Ticker

10/recent/ticker-posts

PINDA AMWAGIA SIFA SERIKALI YA AWAMU YA TANO UTEKELEZAJI MIRADI MIKUBWA YA MAENDELEO YA KUAKISI UCHUMI WA VIWANDA

Waziri Mkuu Mstaafu wa Mizengo Pinda akizungumza wakati wa kufunga maonesho ya wiki ya Viwanda vya Mkoa wa Pwani yaliyokuwa yakifanyika katika viwanja vya ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani , Mjini Kibaha.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo akizungumza namna walibyoweka mazingira ya uwekezaji wa viwanda katika mkoa katika maonesho ya viwanda vya Mkoa wa Pwani yaliyokuwa yakifanyika katika viwanja vya ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mjini Kibaha.
Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda akimkabidhi Tuzo mmoja wa wadhamini ya maonesho ya wiki ya viwanda mkoa wa Pwani Mkuu wa Kanda ya Mashariki wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA)Mhandisi Lawi Odiero.
Mkuu wa Kanda ya Mashariki wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA)Mhandisi Lawi Odiero akiwa na watendaji wa kanda hiyo kwa pamoja wakifurahia tuzo walioipata katika maonesho ya wiki ya Viwanda vya Mkoa wa Pwani yaliyokuwa yakifanyika katika viwanja vya ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani ,Mjini Kibaha.
Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda akitoa maelezo katika Banda huduma za pamoja katika Ofisi ya Mkemia mkuu wa Serikali maonesho ya wiki ya Viwanda vya Mkoa wa Pwani yaliyokuwa yakifanyika katika viwanja vya ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani ,Mjini Kibaha.
Mgeni Rasmi Waziri Mkuu, Mstaafu Mizengo Pinda akiwa katika picha ya pamoja na wadhamini wa maonesho ya wiki ya viwanda mkoa.

Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
WAZIRI Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda amesifu Serikali ya awamu ya tano kwakuendelea kutekeleza mpango wa maendeleo wa Taifa wa mwaka 2016 /2021 kwa kukuza uchumi wa viwanda hali ambayo itafanya wananchi kuondokana nan a umasikini kutokana na viwanda hivyo kutumia malighafi zilizopo nchini.

Waziri Mkuu Mstaafu Pinda aliyasema hayo wakati akifunga maonesho ya bidhaa za viwandani vilivyoko Mkoa wa Pwani yaliyokuwa yakifanyika katika viwanja vya Mkuu wa Mkoa wa Pwani ,Kibaha Mjini.

Amesema, moja ya mpango huo ni ujenzi wa reli ya mwendokasi kutoka Dar es Salaam- Morogoro na makutopora na kwamba kukamilika kwake itakuwa na mchango mkubwa kwa Taifa ambapo mkoa wa Pwani utakuwa umepata fursa kubwa itakayokuwa inawasaidia wawekezaji wake katika kufanya biashara kutokana na mnyororo wa usafiirishaji.

Pinda amesema uwepo wa Shirika la Ndege la Tanzania(ATCL) kwa kuwa na ndege mchango wake mkubwa kwa faida ya maendeleo ya Taifa na kuiingizia nchi fedha za kigeni kutokana na wafanyabiashara wengi kuja nchini kwa ajili ya uwekezaji pamoja na fursa za utalii.

" Baadhi ya watu walikuwa wanasema maneno ya hovyo sana,mara vindenge vyenyewe vidogo,havijazi watu na maneno mengine mengi ya kubeza juhudi hizo lakini sasa hivi watu wanaruka moja kwa moja kutoka India kwa ndege hizohizo kwahiyo lazima tukubali matokeo,"alisema Pinda
Mbali na miradi lakini alisema Rais Magufuli ,anajenga mradi wa kufua umeme wa Mwalimu Nyerere huko Rufiji Mkoani Pwani ambao kukamilika kwake utakuwa na uwezo wa kufua umeme zaidi ya megawati 2000 ambao utasaidia kuboresha mazingira ya uendeshaji kwa wamiliki wa viwanda nchini.

Alisema kuwa,mradi huo wa umeme ulibuniwa miaka mingi ya nyuma tangu enzi za Mwalimu Julius Kambarage Nyerere lakini Rais Magufuli amefanikiwa na sasa anajenga kwa fedha nyingi kwahiyo lazima watu wakubali matokeo hayo ya maendeleo na ikiwezekana waunge mkono juhudi za Serikali.

Hatahivyo,Pinda alizipongeza taasisi wezeshi kwa namna zilivyojipanga kuendeleza shughuli za uwekezaji wa viwanda hapa nchini kwakuwa jambo hilo litasaidia kuimarisha uchumi wa nchi.

Mkuu wa Mkoa wa Pwani Evarist Ndikilo ,alisema chimbuko la maonesho hayo limetokana na wamiliki wa viwanda kuonyesha changamoto za ukosefu wa masoko kupitia bidhaa wanazozalisha na hata kutofahamika kwa Wananchi.

Ndikilo,alisema malengo mahususi ni kutangaza bidhaa zinazozalishwa na viwanda vya mkoa wa Pwani pamoja na kusaidia kutafuta masoko kwa bidhaa hizo na kwamba mpaka maonesho hayo yanakamilika zaidi ya watu 10,000 wametembelea.

Alisema kuwa,kupitia maonesho hayo wawekezaji wamepata masoko mbalimbali na hata baadhi ya wananchi wamenufaika kwa kutambua bidhaa mbalimbali zinazopatikana mkoa wa Pwani huku akisema kupitia kauli mbiu ya ujenzi wa viwanda mkoa umetenga zaidi ya ekari 53,000 kwa ajili ya wawekezaji.

Ndikilo,aliongeza kuwa juhudi nyingine ni kuendelea kuwavutia wawekezaji zaidi pamoja na kushirikiana na taasisi wezeshi ili waweze kuona namna ya kufikia malengo ya uchumi wa kati kupitia ujenzi wa viwanda.


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/31J4VJm
via

Post a Comment

0 Comments