MAJINA YA WALIOPATA MKOPO ELIMU YA JUU HAYA HAPA

  Masama Blog      
BODI ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imetangaza orodha ya awamu ya kwanza yenye wanafunzi 30,675 wa Mwaka wa Kwanza kwa mwaka wa masomo 2019/2020 waliofanikiwa kupata mikopo yenye thamani ya TZS 113.5 bilioni.


Akizungumza na wanahabari leo (Alhamisi, Oktoba 17, 2019) na Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB Bw. Abdul-Razaq Badru, amesema katika orodha hiyo, wanaume ni 19,632 (64%) na wanawake ni 11,043 (36%).


Badru amefafanua kuwa waombaji mikopo wafungue akaunti zao binafsi (SIPA – Student’s Individual Permanent Account) walizofungua kuomba mkopo kupitia mfumo wa HESLB (olas.heslb.go.tz) ili kupata taarifa za mikopo. from MICHUZI BLOG https://ift.tt/35JVaOx
via
logoblog

Thanks for reading MAJINA YA WALIOPATA MKOPO ELIMU YA JUU HAYA HAPA

Previous
« Prev Post