MGOGORO WA KUGOMBEA MALI ZA MAREHEMU BILIONEA ERASTO MSUYA WAPATIWA UFUMBUZI

  Masama Blog      
Na Woinde Shizza,Arusha

Mgogoro wa kugombea mali wa Familia ya Marehemu Bilionea Erasto Msuya uliodumu kwa zaidi ya Miaka sita ,umepata ufumbuzi Mara baada ya upande mmoja kukubali kuondoa kesi ya Miradhi mahakama ili kujadili jambo hilo mezani.

Akiongea mbele ya Mkuu wa wilaya ya Arumeru ,Jerry Muro aliyekuwa akiongoza kikao cha familia hizo,ofisini kwake,mama wa marehemu,Ndeshu Msuya amesema kuwa wao kama wazazi wa marehemu wamekubali kuondoa kwa muda shauri hilo mahakamani ili kurejea meza ya mazungumzo.

Ameongeza kuwa wao kama wazazi hawana nia ya kupoka Mali za marehemu ila wanachopigania ni haki ya urithi wa Mali kwa watoto wanne walioachwa na marehemu Bilionea Erasto Msuya, ambazo hadi sasa hazijagawanywa huku ikidaiwa kuwanufaisha ndugu wa upande wa Mke wa marehemu.

"Nitakwenda mahakamani na mwanasheria wangu tukalitoe kwa muda jambo hilo na kurejea meza ya mazungumzo" Alisema mama Ndeshu

Awali mtoto mkubwa wa marehemu,aitwaye Kelvin Saimoni Msuya alisema kuwa yupo tayari kukaa meza moja ya mazungumzo na upande wa wazazi wa baba yake na kuwataka ndugu hao kuwa na upendo na mama yake anayesota Gerezani kwa kesi ya mauaji.

Katika kikao hicho dada wa marehemu aitwaye Dkt Easter Msuya naye akatoa wosia kwa watoto wa marehemu ambapo aliwataka kupendana na kumtanguliza Mungu katika kila jambo

Baadae Mkuu wa wilaya hiyo Jerry Muro akahitimisha kikao hicho kwa kumwaga maombi mazito huku akiishukuru familia ya Msuya kwa kuondoa shauri hilo mahakamani ili kufanya mazungumzo ya kugawanya Mali hizo na watoto warejee masomoni.
 Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Jerry Muro akisuluhisha mgogoro wa miradhi uliokuwa ukiikabili familia ya marehemu bilionea Erasto Msuya.


 Wanafamilia ya marehemu Erasto Msuya wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Ofisini kwake jana 
mkuu wa wilaya ya Arumeru Jerry Muro akimkumbatia mtoto wa marehemu Erasto Msuya kijana anaejulikana kwa jina la Kelvin Saimoni Msuya mara baada yakusuluhisha


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2pJtJnC
via
logoblog

Thanks for reading MGOGORO WA KUGOMBEA MALI ZA MAREHEMU BILIONEA ERASTO MSUYA WAPATIWA UFUMBUZI

Previous
« Prev Post