Ticker

10/recent/ticker-posts

NAIBU WAZIRI MABULA AWATAKA WANANCHI KUCHANGAMKIA ZOEZI LA URASIMISHAJI

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi ambaye ni Mbunge wa jimbo la Ilemela Dkt Angeline Mabula akizungumza na wananchi wa Mtaa wa Kabangaja kata ya Bugogwa mkoa wa Mwanza wakati wa ziara yake ya kukagua utendaji kazi katika sekta ya ardhi katika mikoa ya Kanda ya Ziwa jana.

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi ambaye ni Mbunge wa jimbo la Ilemela Dkt Angeline Mabula akiwa na wananchi wa Mtaa wa Kabangaja kata ya Bugogwa mkoa wa Mwanza wakati wa ziara yake ya kukagua utendaji kazi katika sekta ya ardhi katika mikoa ya Kanda ya Ziwa jana.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi ambaye ni Mbunge wa jimbo la Ilemela Dkt Angeline Mabula akiwa amemshika Mbuzi kabla ya kukabidhi kwa mshindi wa kwanza wa mashindano ya MAGA NDONDO CUP ambapo timu ya Warrious iliibuka mshindi wa mashindano hayo kwa kuifunga timu ya Best kwa mikwaju ya penati 3-1.

…………………….

Na Munir Shemweta, WANMM ILEMELA

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula amewataka wananchi kuchangamkia zoezi la urasimishaji linaloendelea nchini ili waweze kuwa na umiliki halali wa ardhi yao watakayoweza kuitumia kujiletea maendeleo.

Dkt Mabula ambaye ni Mbunge la Ilemela mkoani Mwanza alitoa kauli hiyo mwishoni mwa wiki alipozungumza na wananchi wa jimbo lake katika Mtaa wa Kabanganya kata ya Bugogwa wilaya ya Ilemela mkoa wa Mwanza akiwa katika ziara yake ya kukagua utendaji kazi wa sekta ya ardhi katika Kanda ya Ziwa.

Alisema, Rais wa Jamhuri ya Muungano John Pombe Magufuli ameelekeza maeneo yote yaliyokuwa katika ujenzi holela yarasimishwe kwa kupimwa ili wananchi wake wawe na umiliki halali kwa kuwa walitumia nguvu nyingi wakati wa kuyaendeleza.

Kwa mujibu wa Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, kupimiwa pekee katika maeneo yaliyorasimishwa hakutoshi na kushauri wananchi kuhakikisha wanapata hati za umiliki ili waweze kuzitumia katika kujipatia mikopo na shughuli nyingine za kimaendeleo.

‘’Wananchi walijenga kwa nguvu zao, serikali haikuwa makini katika kupanga maeneo ili watu wakae katika mpangilio mzuri hivyo Rais aliagiza wananchi warasimishiwe ili waweze kuwezeshwe kiuchumi na kutumia ardhi yao na majengo kuendelea katika shughuli za uchumi na kuweka dhamana na zoezi hili linafanyika kwa miaka kumi na kumalizika 2023’’ alisema Dkt Mabula.

Akizungumzia shughuli za maendeleo katika jimbo lake la Ilemela, Dkt Mabula alisema tangu achaguliwe kuwa Mbunge wa jimbo hilo amefanya mambo makubwa katika sekta ya elimu kwa kuwezesha ujenzi wa shule za msingi na sekondari sambamba na kuongeza vyumba vya madarasa kwa baadhi ya shule hizo tofauti na miaka ya nyuma.

from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2BbN0At
via

Post a Comment

0 Comments