MAHFALI KIDATO CHA NNE, SHULE YA SEKONDARI MAKONGO YAFANA

  Masama Blog      
Na Karama Kenyuko, Michuzi TV

KANALI Philip Mahende wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), amewaasa wazazi nchini kuishi katika misingi bora, kushiriki katika mambo ya kijamii kwa sababu Watoto hujifunza kutokana na kile wanachofanya wazazi.

Akizungumza katika Mahafali ya Kidato cha Nne ya Shule ya Sekondari ya Makongo ya jijini Dar es Salaam leo Oktoba 19, 2019, Kanali Mahende kwa niaba ya Mkuu wa JKT, Brigedia Jenerali Charles Mbuge, amewaasa pia wazazi kutumia muda mwingi kukaa na familia zao hasa watoto wadogo ambao bado wanakua na kuweza kujifunza kwenye maadili.

Aidha amesema, Jeshi la Kujenga Taifa linazo shule ambapo linalea Wanafunzi kuanzia ngazi ya Shule ya Msingi hadi Sekondari, tumekuwa tukiwapa malezi ya aina zote, stadi za maisha stadi za kazi ujasiliamali pamoja na mbinu za kivita ili kiwajengea misingi imara ya maisha hata pale wanapokuwa wamemaliza masomo yao

Kwa upande wake, Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Makongo, Kanali Yuda Kitinya amewataka wazazi kushirikiana na walimu kuhakikisha  Wanafunzi wa Kidato cha Nne ambao hawahudhurii masomo shuleni katika kipindi kifupi kilichobakia cha kuelekea mtihani wa taifa wafike ili kuweza kufundishwa kile ambacho wamebakiza.

"Watoto wetu baadhi kwa huu muda mfupi uliobaki hawafiki shuleni, wazazi naomba tushirikiane kwa hilo, wanatafuta vituo vingine mitaani, inatuwia vigumu. Mwalimu amepanga kwa ajili ya kumalizia vile anavyoona vitakuwa vigumu, halafu mtoto ametafuta mwalimu mwingine mitaani ambae hamjui udhaifu wala uwezo wake, kwa hiyo yeye atamfundisha akimhakikishia kuwa yeye ni mwalimu bora kuliko wote hapa Da es Salaam kumbe anamlia pesa zake". Amesema Kanali Kitinya


Amewaambia wanafunzi hao kuhakikisha wanautumia muda mfupi uliobaki kujisomea ili waweze kufaulu katika mtihani wao.

Amesema wamekuwa wakitumia mbinu mbal mbali ili kuweza kuwafikisha wanafunzi hao mahali pale wakiamini kuwa wakizifuata na kizishika mbinu hizo basi wote wataweza kufaulu na kuongeza kuwa katika wiki mbili zilizobaki watahakikisha wanarekebisha pale ambapo watakuwa hawajajiweka vizuri ili kuwawezesha kufanya mitihani yao kwa ufanisi mkubwa.

Mbali na elimu pia tumewajenga kitabia na nidhamu na tumewajengea, ukakamavu na stamina ili kufanya miili yao iwe na nguvu na kutumia vizuri muda wao ndio maana kuna maeneo hapa shuleni hawaruhusiwi kutembea isipokuwa kukimbia".

Ameongeza kuwa, shule ya Makongo pia imekuwa ikishiriki katika michezo mbali mbali kwa mafanikio makubwa ambapo imekuwa ikiongoza kwenye michezo mbali mbali kwa kupitia shule yenyewe ama timu ya mkoa wa Dar es Salaam kwa kuwa wanafunzi wake wame wakishiriki na mpaka sasa kwa miaka mitano mfululilzo shule hiyo imekuwa ikiongoza na kutoa wawakilishi kitaifa.

Aidha amesema kuwa, uongozi wa shulenhiyo umekuwa ukijitahidi kuboresha maeneo mbali mbali japo kazi ya kuboresha miundombinu shuleni hapo ni kazi ngumu ila

Kanali Kitinya amesema shule hiyo inajabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo tatizo la ufinyu na uchakavu wa maktaba ya shule eneo ambalo ni muhimu sana kwa mahitaji ya shule kwani jengo letu ni dogo na linahitaji marekebisho.

Pia màabra zetu ni za zamani, zinahitaji kufanyiwa marekebisho makubwa ama kujengwa mpya. Pia madarasa yetu ni ya muda mrefu kwani kama mnavyojua Makongo ilianza zamani sana majengo yamechoka na yanahitaji ukarabati mkubwa.

Ameongeza kuwa, shule imekuwa na changamoto kubwa ya usafiri safiri hasa kwa wanafunzi wa kutwa ambao wamekuwa wakipatwa na adha mbali mbali hususani kipindi cha mvua. "Hosteli yetu ni ndogo na haitoshelezi wanafunzi wote, wanafunzi wa nje wanakuwa na changamoto ya usafiri hasa kipindi cha mvua..., tunataka wanafunzi haww waweze kufika shuleni kwa urahisi wakiwa hawajachoka na kupata muda mzuri wa kusoma na kufundishwa,amesema.

"Tunatarajia watoto hawa baada ya kumaliza mitihani yao na kwenda uraiani watakuwa mabalozi wazuri na wanajamii safi, hatutegemei mmoja akakamatwa na polisi kwamba kafanya jambo baya, ama akawekwa gerezani...,tunaamini kww elimu waliyoipata hapa basi wote watakuwa ni wazalishaji wa kutegemewa kuanzia nyumbani mpaka jamii nzima inayowazunguka" amesema Kanali Kitinya.


Kwa upande wake mwalimu wa Taaluma kapteni Rajabu Mohamed amesema, anaamini wanafunzi wote wanaomaliza kidato cha nne watapata ufaulu kwa alama za juu kwa kuwa taaluma waliyokuwa wakiwapatia ni bora kwani walikuwa wakihakikisha wanajisome kwa kuwapatia mitihani mara kwa mara.

"Tunatarajia wanafunzi hawa watapata matokeo bora hivyo ninawasii wazazi wasisite kuleta watoto wao Makongo Sekondarikwani hapa mbali na kuwapatia elimu pia tunawalea kwa nudhami bora, utimamu na kuwashirikisha katika michezo mbali mbali.
 Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Makongo (Mwenye sare za Jeshi), Kanali Yuda Kitinya akizungumza katika Mhafali hayo ya Kidato cha Nne shuleni hapo aambapo amewataka wazazi kushirikiana na walimu kuhakikisha  Wanafunzi wa Kidato cha Nne ambao hawahudhurii masomo shuleni katika kipindi kifupi kilichobakia cha kuelekea mtihani wa taifa wafike ili kuweza kufundishwa kile ambacho wamebakiza.
  Vijana wa Skauti katika Shule ya Sekondari ya Makongo wakionyesha Ukomando mbele ya Mgeni rasmi.
KANALI Philip Mahende wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) akizungumza kwa niaba ya Brigedia Jenerali Charles Mbuge, amewaasa wazazi kutumia muda mwingi kukaa na familia zao hasa watoto wadogo ambao bado wanakua na kuweza kujifunza kwenye maadili. , amewaasa wazazi nchini kuishi katika misingi bora, kushiriki katika mambo ya kijamii kwa sababu Watoto hujifunza kutokana na kile wanachofanya wazazi.from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2VWqlla
via
logoblog

Thanks for reading MAHFALI KIDATO CHA NNE, SHULE YA SEKONDARI MAKONGO YAFANA

Previous
« Prev Post