Ticker

10/recent/ticker-posts

RC MAKONDA AWASILISHA TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA ILANI YA CCM, DKT. BASHIRU ATOA NENO

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi CCM Taifa Dkt. Bashiru Ally akizungumza katika mkutano wa viongozi wa CCM ngazi zote mkoa wa Dar es salaam uliofanyika kwenye uwanja wa Uhuru.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makondaakizungumza katika mkutano wa viongozi wa Chama Cha Mapinduzi mkoa wa Dar es salaam ngazi zote uliofanyika kwenye uwanja wa Uhuru leo.
Baadhi ya viongozi wa Chama Cha Mapinduzi Ngazi zote mkoa wa Dar es salaam wakiwa katika mkutano huo uliofanyika kwenye uwanja wa Uhuru.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda akizunguza na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es salaam Mama Kate Kamba.
Katibu Mkuu wa CCM Dkt. Bashiru Ali akizungumza jambo na Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mh. Paul Makonda.

 


 
 
 
…………………………………………

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda leo October 05 amewasilisha kwa Viongozi wa Chama cha Mapinduzi CCM kuanzia ngazi ya Taifa, Mkoa,Wilaya, Kata na Mashina taarifa ya miradi ya maendeleo inayotekelezwa na Serikali ya awamu ya Tano kwenye Mkoa huo kwa mwaka 2019 ikiwa ni sehemu ya Utekekelezaji wa Ilani ya CCM inayolenga kutatua kero za Wananchi.

RC Makonda amesema miongoni mwa miradi inayotekelezwa kwenye mkoa huo ni Ujenzi wa Barabara chini ya TANROAD, TARURA na DMDP zenye urefu wa Km 5,153, Ujenzi wa Miundombinu ya upatikanaji wa Maji, Ujenzi wa Mejengo ya Hospital, Vituo vya Afya, Zahanati na Vifaa Tiba ambavyo vimesaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza changamoto kwa wananchi.

Aidha RC Makonda ameitaja miradi mingine inayotekelezwa ni sekta ya Elimu kupitia ujenzi wa Vyumba vya madarasa, ofisi za walimu na matundu ya Vyoo, Sekta ya Nishati ya Umeme, Ujenzi wa Viwanda, Sekta ya Ardhi, Usafiri pamoja na suala la Ulinzi na usalama.

Kwa Upande wake katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi CCM Taifa Dkt. Bashiru Ally amepongeza mkoa wa Dar es salaam kwa kazi kubwa na nzuri ya kuwaonyesha wananchi kwa vitendo kile kinachofanywa na Serikali yao ya Awamu ya tano chini ya Rais Dkt. John Magufuli.

Aidha Dkt. Bashiru amepongeza Mkoa huo kwa kuwa kinara wa kusimamia makusanyo ya kodi, kusimamia kikamilifu suala la ulinzi na usalama, kusimamia Usafi wa Mazingira pamoja na kuwa na utamaduni mzuri wa kushirikiana na Wasanii na vyombo vya habari.


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2oUWYDv
via

Post a Comment

0 Comments