Ticker

10/recent/ticker-posts

MAZIRI WA AFYA NCHI SADC KUKUTANA DAR, WAZIRI UMMY MWALIMU ATOA NENO

Na Said Mwishehe, Michuzi TV

WAZIRI Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amesema kuwa Tanzania inauwezo na utaalamu mkubwa katika kuleta matokeo chanya katika sekta ya afya na mapambano dhidi ya UKIMWI.

Mwalimu amesema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati anazungumzia maandalizi ya mkutano wa mawaziri wa afya waa nchi za Jumuiya ya Maendelelo ya Nchi za Kusini mwa SADC unaotarajia kufanyika nchini kuanzia Novemba nne hadi Novemba 8 mwaka huu.

Hivyo wakati anaelezea kuhusu mkutano huo amefafanua masuala mbalimbali na mada ambazo zitapewa kipaumbele kujadiliana na mawaziri wa afya wa SADC ,hivyo ametumia nafasi hiyo kuweka wazi kwamba Tanzania imejipanga na itatoa ushirikiano wa kutosha katika kueleza namna ambavyo nchi inafanya kuboresha sekta ya afya na mapambano dhidi ya UKIMWI.

Hata hivyo amesema kuhusu sekta ya afya na mapambano dhidi ya UKIMWI, Waziri Mwalimu amesema kauli mbiu ya mkutano wa mawaziri wa afya wa SADC inasema ushirikiano nchi za SADC ni nguzo kuu kufikia maendeleo ya sekta ya afya na mapambano dhidi ya Ukimwi.

"Kuanzia Novemba 4 hadi Novemba 8 mwaka huu nchi yetu itakuwa mwenyeji wa mkutano wa sekta ya afya ambao utafanyika jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa Benki Kuu. Nchi zote za SADC bado kunachangamoto kubwa ya maambukizi ya UKIMWI ingawa kwa Tanzania kasi ya maambukizi imepungua kutoka asilimia saba mpaka asilimia nne.

Ametumia nafasi hiyo kueleza kuwa kuna mikakati iliyowekwa kidunia katika kukonesha maambukizi ya ugonjwa,hivyo.mawaziri wa afya wa nchi za SADC watatumia mkutano huo kujadiliana kwa kina hatua za kuchukua zaidi katika eneo la mapambano ya UKIMWI.

"Kupitia mkutano huo mawaziri wa afya wataangalia wamefikia wapi katika kutekeleza malengo ya dunia,"amesema Waziri Mwalimu na kuongeza kuwa kupitia mkutano huo waatajadili kuhusu ugonjwa wa Kifua Kikuu( TB) ambao bado unasumbua.

Wakati huo huo amesema katika mkutano huo watazungumzia ugonjwa wa malaria ambao nao umekuwa ukisumbua nchi nyingi za jumuiya ya SADC."Kwa Tanzania tumefanikiwa kupungua ugonjwa wa malaria kutoka asilimia 14.7 hadi asilimia saba.Hata hivyo tunaendelea kuongeza juhudi kuhakikisha tunatokomeza malaria nchini kwetu."amesemaa.

Pamoja na mambo.mengine Waziri Mwalimu amesema Tanzania itatumia nafasi ya mkutano huo kukitangaza kiwanda cha viuadudu kilichopo Kibaha mkoani Pwani ambacho kimejikita kutengeneza dawa za kuua wadau maeneo malaria na hata wadudu wanaoeneza ugonjwa wa dengue.

Amesema watahamadisha mawaziri wa nchi hizo kununua dawa za kiwandani hapo na katika ratiba iliyopo mawaziri wa nchi hizo watambelea kiwanda hicho ili kuona uzalishaji dawa za viuadudu na zinavyofanya kazi.

Wakati huo huo Waziri Waziri Mwalimu amesema mawaziri hao watakuwa na majadiliano kuhusu nini kifanyike kukabiliana na changamoto ya udumavu kwa nchi za SADC ,hivyo wataweka mikakati katika eneo hilo.

Pia ajenda nyingine ambayo itazungumzwa na mawaziri hao ni eneo la sekta ya afya kwa ujumla ambapo watatumia nafasi hiyo kuzungumzia mikakati ya kukomesha vifo vya mama wajawazito.

"Pia kutokana na kuendelea kuripotiwa kwa ugonjwa ebora nchini Congo , mawaziri wa afya watajadiliana namna ya kukabiliana na ugonjwa huo,"amesema. 
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akizungumza na Waandishi wa Habari leo jijini Dar es Salaam kuhusu Tanzania kuwa mwenyeji wa Mkutano wa Mawaziri wa Sekta ya Afya na UKIMWI kutoka Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) unaotarajiwa kufanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Benki Kuu ya Tanzania jijini Dar es Salaam kuanzia Novemba 04 hadi 08,2019,ambapo Mkutano huo inaelezwa kuwa utafunguliwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan,Mkutano huo umebeba kaulimbiu isemayo “Ushirikiano wa nchi za SADC ni nguzo kuu kufikia Maendeleo Endelevu ya Sekta ya Afya na Mapambano dhidi ya UKIMWI”(SADC Cooperation is a Major Pillar to Sustainable Health Development and Fight Agaist AIDS).
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu (katikati) akifafanua jambo mbele ya Waandishi wa Habari leo jijini Dar es Salaam,kuhusu mambo mbalimbali kuhusu maandalizi ya Mkutano wa Mawaziri wa Sekta ya Afya na UKIMWI kutoka Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) unaotarajiwa kufanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Benki Kuu ya Tanzania jijini Dar es Salaam kuanzia Novemba 04 hadi 08,2019,pichani kushoto ni Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Zainab Chaula na kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Zainab Chaula,Mkurugenzi wa Kinga kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Leonard Subi. 
Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari MAELEZO,Zamaradi Kawawa akimkaribisha Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu kuzungumza na Waandishi wa Habari leo jijini Dar es Salaam kuhusu Tanzania kuwa mwenyeji wa Mkutano wa Mawaziri wa Sekta ya Afya na UKIMWI kutoka Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) unaotarajiwa kufanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Benki Kuu ya Tanzania jijini Dar es Salaam kuanzia Novemba 04 hadi 08,2019


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2MVHFEc
via

Post a Comment

0 Comments