KIGWANGALA ATOA SIKU SABA KWA MANAIBU KATIBU WAKUU NA KATIBU MKUU KUWASILISHA MCHAKATO WA MSWAADA WA SHERIA UUNDWAJI JESHI USSU

  Masama Blog      
Gwaride la wahitimu wa mafunzo ya jeshi ussu wakipita mbele ya Waziri wa utalii na maliasili katika sherehe hizo.
Mmoja wa wahitimu wa mafunzo ya awali ya jeshi ussu akipita juu ya kamba katika moja ya maonesho yaliyofanyika mbele ya waziri wa utalii na maliasili Mhe.Khamis Kigwangaka katika sherehe ya kuhitimisha mafunzo hayo

Na Jusline Marco-Arusha

Waziri wa maliasili na utalii Dkt.Khamis Kigwangala ametoa siku saba kwa manaibu katibu wakuu na katibu mkuu wa wizara hiyo kuwasilisha mchakato wa mswada wa sheria ya uundwaji Jeshi Ussu ofisini kwake ili iweze kuwasilisha bungeni.

Ametoa agizo hilo katika sherehe za kuhitimisha mafunzo ya Awali ya Jeshi Ussu katika kituo cha mafunzo cha Mbulu-mbulu kilichopo katika kata ya Kambi ya simba,Wilayani Karatu Mkoani Arusha.

Dkt.Kigwangala amesema kuwa kutokukamilika kwa mswada huo ni mapungufu ya wizara kwani amekuwa akielekeza mara kadhaa mswada huo ukamilike na umekuwa haukamilishwi.

"Katika maagizo niliyopewa na Mhe.Rais sikusudii kujiona nikitumbuliwa kwasababu ya kuchelewa kutimiza wajibu wangu,"Alisema Dkt.Kigwangala huku akiongeza kuwa kama ni madokezo ameandika mara kadhaa lakini wamekuwa wakijivuta.

Ameongeza kuwa kwa  zaidi ya miaka kumi tangu ilipoelekezwa na sheria ya uhifadhi ya wanyamapori haijawahi kuanza ila kwasasa taasisi mbalimbali za uhifadhi wa wanyamapori zimeanza kuonyesha bidii katika kuwapatia mafunzo wafanyakazi wao kwenye eneo la Jeshi Ussu.

Vilevile ametoa jukumu kwa bodi ya mamlaka ya uhifadhi wa wanyamapori Ngorongoro kupeleka ushauri wa mapendekezo yaliyotolewa ya kufanya kiwtuo hicho kuwa kamili kwa kuangalia vigezo vyote vitakavyowezesha kufanya kituo hicho kuwa kituo cha kudumu.

Awali akitoa risala yake kwa mgeni rasmi  mkuu wa kutuo hicho Kanali Martin kilugha  amesema kuwa jumla ya wahitimu wa mafunzo hayo ni 112 ambapo katika mafunzo hayo wakufunzi wa ndani wametumika,wakufunzi wa hifadhi pamoja na wakufunzi wa muda kutoka katika jeshi la JWTZ kwa ajili ya kuimarisha Jeshi Ussu.

Amesema kuwa wahitimu hao wamefundishwa mafunzo mbalimbali ya uhifadhi ikiwemo utimamu wa mwili,na ulinzi wa nadharia na vitendo na kufaulu kwa madaraja mbalimbali.

Kwa upande wake mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe.Mrisho Gambo amesema kuwa kumekuwa na matukio mengi ya ujangili ya kuuawa kwa wanyama hivyo wahitimu wa mafunzo hayo wanapaswa kufahamu kuwa wanajukumu kubwa la kuhakikisha wanalinda rasilimali za nchi.

"Niwaomba wahitimu walio chini ya uongozi wako Mhe.Waziri wakapambane na ujangili ili kukomesha mchezo huo na rasilimali za nchi ziweze kuwa salama kwa faida ya wananchi kwani huo ndio msimamo wa Rais wetu ndiyo maana ameridhia tuende kwenye mfumo wa kijeshi kama sehemu yake ya kuonyesha dhamira ya kupambana na ujangili na kulinda rasilimali zetu".Amesema  Mkuu huyo.


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/30YiPaw
via
logoblog

Thanks for reading KIGWANGALA ATOA SIKU SABA KWA MANAIBU KATIBU WAKUU NA KATIBU MKUU KUWASILISHA MCHAKATO WA MSWAADA WA SHERIA UUNDWAJI JESHI USSU

Previous
« Prev Post