MWAKYEMBE AWATAKA WASANII KUEPUKA MIKATABA FEKI

  Masama Blog      
     Na.Khadija seif, Michuzi TV

WAZIRI wa habarii, Utamaduni, Sanaa na Michezo nchini  Dk Harrison Mwakyembe amezindua rasmi awamu ya pili ya kamati ya kusimamia haki za wasanii.

Aidha, Mwakyembe amefafanua zaidi kuwa kamati hiyo ipo kwa ajili ya kusaidia wasanii na katika awamu ya Kwanza ya kamati hiyo imeweza kusaidia wasanii wenye malalamiko kwa kiasi kikubwa na kufanikisha kupata haki zao.

" Mama Kanumba,Marehemu mzee majuto Ni miongoni mwa watu ambao tuliweza kutatua matatizo yao ambapo baadhi ya makampuni yalikua yakilegalega kufanya malipo kwao,"

Pia amewataja wasanii kama Ay na Mwana Fa kuwa Ni miongoni mwa wasanii ambao kamati ilisaidia  wapate haki zao na kutokana na uvumilivu wao waliweza kupata jasho lao.

Hata hivyo Mwakyembe ametoa wito kwa wasanii ambao wanaingia mikataba bila kuweka wakili au wanasheria kuacha mara moja kwani wanajidhurumu jasho lao na kupelekea kudhurumiwa wao wenye.

"Wapo vijana 10 ambao walifanyishwa kazi na mtu asiejulikana na kukimbilia nchini kwao lakini tutafanya juu chini kuhakikisha tunamfikisha kwenye vyombo vya sheria kwani tunaamini wasanii wanapigana usiku na mchana kutafuta riziki na kuendesha maisha yao Kama kazi zingine,"

Kwa upande wake Mwanasheria katika kamati hiyo Dora  Mwenegoha amebainisha changamoto walizokumbana nazo wakati wa kutatua matatizo kwa awamu ya kwanza.

"Baadhi ya makampuni yalikua hayatoi  ushirikiano wakutosha katika kusuluhisho migorogoro na wasanii walioingia nao mikataba,"

Aidha, Mwenegoha amewapongeza makampuni Kama startimes kwa kutii agizo la Waziri Mwakyembe kwa kuwalipa stahiki zao wasanii ambao walikua wakidai haki  zao na kutaka makampuni mengine kutekeleza Jambo mara moja .
 Waziri wa habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe (kulia) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari wakati akizindua Kamati ya kusimamia haki za kazi za wasanii nchini mapema hii leo jijini Dar es Salaam, katikati ni Mwenyekiti wa kamati hiyo Bi. Sarah Nsangizyo Zilahulula na kushoto ni mjumbe Dkt. Dorah Mwenegoha
   Baadhi ya wajumbe wa kamati ya kusimamia haki za kazi za wasanii nchini wakimsikiliza Waziri wa habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe (hayupo pichani) wakati waziri alipokuwa akizindua kamati hiyo mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Kamati ya kusimamia haki za kazi za wasanii nchini mara baada ya kuizindua mapema hii leo jijini Dar es Salaam
from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2p5kG0h
via
logoblog

Thanks for reading MWAKYEMBE AWATAKA WASANII KUEPUKA MIKATABA FEKI

Previous
« Prev Post