Kanisa la Arusha Praise center laandaa maombi ya kuombea Taifa

  Masama Blog      
Na woinde shizza, Michuzi blog, Arusha
TAASISI ya Kanisa la Arusha Praise Center  limeandaa Maombi makubwa ya kuliombea Taifa kwa ajili ya uchaguzi mkuu na amani ya nchi litakalofanyika tarehe 17 mwezi wa November jijini Arusha kwenye ukumbi wa Hotel ya Mount Meru eneo la kata ya Sekei jijini hapa.

Akizungumza na waandishi wa habari Askofu wa kanisa hilo Aminiel  Mgonja alisema kuwa Kongamano hilo litaenda sambamba na kuombea nchi hususani kuona umuhimu wa wananchi kuchagua na kuchaguliwa wakiwa kwenye Amani na utulivu.

Amesema Taifa lolote lisilo na Amani na utulivu haliwezi kuwa na uchaguzi huru na haki hivyo kwetu sisi kama watanzania ndio tumeona tuliombee taifa letu wakati huu linaenda kwenye uchaguzi mkuu wa serikali za mitaa na baadae uchaguzi wa madiwani wabunge na Rais hapo mwakani.

Ameeleza kuwa kwa msingi huo ili kuwapata viongozi lazima wapewe kibali na Mungu ndio maana tumekuwa na utaratibu wa kuchagua viongozi kila baada ya miaka mitano hivyo maombi yetu ni kuombea taifa letu wakati huu tunapoenda kuchagua viongozi.

“Niwasihi sana viongozi wetu na watanzania kuona umuhimu wa kujiandikisha kwa ajili ya uchaguzi wa serikali za mitaa utakaofanyika mapema mwaka huu na mwakani sisi tumejipanga kuombea taifa kupita salama kwenye chaguzi hizi”

Amesema kuwa maombi hayo yatawashirikisha wadau mbali mbali wakiwemo viongozi wa serikali akiwemo Mkuu wa mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo na mkuu wa wilaya ya Arumeru, Jerry Muro pamoja na masheikh na Maaskofu wa makanisa ya KKKT Katoriki na madhehebu mbalimbali.

Kwa upande wake Mratibu wa Tamasha hilo la kuombea uchaguzi Mkuu, Zacharia Isack amesema kuwa tamasha hilo ni sehemu ya kuwaleta jamii kuwa wamoja wakati huu tunapoelekea kwenye uchaguzi mkuu wa serikali za mitaa.

Amesema kuwa wanatoa rai kwa jamii ya mikoa ya kaskazini bila kujali itikadi zao kushiriki kwa pamoja kwenye tamasha hilo ambalo limelenga kuliombea taifa Amani na utulivu kwenye kipindi cha uchaguzi mkuu na hakutakuwa na malipo kwenye tamasha hilo.

Amesema kuwa mziki wa injili ndio utabeba tamasha hilo na wamejipanga sana kuwapokea wageni hao kwa ajili ya tamasha hilo katika ukumbi wa Hotel ya Mount Meru na kuwataka watu wa dini zote kujitokeza kuja kuliombea taifa lao kipindi hichi cha uchaguzi wa Serikali za mitaa na baadae uchaguzi mkuu 2020.

Mkurugenzi wa Kismart Media ya Jijini Arusha Mary Mollel amesema kwamba tamasha hilo litabeba vyombo vya habari kwa lengo la kutoa taarifa kwa jamii juu ya kuombea Amani pamoja na kufikia uchaguzi wenye amani na utulivu
Askofu wa kanisa la Arusha Praise center,  Aminiel  Mgonja akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jijini Arusha.


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2pCSbqG
via
logoblog

Thanks for reading Kanisa la Arusha Praise center laandaa maombi ya kuombea Taifa

Previous
« Prev Post