Ticker

10/recent/ticker-posts

MWANARIADHA FARAJA DAMAS ATINGA FAINALI MASHINDANO YA MAJESHI YA DUNIA NCHINI CHINA, SIMBU AJIPANGA MARATHON

Mwanariadha Faraja Damas wa JWTZ Mwenye namba 1505 akichuana vikali na wanaridha kutoka mataifa Mbalimbali katika mashindano ya Dunia ya Majeshi yanayoendelea nchini China Faraja aliibuka mshindi wa kwanza na kuingia Fainali. (Picha na Luteni Selemani Semunyu).
Na Luteni Selemani Semunyu, China.

Mwanaridha kutoka Tanzania Faraja Damas amefuzu kuingia fainali ya Mita 5000 katika mashindano ya majeshi ya dunia yanayoendelea nchini  China huku akiwapita wanariadha wengine 24.

Faraja alishika nafasi ya kwanza baada ya kukimbia kwa dakika 14:39.24   huku akiwaacha nyuma wakimbiaji wengine katika kundi la pili la wakimbiaji waliokuwa wakisaka nafasi ya kuingia fainali.
Hata hivyo siku haikuwa Njema kwa mwanaridha Joseph Panga baada ya kushindwa kufuzu katika hatua ya Fainali baada ya kukimbia nafasi ya sita nyuma kwa dakika 14:10.47 katika kundi ambalo pia lilikuwa na wakimbiaji 24.

Katika kundi hilo Mkenya  Peter Ndegwa aliongoza baada ya kukimbia kwa dakika 14:04.67 na kufanikiwa kutinga fainali huku akiwa na kibarua cha kukabiliana na wanaridha wengine Tisa waliofuzu kwa Fainali.

Wanariadha hao wa mbio za Mita 5000 wanatarajia kuchuana Oktoba 26 ili kumpata mshindi wa kwanza wa pili na watatu watakaonyakua Medali. Wakati huo huo Mwanariadha Private Gisamoda Emannuel ameshika nafasi ya nne kati ya wanariadha 39 kutoka nchi 46 zilizoshiriki mbio za mita elfu kumi akitanguliwa na El aaraby Mohamed kutoka Moroko  aliyeshika nafani ya kwanza.

Petros  Amanal  wa Ujerumani akishika nafasi ya pili na tatu ikishikwa na  Sahli Hamza naye wa Moroko huku Mtanzania Mwingine Marco Sylvester aliyeshika nafasi ya sita. Mwanariadha Private  Magdalena Shauri aliyeshinda mashindano ya Majeshi Afrika Mashariki anatarajiwa kukimbi leo usiku  sambamba na katika fainali za mbio za Mita 5000 huku  wanariadha wa Marathoni wakiongozwa na Private Felix Simbu wakitarajiwa kukimbia tarehe 27.

Wakati huo huo bondia selemani kidunda ametolewa katika hatua ya robo fainali baada mpambano mkali ambapo  kidunda alipambana  muda wote na kumrushia mpinzani wake makonde mazito.
Hata hivyo mpaka mwisho wa Mpambano Kidunda alipata pointi 26 huku mpinzani wake Ghousoon Ahmad wa syria akipata pointi 30 na kutangazwa mshindi baada ya maamuzi ya majaji wote watano.


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/33Xi2Za
via

Post a Comment

0 Comments