi nzima, uwepo wa mawakala hao wamechangia katika kufikisha huduma za kifedha katika maeneo mbalimbali nchini.

“... T-PESA imekuwa miongoni mwa kampuni zenye gharama nafuu za miamala kulinganisha na watoa huduma wengine. Hivyo watanzania wanahaki ya kujivunia zaidi na kutuunga mkono zaidi kwa kutumuia huduma zetu za T-PESA.” Alisisitiza.

“...Vifurushi hivi vinapatikana kwa mteja wa T-PESA. Jinsi ya kujiunga ni rahisi, mteja anatakiwa kupiga*150*71#. kuchagua namba 3 kununua Muda wa Maongezi au Vifurushi, halafu namba 2 kununua Vifurushi, kisha kuchagua namba 1 Bando Tam Tam.”


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2NrhAvt
via
logoblog

Thanks for reading T-PESA WAZINDUWA BANDO LA TAMTAM

Previous
« Prev Post