Ticker

10/recent/ticker-posts

RAIS MAGUFULI KUUWEKA MKOA WA KATAVI CHINI YA UANGALIZI WA JWTZ

Rais John Magufuli ameuweka Mkoa wa Katavi chini ya uangalizi wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), kutokana na kukithiri kwa vitendo vya uhalifu na ujambazi, vinavyohusishwa na wakimbizi.

Amesema kuna baadhi ya wakimbizi ambao wameficha silaha kwenye vichaka hivyo serikali inafuatilia kwa karibu ili kuwanasa wakaonyeshe walikowauzia.

Rais Magufuli aliyasema hayo jana akiwa katika Wilaya ya Tanganyika, mkoani Katavi, wakati akizindua kipande cha barabara ya Mpanda – Uvinza iliyojejwa kwa kiwango cha lami.

Aliagiza JWTZ kupitia Brigedi ya 201 ya Tabora kutekeleza jambo hilo huku akisisitiza kuwa nchi haiwezi kuchezewa na mtu yeyote.

"Kwa hiyo Jeshi la Wananchi Tanzania mpeleke base pale. Brigedi ya 201 ya Tabora ndiyo watakuwa wanahudumia hapa kwa sababu ni karibu. Nchi hii haiwezi kuchezewa na mtu yeyote. Kama kuna mkimbizi anafikiri anaweza kuichezea amepotea, tunahitaji upendo wa kweli mambo ya kui-beep Tanzania hayapo.

"Wapo walioishi miaka mingi, wapo waliopewa uraia na wapo wachache wameanza kuharibu sifa za ukimbizi kwa kujihusisha na ujambazi," alisema

Aidha, aliongeza kuwa kumekuwa na matukio ya uhalifu wa maliasili katika msitu wa Tongwe na kwamba baadhi ya wakimbizi wanaoaminika kuwa na silaha wamekuwa wakihusishwa.

"Waache tabia hiyo mara moja wamekimbia kule kutokana na migogoro waliyoisababisha wao. Ukija hapa kaa utulie, hapa si mahali pa kuleta migogoro na ukikimbilia taifa lingine kaa utulie usijifanye unajua,"alisema.



Pia alisema serikali haina matatizo na wakimbizi ambao ni watulivu kwa kuwa nchi inawapokea kwa maslahi mapana lakini wanapowashambulia wakulima wakiwa shambani, kuvamia mabasi na kupora abiria serikali lazima iingilie kati.


from CCM Blog https://ift.tt/2MxUYsZ
via

Post a Comment

0 Comments