Ticker

10/recent/ticker-posts

KOCHA MKUU TAIFA STARS AELEZA ANAVYOWAPATA WACHEZAJI WAKE,AGUSIA WALIOKO NJE YA NCHI

Na Said Mwishehe, Michuzi TV

KOCHA Mkuu wa Timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' Etienne Ndayiragije amefunga kwa kueleza mambo mbalimbali kuhusu timu ya Taifa huku akitumia nafasi hiyo kueleza vigezo anavyotumia kuwapata wachezaji wa timu hiyo.

Akizingumza leo Oktoba 31 katika mahojiano maalumu kati yake na watangazaji wa kipindi cha Sport Arena kinachorushwa na kituo cha redio cha Wasafi FM Kocha Mkuu wa Taifa ya Tanzania amesema yeye anao mfumo wake ambao anatamani kuona wachezaji wanautumia kupata mafanikio ya timu na ushindi kwa mechi wanazokutana nazo.

Hivyo amesema ili kupata kikosi kizuri amekuwa akifuatilia taarifa za wachezaji na vilabu wanavyochezea na hivyo anakuwa na taarifa za kutosha za kila mchezaji na uwezo wake wa soka uwanjani.

Amesema pamoja na mambo mengine yeye anapenda kuwa na wachezaji ambao mashambulizi yanaanza kwa mlinda mlango ili kuhakikisha wachezaji wanapeleka mashambulizi kwa timu mpinzani.Pia anapenda kuwa na wachezaji wenye uwezo wa kumiliki mpira kwani hiyo inasaidia kupanga mipango ya kushinda.

"Ili kupata wachezaji hao lazima ufuatilie kwa karibu kwenye klabu wanazochezea na nafasia ambazo wanapewa na baada ya hapo naangalia nimuite nani na kwa wakati gani na kubwa zaidi hawa naangalia na pia muungano wa wachezaji kati ya mchezaji mmoja na mwingine ukoje?

"Hata hivyo tukubali kuwa muda wa kuita wachezaji unakuwa mfupi kulingana na ratiba zinapotolewa, lakini cha pili ninaita wachezaji kulingana na mahitaji ya wakati huo na timu ambayo tunakutana nayo kwenye michuano.Naamini kuna wachezaji wengi ambao bado hawajapata nafasi ya kuitwa Taifa Stars lakini naamini wakati utafika,"amesema.

Ameongeza kuwa pamoja na kuita wachezaji kutokana na uwezo wanaoonesha kwenye vilabu vyao anatambua kuwa timu ya Taifa inacheza michuano ya kimataifa, hivyo lazima awe anapata wachezaji ambao wanatoka pia kwenye vilabu ambavyo vinashiriki michuano ya kimataifa mara kwa mara ambapo ametolea mfano wa klabu za Yanga, Azam FC na Simba.

Alipoulizwa kwanini kwenye timu ya Taifa anaita zaidi wachezaji wa klabu ya Simba na Azam kuliko wa kutoka vilabu wengine, Kocha Ndayiragije amejibu kuwa anaamini huwa anachukua Watanzania kwa ajili ya kuisaidia timu yetu ya Taifa"Huwa nachukua wachezaji Watanzania na si vinginevyo."

Kuhusu kuwaita na kuwachezesha wachezaji walioko nje ya Tanzania, Kocha huyo amejibu kuwa anatamani wote wawepo kwenye timu ya Taifa ili kusaidia na kutoa mchango wao lakini mazingira ya rariba kwa wachezaji hao inakuwa ngumu kuwepo kikosini.

"Nimekuwa naita wachezaji walioko nje lakini changamoto kubwa ni muda, hivyo tunakosa nafasi ya kutosha ya kuepena maelekezo.Hivyo ninajaribu kuangalia kipindi cha Desemba ambako ligi nyingi zinakuwa kwenye mapumziko ambako tutaita wachezaji walioko nje ili tuje tujumuike pamoja na hapo tutakuwa na uhakika wa nani ni nani na anaweza kusaidia vipi tumu yetu.

"Hivyo ni suala la muda tu lakii natambua na kuthamini mchango wachezaji wa nje na nafuatilia kila mchezaji huko aliko,"amesema Kocha huyo wakati anazungumza kwenye kipindi hicho.


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/36lmRgU
via

Post a Comment

0 Comments