Ticker

10/recent/ticker-posts

RC SINGIDA AFUNGUA MAONESHO YA SIKU YA CHAKULA DUNIANI


 Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt.Rehema Nchimbi ambaye alikuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa maonesho ya maadhimisho ya siku ya chakula duniani ambayo kitaifa yanafanyika mkoani hapa.
 Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Dkt.Bedan Masuruli akimkaribisha Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt.Rehema Nchimbi katika banda la wizara hiyo kwenye maonesho hayo.
 Afisa Mifugo Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Mary Yongolo (kushoto) akimpa zawadi ya maziwa Dkt.Rehema Nchimbi baada ya kutembelea banda la Kampuni ya Tanga Fresh. Kulia ni Kaimu 
Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo na Mifugo, Dkt. Bedan Masuruli.
 Mtafiti wa Zao la Maharage kutoka Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI) Arusha Edith Kadege akimuelekeza Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dkt.Rehema Nchimbi kuhusu maharage lishe yaliyofanyiwa utafiti na kituo hicho.
 Afisa Mtendaji Mkuu (CEO)  wa Taasisi ya Promised Eden Environmental care (PEEC) Ascarlyon Lufurano (kushoto) akimuelekeza Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dkt.Rehema Nchimbi kuhusu kilimo cha mapapai yanayo zalishwa na Taasisi  hiyo.
 Afisa Kilimo Mkuu Wizara ya Kilimo Dodoma, Deograsias Ruzangi, akitoa maelezo mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Singida kuhusu machapisho mbalimbali yanayohusu kilimo na uvuvi.
 Wanakwaya ya Kanisa la AICT mkoani Singida wakitoa burudani.
 Hafla ya ufunguzi maonesho hayo ikiendelea.
 Hafla ya ufunguzi maonesho hayo ikiendelea.
 Msanii wa muziki wa Sengeli Mzee wa Bwax akipagawisha katika hafla hiyo.
 Meya wa Manispaa ya Singida, Alhaji Chima Mbuwa akizungumza katika mkutano huo.
 Taswira ya mkutano huo.
 Wasanii wa kikundi cha Mbaramwezi wakitoa burudani.
 Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Honest Kessy akizungumza.
 Wasanii kutoka Singida Mjini wakitumbuiza.



Afisa Masoko wa Kampuni ya Hughes Agricultural (T) Ltd, Lawrence Kisoka akizungumzia 
ubora wa matrekta aina ya New Holland Agriculture yanayosambazwa na kampuni hiyo.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt.Rehema Nchimbi akiwa katika picha ya pamoja na viongozi 
Mkurugenzi wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Mikalu Mapunda akizungumza na Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Mwenge waliotembelea banda la NFRA.
Afasa Manunuzi na Ugavi Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko ( CPB) akizungumza na Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Mwenge waliotembelea banda la bodi hiyo.


Dotto Mwaibale na Boniphace Jilili Singida. 

HALMASHAURI za mkoa wa Singida zimetakiwa kuviwezesha kupata pembejeo bora za kilimo vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu kupitia asilimia kumi zinazotengwa na 
halmashauri kote nchini kwa ajili ya makundi hayo. 

Agizo hilo lilitolewa juzi na Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi wakati akifungua rasmi maonesho ya kitaifa Mkoani humo ya maadhimisho ya siku ya Chakula duniani.

Alisema zile asilimia kumi zinazotengwa na halmashauri kwa ajili ya kuvisaidia vikundi vya akinamama,vijana na watu wenye ulemavu ni vyema halmashauri zikawatafutia matrekta 
kwa kuwakopesha ili kuinua kwa haraka kipato chao.

Hata hivyo alisema kupitia elimu inayoendelea kutolewa kwenye maonesho hayo viongozi waichukue na kuwapelekea wananchi kwenye maeneo yao,huku akiziagiza halmashauri za wilaya 
za mkoa huo kutenga maeneo kwa ajili ya malisho, na kuziagiza kila shule za mkoa huo kutenga nusu hekari ili kulima maharage yatakayo tumika kutengenezea uji wa lishe kwa ajili ya wanafunzi.

Dkt Nchimbi alisema taifa lolote lililo simama imara watu wake wana lishe bora na hivyo ili kufikia uchumi wa kati wa Tanzania ya Viwanda ni lazima watu wawe na lishe bora.

Aidha kaimu katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi Dkt Berdan Nasuruli alisema ujumbe wa Wizara ni kutaka raslimali nyingi ilizonazo Tanzania ziwasaidie wananchi kupata lishe bora.

Amesema licha ya Tanzania kuwa ya pili barani afya kwa ufugaji wa ng'ombe lakini watu wake hawatumii maziwa,hivyo viongozi wahimize watu kunywa maziwa na kula Samaki ili kuwa na lishe bora,na maadhimisho hayo yatakuwa na maana endapo watu watabadilika kwa kuanza kutumia vyakula vyenye lishe bora. 

Naye kaimu katibu Mkuu Wizara ya kilimo Honest Kessy alisema maadhimisho hayo ni ya 39 tangu yalipoanza kuadhimishwa mwaka 1981,na kauli mbiu ya mwaka huu ni "Lishe bora kwa ulimwengu usio na njaa" ambapo mwaka huu kitaifa yanaadhimishwa mkoani hapa.

Kessy aliwataka wananchi wa mkoa huo na wote wanaoweza kufika kwenye maonesho hayo kutumia fursa hiyo kujifunza mambo mbalimbali yahusuyo lishe bora ili kuboresha afya zao kwa 
maendeleo yao na taifa kwa ujumla. 

Kwa upande wake Meneja wa Kampuni ya Tanga Fresh Mkoa wa Singida, Alfred Masawe aliwashauri wananchi kutumia Maziwa ya kampuni hiyo ambapo kuna Maziwa fresh, Maziwa mtindi, Loghurt,Cheese pamoja na Unsal



.


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2ppko3R
via

Post a Comment

0 Comments