Ticker

10/recent/ticker-posts

MBUNGE KINGU ATOA MIFUKO 85 YA SARUJI KUSAIDIA UJENZI WA SHULE

Mbunge wa Jimbo la Singida Magharibi, Elibariki Kingu akihutubia katika mahafali ya kidato cha nne katika Shule ya Sekondari ya Muungano iliyopo Kata ya Iseke wilayani Ikungi mkoani Singida jana. 
Wananchi wakiwa katika mahafali hayo.
Mahafali yakiendelea.


Na Dotto Mwaibale, Singida

MBUNGE wa Jimbo la Singida Magharibi, Elibariki Kingu ametoa mifuko ya saruji 85 kwa ajili ya ujenzi wa ofisi ya Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Muungano iliyopo Kata ya Iseke wilayani Ikungi mkoani Singida.

Kingu ambaye alikuwa mgeni rasmi katika mahafali ya kidato cha nne alitoa msaada huo juzi baada ya kusomewa risala na wahitimu hao na kuelezea changamoto kadhaa za shule hiyo."Mimi kama mzazi na kiongozi nimeguswa na risala yenu natoa mifuko 85 ya saruji iweze kusaidia ujenzi wa ofisi ya mwalimu mkuu pamoja na choo" alisema Kingu.

Kingu alitumia nafasi hiyo kuwataka wahitimu hao kujiandaa kwa mtihani wao ambao watautanya hivi karibuni na kuwa anategemea watafanya vizuri.Alisema kuwa kumaliza kidato cha nne ndio safari inaanza ya kuendelea na kidato cha tano na sita hadi elimu ya juu hivyo waache michezo isiyo na maana badala yake wajikite kwa kujisomea.

Kingu aliwataka walimu na wazazi kuendelea kushirikiana ili kuwasaidia wanafunzi kutatatua changamoto zao badala ya kusubiri serikali.


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2BDjMuC
via

Post a Comment

0 Comments