Ticker

10/recent/ticker-posts

SBL yawekeza Paundi Mil 10 kupanua uzalishaji wake Dar, Moshi

Kampuni inayoongoza kwa uzalishaji wa bia nchini, Serengeti Breweries Limited (SBL) imetangaza mpango wake wa upanuzi wenye thamani ya paundi milioni 10 kwa viwanda vyake vya Dar es salaam na Moshi. 

Uwekezaji huo unapelekea kampuni hiyo kuongeza uwezo wake wa uzalishaji wa bia na hivyo kukidhi mahitaji ya wateja wa bidhaa zake yanayoongeza kila siku. 

Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mtendaji wa SBL, Mark Ocitti, kazi ya upanuzi tayari imeshaanza Dar es salaam, ambalo ni tawi la kwanza la uzalishaji kati ya matatu lililoanzishwa mwaka 1996. Matawi mengine ya uzalishaji ni Moshi na Mwanza 

"Upanuzi huu haumaanishi tu kupata uwezo wa ziada wa uzalishaji wa bia kwa sisi (SBL), lakini pia unaongeza fursa zaidi za ajira kwa watanzania na kuongeza uhitaji zaidi wa shayiri, mahindi na mtama ambavyo kampuni hununua kutoka kwa wakulima wa ndani," Mkurugenzi Mkuu huyo anasema. 

SBL kwa sasa imeajiri wafanyikazi wa moja kwa moja zaidi ya 800 na wengine katika viwanda vyake. Kuna maelfu ya wanufaika wengine wakiwamo wasambazaji, wasafirishaji, wakulima, wamiliki wa baa na wafanyikazi ambao hutegemea bidhaa za kampuni hiyon kama chanzo cha mapato. 

Kampuni hiyo hutegemea vyanzo vya ndani vya shayiri, mahindi na mtama kwa uzalishaji wake wa bia. Mkurugenzi huyo anafafanua kuwa, hadi kufikia mwishoni wa mwaka jana, kampuni yake ilichukua nafaka za ndani hadi kufikia tani 15,000, ambayo ni sawa na asilimia 60 ya mahitaji kamili ya malighafi ya SBL kwa uzalishaji wa bia kwa mwaka. 

SBL ina bidhaa nyingi zinazouzika na zina ubora wa hali juu kwa jina lake. Chapa yake kuu ya Serengeti Premium Lager imekuwa bia ya kwanza nchini Tanzania kufanywa kuwa malt kwa asilimia 100. Hivi karibuni SBL ilizindua bidhaa yake nyingine ya Serengeti Premium Lite, ambayo ni ya kwanza nchini Tanzania iliyoingizwa sokoni mwaka wa 2017. 

"Wateja wetu walionesha uhitaji wa bia halisi ya kitanzania na ndio maana tulizindua Serengeti Premium Lite miaka miwili iliyopita. Watanzania wameipokea vyema bidhaa hii mpya ambayo imekuwa ikifanya vizuri katika soko, "Ocitti anasema na kuwashukuru wateja kwa kuunga mkono chapa hiyo. 

Utafiti uliofanywa na Kampuni ya Deloitte mwaka 2018 juu ya uchangiaji wa SBL kwenye uchumi wa Tanzania ulionyesha kuwa, SBL ilichangia thamani ya shilingi bilioni 567 katika uchumi wa Tanzania kwa mwaka jana. Hii ni sawa na asilimia moja ya uchangia kwenye pato la taifa kwa bidhaa za ndani (GDP) ) ambalo kwa sasa linakadiriwa kufikia dola bilioni 55, karibia sawa na shilingi trilioni 127. 

SBL ilianzishwa na wajasiriamali wachache wa Kitanzania mwaka 1996 na kiwanda kimoja ambacho kilijengwa jijini Dar es salaam. Kati ya mwaka 2010 na 2013 muundo wa umiliki wa kampuni ulibadilika na kuja na bodi ya kampuni kubwa ya bia ya East Africa Breweries Limited (EABL), mtayarishaji wa vinywaji duniani, Diageo, ambao wamechangia ongezeko la uwekezaji zaidi kwa kufungua viunga vikuu viwili vya nyongeza vya uzalishaji katika Jiji la Mwanza na Moshi. 

Hadi sasa, kampuni imepanua wigo kwa kuzalisha bidhaa za bia zinazoongoza kama vile Pilsner Lager, Tusker Lager, Guinness na Senator Of Late - Serengeti Premium Lite. 

Halikadhalika, SBL pia inasambaza katika soko la Tanzania bidhaa zingine za kwanza za Diageo za Kimataifa kama vile Johnnie Walker, Gordons, Smirnoff Black ICE na zingininezo.



from MICHUZI BLOG https://ift.tt/33nwaL4
via

Post a Comment

0 Comments