Ticker

10/recent/ticker-posts

NDITIYE: WANANCHI MKIWASILIANA SERIKALI TUNAPATA HELA

Prisca Ulomi, Geita

Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye yuko ziarani mkoani Geita kukagua upatikanaji wa huduma za mawasiliano, kuhamasisha wananchikusajili laini za simu kwa njia ya alama ya vidole kwa kutumia kitambulisho cha taifa chaNIDA na kufuatilia utekelezaji wa mpango wa anwani za makazi na postikodi mkoanihumo.

Wakati akiwa kwenye ofisi ya Mkuu wa Wilaya wa Mbogwe, Nditiye amesema kuwamalengo ya Serikali ni kuhakikisha kuwa wananchi wanawasiliana, huduma zamawasiliano zinakuwa zenye ubora unaotakiwa, za uhakika na kunakuwa na usikivumzuri wa mawasiliano kwa kuwa Serikali inataka wananchi wawasiliane.

“Serikali tunataka wananchi wawasiliane kwa kuwa wakiwasiliana tunapata mapatoambayo yanaendesha shughuli mbali mbali za kuhudumia wananchi,” amesema Nditiye.Mkuu wa Wilaya ya Mbogwe, Martha Mkupasi amemweleza Nditiye kuwa wanashida yamawasiliano kwenye wilaya yao na mara nyingine wanakwama kukusanya mapato yaSerikali hivyo inawapa changamoto katika kuwatumikia wananchi na utekelezaji wamajukumu ya kila siku ya Serikali.

“tunashida ya mawasiliano kwenye wilaya yetu na mara nyingine tunakwama hata kukusanya mapato na kupeana taarifa za ulinzi na usalama hasa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi,” amefafanua Mkupasi.

Nditiye amemweleza kuwa amekagua upatikanaji wa huduma za mawasiliano wilayani humo na amegundua kuwa Wilaya ya Mbogwe inapata mawasiliano kwa kiwango cha asilimia 90 na ina mitandao mingine ya mawasiliano ila wananchi wanaonekana wanapenda mtandao wa Vodacom.

Naye Mbunge wa Mbogwe, Agostino Maselle amekiri kuwa wanapata huduma zamawasiliano za mitandao mingine ya TTCL, tigo, halotel, airtel na yote iko vizuri ila mtandao wa Vodacom unasumbua na huduma za m-pesa kwenye kata ya Ilolangulu, Itobe na Isesya.

Akizungumza kwa niaba ya wananchi wakati wa mkutano wa hadhara kwenye Kata ya Ilolangulu, mkazi wa kata hiyo Daniel Mishigitu amemweleza Nditiye kuwa wanapata kero ya mawasiliano ya Vodacom na wakitumiwa hela inakaa muda mrefu kwenye mtandao. Naye Vedastus Rwechungura amemshukuru Nditiye kwa kufika na kusikiliza shida ya mtandao huo na mzunguko wanaoupata wakitaka kutoa pesa ambapo mara nyingine wanalazimika kusafiri kwenda Ushirombo.

Akijibu malalamiko ya wananchi, Nditiye amewaeleza kuwa amegundua kuwa kuna mzunguko wa hela kwenye kata hiyo na uchumi wa wananchi uko vizuri, hivyo ameielekeza kampuni ya Vodacom kuwa ndani ya muda wa miezi sita mnara uwepo ili wananchi waweze kuwasiliana, kutuma na kupokea pesa kwa kuwa lengo la Serikali ni kuhakikisha wananchi wanawasiliana na wakiwasiliana inapata mapato.

Nditiye amefanunua kuwa sehemu inapokuwa na mawasiliano ya kampuni mojainatosha na sio lazima kuwa na mitandao yote ila kwa kuzingatia kuwa wananchi wamehitaji mtandao huo hivyo UCSAF kwa kushirikiana na Vodacom ihakikishe kuwa mnara huo unajengwa na TCRA wafuatilie na kusimamia jambo hilo.

Katika ziara hiyo, Nditiye ameambatana na wataalam kutoka wizarani kwake Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania na watoa huduma wa kampuni ya Vodacom
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye akitoa
maelekezo kwa Mhandisi wa Vodacom, Benedict Mara (wa kwanza kulia) kuhakikisha mawasiliano yanapatikana muda wote Kata ya Ilolangulu wakati wa zaiara yake ya kukagua upatikanaji wa hudumaza mawasiliano wilayani Mbogwe, Geita.
Mkuu wa uendeshaji wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote, Mhandisi Albert Richard akitoa taarifa kwa Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye (wa kwanza kushoto) kuhusu mnara wa Ilolangulu wakati wa ziara yake ya kukagua upatikanaji wa mawasiliano Mbogwe mkoani Geita.
Mbunge wa jimbo la Mbogwe, Agostino Masele akimuonesha Naibu Waziri wa
Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye vijiji ambavyo havina
mawasiliano ya uhakika wakati wa ziara yake ya kukagua upatikanaji wa mawasiliano wilayani Mbogwe mkoani Geita.
Mkuu wa Wilaya ya Mbogwe, Martha Mkupasi akitoa taarifa ya hali ya mawasiliano kwa Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye wakati wa ziara yake wilayani humo ya kukagua upatikanaji wa huduma za mawasiliano.


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2onpVYL
via

Post a Comment

0 Comments