Ticker

10/recent/ticker-posts

JUKWAA LA MABADILIKO YA TABIANCHI WAISHAURI SERIKALI KUONGEZA FEDHA KATIKA SEKTA YA NISHATI JADIDIFU

Na Penina Malundo

JUKWAA la Mabadiliko ya Tabianchi limeishauri Serikali kutoa kipaumbele katika eneo la nishati jadidifu kwa kutengaji wa bajeti ya kutosha kwa lengo la kusaidia kupambana na athari za mabadiliko ya tabianchi.

Hayo yamesemwa jana jijini Dar es Salaam na Mratibu wa Mradi wa masuala ya nishati jadidifu unaofadhiliwa na Shirika la Hivos kutoka Jukwaa la Mabadiliko Tabianchi(FORUMCC) ,Euphrasia Shayo wakati wa mkutano wa wadau mbalimbali wakiwemo vijana,wanawake pamoja na kundi la watu walemavu waliokutana na kujadili masuala ya nishati jadidifu zinavyoweza kupunguza mabadiliko ya tabianchi.

Amesema kila mwaka fedha nyingi zinatengwa katika nishati ambazo sio jadidifu ikiwemo nishati ya makaa ya mawev ambapo bajeti ya mwaka 2016/17 inaonyesha ilitengewa asilimia 35 huku kwa nishati jadidifu ilitengewa asilimia 5 tu ya bajeti.

“Katika bajeti ya Serikali inayowekwa kila mwaka pesa nyingi zinakwenda kwa nishati za kawaida ambazo asilimia kubwa ndo zinaleta mabadiliko ya tabianchi na sio kwenye nishati jadidifu ambapo wafadhili wanaweka fedha ili kuweza kupunguza kasi ya kuwepo kwa mabadiliko ya tabianchi,”amesema.

Ameongeza kwamba wanataka Serikali iweke kipaumbele katika masuala ya nishaji jadidifu kwani bajeti ya mwaka 2016/17 waligundua Serikali ilitenga asilimia 30 ya kupata nishati kwa kupitia makaa ya mawe ambayo yanaleta mabadiliko ya tabia nchi huku kwa nishati jadidifu ilitenga asilimia 5 tu, hivyo wanatamani katika suala la nishati jadidifu bajeti yake ifike hata asilimia 50.

Ameongeza kuwa nishati jadidifu ni nishati inayotokana na mwanga wa jua,upepo na wakati mwingine maji na nishati hiyo inachafua mazingira kwa asilimia ndogo ukilinganisha na nishari ya Mkaa,Kuni na makaa ya mawe ambapo uchafua mazingira kwa asilimia kubwa na kusababisha mabadiliko ya tabianchi.

“Tumeingia katika mradi huu wa masuala ya nishati jadidifu unaofadhiliwa na Shirika la Hivos kutoka nchini Nethaland kutokana na nishati jadidifu kuwa ni moja ya njia ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi hivyo imeweza kutufadhili kwa kutoa elimu ipasavyo juu ya umuhimu wa nishati jadidifu,”amesema.

Aidha amefafanua kuwa asilimia kubwa ya watumiaji wa nishati nchini ni wakinamama, hivyo Shirika lao litaweza kutengeneza jukwaa la pamoja lenye kuzungumza sauti ya pamoja itakayotoa nafasi ya Serikali kufanya kitu cha kuweza kusaidia nishati jadidifu inatumika ipasavyo.

“Tanzania maeneo yake mengi hayana nishati ya umeme wa kutosha na hii inafanya watu wengi kutofikiwa na nishati hiyo hivyo endapo jitihada zikiwekwa na Serikali ikawezesha nishatijadidofu kutumika ipasavyo hususani vijijini itaweza kusaidia mazingira kuwa safi na salama,”amesema

Kwa Upande wake Mratibu wa Mradi wa kushawishi Benki ya Maendeleo ya Afrika kuelekeza uwekezaji kwenye sekta ya nishati jadidifu unaotekelezwa katika nchi sita ambao unafadhiriwa na Christiani Aid kupitia African Climate Justice Alliance (PACJA),Msololo Onditi alisema Jukwaa lao la ForumCC kwa sasa linatekeleza mradi wa pili unaohusiana na nishati jadidifu.

Amesema matumizi makubwa yanayotumiwa na watanzania ni matumizi ya nishati ya kuni na mkaa ambayo asilimia kubwa yanasababisha mabadiliko ya tabianchi hivyo uwekezaji mkubwa wa nishati jadidifu utaweza kusaidia kumudu utumiaji wa nishati safi.

“Kupitia mradi huu tunajengeana uwezo kama asasi za kiraia kupitia nishati jadidifu katika mazingira ya mabadiliko ya tabianchi na kushawishi watendaji wa Serikali kuwa na sera mikakati na mipango ambayo itavutia uwekezaji mkubwa katika upande wa nishati jadidifu,”amesema Onditi.

Amefafanua bado nchi haina sera wala mkakati unaosimama na kuongoza katika matumizi la nishati Jadidifu kwani sera iliyopo ni ile ya nishati ya jumla kwa sasa.

Hata hivyo wadau wa Jukwaa la mabadiliko ya tabianchi wamezungumzia kwa kina umuhimu wa Serikali kuweka sera maalum ambayo itasimamia nishati jadidifu kwani kwa sasa kuna sera moja tu ambayo inahusu nishati kwa ujumla na hivyo kuonekana kwa usimamizi mzuri wa nishati jadidifu na hivyo wanaishauri Serikali kuweka sera inayojitegemea katika sekta hiyo.
Wadau wa Jukwaa la mabadiliko ya tabianchi wakiwa makini kufuatilia mada mbalimbali wakati wa mkutano maalum uliowakitanisha wadau hao jijini Dar es Salaam chini ya.mwamvuli wa Jukwaa la FORUMCC


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/3684fAL
via

Post a Comment

0 Comments