Ticker

10/recent/ticker-posts

OKTOBA 13, SIKU YA KUPUNGUZA MAAFA DUNIANI, BILIONI 30 ZATUMIKA KUREJESHA HALI MKOANI KAGERA

Anaandika Abdullatif Yunus - Michuzi TV.
Oktoba 13 kila Mwaka Dunia huadhimisha Siku ya Kimataifa ya Kupunguza Maafa ambayo husababishwa na majanga mbalimbali na kupelekea athari vikiwemo vifo katika jamii husika.

Kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa na Katibu Tawala Mkoa wa Kagera Profesa Faustine Kamuzora, wakati akizungumza na waandishi wa Habari Ofisini kwake ameeleza kuwa kwa kipindi cha takribani miaka mitatu iliyopita Mkoa wa Kagera umekuwa ukipitia katika majanga tofauti likiwemo Tetemeko, Mvua, Radi, moto, yaliyopelekea maafa makubwa, ambapo athari zake ni pamoja Vifo, uharibifu wa miundo mbinu, majengo n.k.

Profesa Kamuzora ameongeza kuwa Kufuatia maafa hayo Serikali imekuwa ikijitahidi kurejesha hali ambapo zaidi ya shilingi Bilioni 30 zimekwisha tumika Kwa kukarabati majengo ya Taasisi, Ujenzi wa Shule Mpya, miundo mbinu ya Barabara na huku elimu ikizidi kutolewa zaidi namna ya kukabiliana na maafa pindi yanapojitokeza, na tayari ipo kamati ya maafa inayohusisha Serikali, Taasisi binafsi na watu binafsi, ambapo pamoja na mambo mengine kamati hiyo ndiyo inasimamia Urejeshaji wa hali kwa kusimamia ujenzi bora wa majengo

Kauli mbiu ya Siku hii Mwaka huu ni, "Chukua hatua endelevu kuounguza uharibifu wa maafa katika miundo mbinu muhimu na huduma za msingi ikiwemo afya na elimu, pamoja na kuimarisha ustahimilivu wake ifikapo 2030" wakati Kitaifa Siku hii inaadhimishwa katika Viwanja vya Nyerere Square Jijini Dodoma.


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2Ba5dhU
via

Post a Comment

0 Comments