SERIKALI YAOMBWA KUBORESHA MIFUMO YA MAJI KATIKA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI

  Masama Blog      
Mwakilishi Mkazi Msaidizi wa UNICEF, Reve Van Dongen akizungumza wakati wa semina ya waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuhusiana na sherehe za kusheherekea Miaka 30 taku kuwepo na sheria ya haki za mtoto zilizosainiwa na nchi zote duniani kwaajili ya kulinda haki za mtoto.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano UNICEF, Usia Nkoma akizungumza na wahariri wa vyombo vya habari jijini Dar es Salaam, kuhusiana na sheria ya haki za mtoto kutimiza miaka 30 na jinsi inavyotekelezwa hapa nchini pamoja na kuelezea mtoto ni nani katika sheria hiyo ya mtoto.
 Katibu wa TEF, Neville Meena akisaini makualiano kati ya UNICEF na wahariri kuandika habari za watoto wakati wa semina iliyotolewa na UNICEF jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya wahariri wakiwa katika semina iliyotolewa na UNICEF.
 Mwakilishi wa agenda za watoto na vijana, Tahseen Alam akizungumza na wahariri wa vyomo vya habari jijini Dar es Salaam kuhusiana na Miaka 30 ya sheria ya haki za Mtoto (CRC).
Wadau wa watoto wakisikiliza mada.
Mwakilishi wa Agenda za ulinzi wa mtoto, Geofrey Machemba akizungumza na wahariri ni jinsi gani mtoto anaweza akalindwa.

TAKWIMU zinaonyesha asilimia 46 ya shule za msingi na shule za sekondari zina huduma ya maji ambayo yanamwezesha mtoto wa kike kujisitiri wakati wa hedhi, na asilimia 54 za shule hizo hazina huduma ya maji.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam wakati wa semina ya wahariri wa vyombo vya habari mbalimbali nchini, Mwakilishi kutoka Femina, Rose mweleka, alisema kuwa anaiomba serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuboresha huduma ya maji katika shule ili kila mtoto afurahie haki ya kupata elimu akiwa shuleni.

Hata hivyo Rose amesema kuwa kwa mtoto wa kike ambaye amefikisha umri wa kupata hedhi anahitaji maji akiwa shule ili aweze kujisitiri akiwa shuleni kwa siku nne hadi saba mbazo atakuwa katika kipindi cha hedhi ili asiweze kukosa masomo.

Rose ameshauri pia jamii iweze kutunza vyanzo vya maji, kwani utunzaji huo utawezesha kuwa maji safi na salama kwa matumizi.

Ikiwa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto UNICEF linasheherekea miaka 30 ya kusainiwa kwa sheria ya haki za mtoto (CRC) hapa nchini ambayo inazungumzia hasa haki ya mtoto, jinsi ya kutekeleza haki za mtoto na inayoelezea haki za mtoto ni zipi.

Hata hivyo Mwakilishi Mkazi Msaidizi wa UNICEF, Reve Van Dongen, alitolea mkazo katika sheria ya Mtoto ya haki ya kusikilizwa kwa mtoto ambayo wazazi kwa maeneo mengi ya Tanzania hawaitimizi haki hiyo ya kumsikiliza mtoto, hii imejitokeza katika mchakato wa ukusanyaji wa  aoni ya watoto kwa kufikia miaka 30 sheria ya Haki za Mtoto.

Nae Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa UNICEF, Usia Nkoma alisema kuwa Sheria ya Haki za Mtoto kifungu 1 hadi 41 inaelezea haki za Mtoto na kufafanua mtoto ni nani, kifungu cha kuanzia 42 hadi 54 zinaelezea namna ya kutekeleza haki za mtoto.

Usia alisema kuwa haki za mtoto lazima zizingatiwe ili kila mtoto aone yupo salama mahari alipo licha ya baadhi ya watoto waliohojiwa katika ukusanyaji wa maoni kuhusu mahali wanapoona wapo salama kuwa ni Nyumbani, ingawa bado kunawatoto wanyanyaswa na kufanyiwa vitendo vya kikatili nyumbani.

Hata hivyo vituo vya afya 68 vinahuduma ya maji katika maeneo mbalimblia nchini hii inaonyesha ni asilimia 32 pekee ya vituo vya afya hapa nchini havina huduma ya maji yanayokidhi mahitaji katika vituo hivyo.


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2WlDQv6
via
logoblog

Thanks for reading SERIKALI YAOMBWA KUBORESHA MIFUMO YA MAJI KATIKA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI

Previous
« Prev Post